Kijana wa Kukaa Shamba anahitajika

The bump

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,488
Reaction score
2,908
Shamba lipo hapo Wilaya ya Kisarawe. Majukumu ya kijana ni kuweka mazingira sawa, kulima na kuhakikisha majani hayaoto kwenye shamba husika.

Shamba ni la heka 2, halijapandwa zao lolote lina majani. Kuna nyumba katikati ya shamba ambayo ndio makazi ya kijana husika.

Nyumba imekamilika inayofaa kuishi binadamu aliekamilika.

Chakula: Juu yangu muajiri
Mshahara: Makubaliano



Picha hapo Juu ni nyumba iliyo Shamba.

Nimeipiga picha nikiwa shamba/kiwanja cha jirani ambae yeye tayari kwake ni kusafi. Ukiangalia hiyo picha kuna eneo halina majani hapa mwanzo, hiki ni kiwanja/shamba cha mtu mwingine yeye kashajenga shamba lake safi kiwanja kimenyooka kama Azam Complex.

Na Kijana ninae mtaka ndio nataka aondoe ile nyumba kutoka kati kati ya majani alime kote kipatikane kiwanja kisicho na majani Nyumba ikae hapo kati. Jukumu kubwa ni hilo usafi wa kiwanja muda wote jani lisiote hata 1.

NOTE: Akitokea mtu na familia yake anataka kukaa huku anakaribishwa, mshahara tutakubaliana, chakula juu yangu muajiri. Ruksa ukitaka kulima, ruksa ukitaka kufuga, ruksa kufanya chochote.

Muhitaji alie serious tu karibu inbox.
 
Vijana wa bongo watakutaka mkubaliane menu ipoje kwa wiki
Sio uongo na wala unachoandika sio utani.

Nilipata vijana hapa Dar kipindi cha nyuma kabla sijawajengea hapo nilipanga chumba kijijini hapo nikawawekea vitu vya kula.

Mchele, unga, viungo (nyanya, karoti, kitunguu), dagaaa...

Siku moja nikapiga simu nikawauliza mko wapi? Wakasema wapo nyumbani, Leo hamjaenda kazini? Wakasema hawajaenda (wana njaa).. kwanini? Chakula mboga karoti zimeisha kuna nyanya na kitunguu tu hatujapika..

Nikagomba pale ikaisha, Siku ingine wakaniletea Kubwa KULIKO wamechoka UGALI na WALI wamekinai wanaomba Hela wanunue Ndizi labda au vyakula vingine.

KESHO yake wote walikuwa wanawasiliana kwenye simu, Mmoja akiwa anaelekea MBEYA kwao mwingine MBAGALA huko...
 
Nahitaji hii mkuu nakutumia namba yangu
 
Unalipa kias Gani mkuu mbona kama hakuna umeme hapo
 
Nimekutumia namba
 
Ngoja nichangamkie fursa💆
 
Hawajui kupambania maisha
 
Mkuu, utaniruhusu kufanya shughuli zangu nyingine...? Nje ya mji...? Maana mimi ni boda boda ila kupitia hapo nimeona kuna fursa ya kilimo ambacho tunaweza kufanya hata kulima mahindi... ukasponsor tukagawana.

Inshort napenda sana kilimo kama upo seriously naomba tuwasiliane .​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…