Kijana unayepambana kimaisha using'ang'anie kuishi uswahilini

Kijana unayepambana kimaisha using'ang'anie kuishi uswahilini

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Kijana unaepambana kimaisha ukipata auheni kidogo hama huko uswahilini, hasa hasa jiji la Dar es Salaam, uswahilini ya Dar es salam ni milango ya kuzimu ..watu wamechoka, watu wamekata tamaa, Jana yao ni Bora sana kuliko Leo.

Mwanyamala kwa kopa, Manzese, Tandika, Mbagala sehemu sehemu. kuendelea kukaa uswahilini kunafunga liziki zako

Kumbuka uswahilini ndio sehemu pekee watu hushindana Kula vizuri Na hapana lingine wanalofikiria..
 
Kijana unaepambana kimaisha ukipata acheni kidogo hama huko uswahilini,hasa hasa jiji daressalam, uswahilini ya daressalam ni milango ya kuzimu ..watu wamechoka, watu wamekata tamaa, Jana yao ni Bora sana kuliko Leo .. mwanyamala kwa kopa, manzese, tandika ..mbagara sehemu sehemu.. kuendelea kukaa uswahilini kunafunga liziki zako ..kumbuka uswahilini ndio sehemu pekee watu hushindana Kula vizuri Na hapana lingine wanalofikiria..
Una hoja, lakini uswahilini ndio kuna supu za jero, maharagwe jero, pande la muhogo 100, yani ukiwa na buku uswahilini asubuhi breakfast unapata, ukiwa na buku mbili unapiga breakfast ya kifahari.

Sasa unapotaka wahamie wakati wanajitafuta wataweze breakfast za shilling 5000 na kuendelea?
 
Nakazia! Gongolamboto, buguruni, mobondenibondeni kimara na mbezi acha kabisa! Uswahilini na uchawi ni ndugu
 
Una hoja, lakini uswahilini ndio kuna supu za jero, maharagwe jero, pande la muhogo 100, yani ukiwa na buku uswahilini asubuhi breakfast unapata, ukiwa na buku mbili unapiga breakfast ya kifahari.

Sasa unapotaka wahamie wakati wanajitafuta wataweze breakfast za shilling 5000 na kuendelea?
Hapo hamna mlo ni kujaza tumbo tu na ukizoea hivyo unakuwa mtu cheap sana.
 
umesahau ulikotoka, hujui unakokwenda

umepata kiburi kuona kipato kimepanda

cc my chemchem ya furaha ephen_
Sio hivyo mkuu! Mimi mwenyewe wakati najitafuta geto langu la kwanza lilikuwa gongolamboto mzambarsauni! Si kwauswahili huo! Nikaamia sinza potelea mbali nikishindia mihogo chpsi dume! Uamuzi uu ulinisaidia sana
 
Sehemu yoyote utakayoishi hapa Tanzania zingatia kitu kinaitwa Authentic Life ( Kuishi maisha yako) na sio kuiga na kufata mkumbo.

Uswahilini kuna watu wamejenga maghorofa ,biashara wanafanya and everything is on map .

Kufanikiwa huwa ni mchakato wa kujua Unataka nini tu na kuanza kupambania na kufanyia kazi.

Then unabidi kuelewa -uswahili watu wengi hawafanikiwi wala kujipata ni kwa sababu wanakuwa Vulnerability (kushambulika ,kimwili ,kiakili kiroho)

Mfano , Ngono ,pombe ,kamali, bangi, kuacha shule na mimba zisizo na baba yote hii humpata MTU ambaye anaishi maisha ambayo sio yake.

Hivyo mkuu , uswahili ni kama ilivyo ushuwani ukiweza kuishi Authentic life - maisha yako halisi Genuine maana yake hata uishi na wazinzi ,walevi ,wezi ,wavuta bangi Ila bado hautokuwa vulnerability na kutoka mchezoni.

Mambo ya lango la kuzimu ni maneno yanayotamkwa na watu wajinga huwezi kuita sehemu lango la kuzimu wakati wengine katika hilo lango wametoboa na wanaishi vizuri
 
Kijana unaepambana kimaisha ukipata acheni kidogo hama huko uswahilini,hasa hasa jiji daressalam, uswahilini ya daressalam ni milango ya kuzimu ..watu wamechoka, watu wamekata tamaa, Jana yao ni Bora sana kuliko Leo .. mwanyamala kwa kopa, manzese, tandika ..mbagara sehemu sehemu.. kuendelea kukaa uswahilini kunafunga liziki zako ..kumbuka uswahilini ndio sehemu pekee watu hushindana Kula vizuri Na hapana lingine wanalofikiria..
Ni maeneo ambayo ukiwa wewe ndo umekulia utaelewa kwanini wakizipata bado hawaamini.
Maisha ya kila mtu ni kichekesho kwa mwengine. Kuna sintofahamu kwenye ile mitaa mpka tuliofanikiwa kuchomoka tunasema ni kwa kudra za mungu.
 
Back
Top Bottom