Kijana unayepambana kimaisha using'ang'anie kuishi uswahilini

Ni kweli mkuu uswahilini kuna changamoto kibao, kelele nyingi na kufuatiliana maisha

Yataje basi maeneo ambayo hayana uswahili ili watu wayatambue.
 
Well said Mkuu

Ila kwanini kijana akiwa na hiyo authentic life kama ulivyoieleza then akiwa anaish uswahilini anakutana na changamoto sana hususa kwa wanaomzunguka?
 
Well said Mkuu

Ila kwanini kijana akiwa na hiyo authentic life kama ulivyoieleza then akiwa anaish uswahilini anakutana na changamoto sana hususa kwa wanaomzunguka?


Changamoto sio kitu kibaya maana changamoto ndo zinamfanya MTU kuwa imara .

Kikubwa inapotekea changamoto yoyote ukiwa uswahilini usiikimbie Ila jikite kutafuta majibu zaidi .

Na changamoto huwa inawagawa watu katika pande mbili survival and victim.

Mfano ukiwa unaishi uswahili , unaweza kupitia changamoto Kama kuibiwa , uchawi , chuki , kisa tu Una I shi authentic life Ila Mwisho wa siku unabidi wewe kuwa mkubwa kuzishinda changamoto na ndo utaitwa survival Ila ukikubali hizo changamoto zikutoe mchezoni utaitwa victim mwathirika.

So Authentic ni silaha ya kuzishinda changamoto .

NB : tunapozungumzia usiige wala kufata mkumbo ni katika maisha yako Ila mambo chanya Kama biashara ,kazi n.k unaweza kuiga.
 
Uswazi huko yani ni vigodoro kwenda mbele,mipasho, wananchi hawawazi maendeleo ni vijiwe tu, huko uswazi full kurogana, wuvu, husda, kuibiana ma bwana, matusi kiujumla hakuna maadili watoto wala sio kwa wakubwa ni matusi kwenda mbele, watu wanaokaa huko hawana ustaarabu kama wewe ni mstaarabu huko hakukufai
 
Sio hivyo mkuu! Mimi mwenyewe wakati najitafuta geto langu la kwanza lilikuwa gongolamboto mzambarsauni! Si kwauswahili huo! Nikaamia sinza potelea mbali nikishindia mihogo chpsi dume! Uamuzi uu ulinisaidia sana
Kaa sehemu unapata changamoto za kukua ki akili sasa uswahilini unatoboaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…