TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
- Thread starter
- #21
😂😂😂Tempe mwaka tu kichwa kitakuwa kimebonyea na uchizi grade 1 ataupata
Atatoboa kabla ya kichwa kubonyea mkuu.
😂😂😂Tempe mwaka tu kichwa kitakuwa kimebonyea na uchizi grade 1 ataupata
Kwamba Afrika ya Kaskazini hawakustahili kuwepo bara moja na huku "gizani"?😂😂Nawaonea huruma Afrika ya kaskazini tu, aibu gani hii mnatuletea. Hata kama ni njaa ila sio hivyo
Kwani huyu ana tofauti gani na boxers wale (mabondia) wanaopigana ngumi ulingoni?Tatizo lingine sugu tulilonalo wabongo ni kusifia mambo ya kijinga na kuyaita "ubunifu"....sasa hiyo hela, hayo maumivu na janga analojitengenezea unaona vipo sawa?
Ni shida mkuu!Ni changamoto kubwa sana.
Wakati vijana wengi katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wakilalamikia changamoto ya ukosefu wa ajira, kijana mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameibua wazo la kipekee la kujipatia kipato kupitia ubunifu wake.
Kijana huyo ameamua kuruhusu watu kumchapa kofi kichwani kwake palipo nyolewa kipara, ambapo kila kofi analopigwa humuingizia kiasi cha fedha. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtu anayehitaji kushiriki katika shughuli hiyo hulipa buku moja kwa kila kofi analompiga.
Mbinu hiyo imevutia maelfu ya watu ambao wamejitokeza kushiriki na kumpa kijana huyo fedha, huku wengi wakimpongeza kwa ubunifu wake wa kutumia hali iliyopo kutengeneza fursa ya kiuchumi badala ya kusubiri ajira rasmi.
Kitendo hicho kimezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya watu wakisema ni mfano wa namna vijana wanavyoweza kutumia ubunifu kujiajiri, wakati wengine wakitazama zaidi upande wa usalama na afya kutokana na aina ya biashara aliyoichagua.
Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1BpsAnYZcR/
Anajali Pesa ila hajali afya yake.Ni shida mkuu!
Yani crocodile we acha tu 😄Kwamba Afrika ya Kaskazini hawakustahili kuwepo bara moja na huku "gizani"?😂😂
Utoto 😆Daaaahhhhh🥹🥹
Huu si unyanyasaji sasa mkuu?
Wacongo usiwaamini ,kaishaenda Kwa mfumu,hapo hata haumii na hayo makofiSiku akutane na kofi zito dishi litayumbaa
Ni tatizo kubwa.Kutingisha ubongo namna hiyo ni tatiz
Na utakuta hapo hana bima yoyote😂😂Ajira zingine inabidi uwe na bima kubwa
Kwa hiyo hapo ameshapikwa akapikika?😂😂Wacongo usiwaamini ,kaishaenda Kwa mfumu,hapo hata haumii na hayo makofi
Anajitafutia ma depression, na tremors kama za Parkinson's.Chronic Traumatic Encephalopathy
Huo ni zaidi ya utoto mkuu😂😂Utoto 😆