Kijana wa Congo abuni biashara ya kipekee, atoza watu shilingi elfu moja kumchapa kofi, wengi wavutiwa na ubunifu wake

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Wakati vijana wengi katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wakilalamikia changamoto ya ukosefu wa ajira, kijana mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameibua wazo la kipekee la kujipatia kipato kupitia ubunifu wake.

Kijana huyo ameamua kuruhusu watu kumchapa kofi kichwani kwake palipo nyolewa kipara, ambapo kila kofi analopigwa humuingizia kiasi cha fedha. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtu anayehitaji kushiriki katika shughuli hiyo hulipa buku moja kwa kila kofi analompiga.

Mbinu hiyo imevutia maelfu ya watu ambao wamejitokeza kushiriki na kumpa kijana huyo fedha, huku wengi wakimpongeza kwa ubunifu wake wa kutumia hali iliyopo kutengeneza fursa ya kiuchumi badala ya kusubiri ajira rasmi.

Kitendo hicho kimezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya watu wakisema ni mfano wa namna vijana wanavyoweza kutumia ubunifu kujiajiri, wakati wengine wakitazama zaidi upande wa usalama na afya kutokana na aina ya biashara aliyoichagua.
Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1BpsAnYZcR/
 
Tuna tatizo kubwa sana hili bara letu la giza.
 
Nakumbuka tukiwa form one Kuna jamaa nilikua namchapa kiboko mia, sharti langu ilikua iwe mbele za watu tukitoka shule, nilikua Nampa 500 namchapa viboko vi5
 
Wakati vijana wengi katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wakilalamikia changamoto ya ukosefu wa ajira, kijana mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameibua wazo la kipekee la kujipatia kipato kupitia ubunifu wake.

Kijana huyo ameamua kuruhusu watu kumchapa kofi kichwani kwake palipo nyolewa kipara, ambapo kila kofi analopigwa humuingizia kiasi cha fedha. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtu anayehitaji kushiriki katika shughuli hiyo hulipa buku moja kwa kila kofi analompiga.

Mbinu hiyo imevutia maelfu ya watu ambao wamejitokeza kushiriki na kumpa kijana huyo fedha, huku wengi wakimpongeza kwa ubunifu wake wa kutumia hali iliyopo kutengeneza fursa ya kiuchumi badala ya kusubiri ajira rasmi.

Kitendo hicho kimezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya watu wakisema ni mfano wa namna vijana wanavyoweza kutumia ubunifu kujiajiri, wakati wengine wakitazama zaidi upande wa usalama na afya kutokana na aina ya biashara aliyoichagua.
Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1BpsAnYZcR/

Tatizo lingine sugu tulilonalo wabongo ni kusifia mambo ya kijinga na kuyaita "ubunifu"....sasa hiyo hela, hayo maumivu na janga analojitengenezea unaona vipo sawa?
 
Back
Top Bottom