k-bee
JF-Expert Member
- Aug 30, 2017
- 1,023
- 1,185
Kama kichwa kinavyojieleza..; Nimefanya uchunguzi wangu mdogo nimegundua maisha ya kijijini yana unafuu na raha zaidi ya maisha ya mjini kwa kijana anayejitafuta..!
Kijijini maisha si mazito kama mjini mana kijijini unapata mboga za majani bure kabisa kwa majirani shambani au unapanda mwenyewe mana ardhi ipo ya kutosha kufanya biashara ya mbogamboga na hata ufugaji wa kuku wa kienyeji..!
Pande hizi nilipo kuku wa kienyeji jogoo aliyeshiba ni elfu 25 mpaka elfu 30 na tetea ni kumi na tano...!!
Vijijini kwa sasa hata biashara ya bodaboda inakua kwa kasi haina haja ya kukimbilia mijini na kuishi maisha yasiyoeleweka
Ulimaji wa mazao kiangazi ( msimu sio wa mvua) kama viazi na mahindi nao unakua kwa kasi na kufanya vijana wa vijijini kuwa na maisha mazuri ya kujitegemea kuliko vijana waliokimbilia mijini
Vijijini kumenoga, turudi tuvijenge vijiji vyetu na tubaki tuviendeleze vijiji vyetu