Yo sella
Member
- Apr 2, 2020
- 57
- 94
Wakati vijana wengi katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wakilalamikia changamoto ya ukosefu wa ajira, kijana mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameibua wazo la kipekee la kujipatia kipato kupitia ubunifu wake.
Kijana huyo ameamua kuruhusu watu kumchapa kofi kichwani kwake palipo nyolewa kipara, ambapo kila kofi analopigwa humuingizia kiasi cha fedha. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtu anayehitaji kushiriki katika shughuli hiyo hulipa buku moja kwa kila kofi analompiga.
Mbinu hiyo imevutia maelfu ya watu ambao wamejitokeza kushiriki na kumpa kijana huyo fedha, huku wengi wakimpongeza kwa ubunifu wake wa kutumia hali iliyopo kutengeneza fursa ya kiuchumi badala ya kusubiri ajira rasmi.
Kitendo hicho kimezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya watu wakisema ni mfano wa namna vijana wanavyoweza kutumia ubunifu kujiajiri, wakati wengine wakitazama zaidi upande wa usalama na afya kutokana na aina ya biashara aliyoichagua.
Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1BpsAnYZcR/
nimecheka sana kwa dakika 5😂😂😂