Kijana unayejitafuta kimaisha, katika utafutaji wako Zanzibar iweke namba moja

Kijana unayejitafuta kimaisha, katika utafutaji wako Zanzibar iweke namba moja

Papaa Gx

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
11,097
Reaction score
17,929
Habari zenu

Naomba kuwapa nasaa kidogo vijana wa kiume na kike wanao jitafuta kimaisha. Hapa nitapenda kufikisha ujumbe huu kwa vijana wote wanao jitambua na kuelewa nini wanatakiwa kufanya katika dunia hii. Vijana wote wenye malengo na ndoto nzuri za kupiga hatua moja kwenda nyingine naomba msome kwa makini maandishi haya kisha utachanganya akili zako mwenyewe.

Nimepata muda wa kuitembelea Zanzibar na kugundua kuwa inawafaa sana vijana ambao wako katika utafutaji wakipambania kufika hatua fulani. Asilimia kubwa ya watu wamekuwa wakitaja maeneo mbalimbali ya kiutafutaji na kuacha kuisemea Zanzibar ambayo vizuri kabisa kwa kijana aliye makini. Vijana ambao mmekuwa mkilalamika kuhusu kukosa mitaji hali inayo pelekea kushindwa kufanya shughuli mzipendazo basi Zanzibar ni mahala sahihi kwa kutafutia mtaji.

Eneo kubwa la pwani ya Zanzibar limezungukwa na Hoteli, hali hii imepelekea vijana wengi kupata ajira katika vitengo mbalimbali. Sasa basi dhumuni langu liko hapa, kwenye hizo hoteli kuna vitengo vingi sana mfano, House Keeping, watu wa mapokezi, wapishi, mafundi, walinzi, watu wa swimming pool, wahudumu, watu wa bar, watu wa usafi, watu wa bustani nakadhalika nakadhalika. Vitengo hivyo vinahitaji uwe na uelewa navyo ama taaluma.

Taaluma ama uelewa utaupata huko huko hotelini muhimu ni kuchukua maamuzi. Kuliko kuendelea kulaumu na kulalamika vijana chukueni maamuzi magumu. Iko hivi kwenye hizo hoteli kuna baadhi ya vitengo mafunzo hutolewa kwa muda wa miezi mitatu kisha wakikuona uko vizuri utapata ajira na kuanza kula mshahara. Pia utapata cheti cha kuhitimu mafunzo ambapo tofauti na hapo unaweza kwenda hoteli nyingine na ukapata ajira.

Vijana tokeni, kwenye kutoka unaweza pata madili. Zanzibar iwekeni namba moja kwenye utafutaji, nenda jipe muda kisha pambana. Nimeandika kwa ufupi kutokana na muda hauruhusu, hivyo nitajibu kama utakuwa na swali lolote. Karibu
 
Anaesikia na asikie, kuna kazi nimeifanya juzi ya kusafisha shamba la mzungu nimeingiz 75k a day. Ni kazi gn dar utaipata ya kulipwa hiyo hela kwa siku
Binafsi nilishaamua long time lazima nije Zanzibar kupiga vibarua vya ujenzi Ili nipate nauli ya kwenda Ukraine kwenye ujenzi baada ya vita kuisha.
 
Back
Top Bottom