Mkuu, ni jambo jema kama ungedadavua hizo gharama
Zanzibar fursa kubwa ni ujenzi plus utalii.Hizi shughuli zimebeba mnyororo mkubwa sana wa kiuchumi.
Shughuli nyingi za ujenzi hufanyika shamba.
Paje,
Nungwi na
Kiwengwa ndiyo shamba kubwa kwa Unguja na pia ndizo vitovu vikubwa vya utalii.
Watu wengi hutoka mjini na kuja kufanya shughuli zao shamba.Kawaida kibarua hulipwa
tsh 15000-20000 kwa kutwa wakati fundi hulipwa tsh
30000-50000 kwa kutwa.
Nauli plus msosi huwa ndiyo kikwazo hasa kwa kibarua, fundi huwa hapati kikwazo sana.Minimum nauli ni
tsh 5000 kwenda na kurudi na msosi ukijibana ni
tsh 5000 kwa siku.
Hapo bado kodi ya chumba plus umeme coz maji sehemu nyingi ni bure na wana msemo wao
'maji ni ya Mungu'!Viburudisho kama bando ni muhimu coz hizi kazi zinategemea sana mawasiliano!
Kupitia mchanganuo huo hapo juu, unaweza kuona jinsi kujichanga kunavyokuwa na changamoto zake (siyo kama haiwezekeni)hasa kwa kibarua.
Ukibahatika kazi za mjini ambazo huwa chache minimum msosi plus nauli ni
tsh 5000 ukijibana.Pia ukibahatika japo (ni ngumu kupata) site za kulala, pia husaidia kujibana, mara nyingi hizi site kama ni kubwa hulindwa na vikosi.
Unatakiwa ufanye nini?? (kibarua)
1) Chukua chumba shamba bei huanzia
50000-
100000.
2) Punguza (piga ndefu) kula na kunywa maji plus juisi na energy. Utaweza?? Kazi zako zinategemea nguvu kwa asilimia 100%
3) Vumilia kwa muda mpaka ukiwa fundi coz ukiweka nia ni muda mfupi kwani faida utakayokuwa nayo fundi wako atakuelekeza kwa vitendo zaidi .
Kama kichwa ni chepesi ndani ya miezi mitatu mpaka sita utakuwa umeiva iwe kwenye tofali, mbao,chuma,tiles,umeme n.k, hakuna notisi ni vitendo tu! Fundi kwa
30000-50000 kwa siku una uwezo wa kufanya chochote!