Kijana wa Umri wa Miaka 18 Auwa Watu 8 Kisha Kujipiga Risasi

Kijana wa Umri wa Miaka 18 Auwa Watu 8 Kisha Kujipiga Risasi

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Kijana wa miaka 18 aliyetajwa kuwa mshukiwa wa shambulio la risasi 13 Feb 2026 lililoua watu wanane na kujeruhi makumi ya wengine huko British Columbia, Canada, Jesse Van Rootselaar alipatikana amefariki katika eneo la tukio kutokana na kujipiga risasi.

Aidha Uchunguzi wa polisi Umesema Kabla ya kujipiga risasi aliacha Ujumbe Mfukoni mwake unaosema " Siwezi kujibu kwanini nimetekeleza mauaji haya, lengo langu Ilikuwa ni kuua zaidi, japokuwa sijafanikiwa waliosalimika watabaki na alama yangu"

Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana. Watu sita waliuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika Shule ya Sekondari ya Tumbler Ridge.

Polisi wamesema mshitukiwa huyo alienda shuleni kutekeleza mauaji baada ya kuwauwa mama yake, baba yake na kaka yake nyumbani.

Hata hivyo mamlaka zilisema Van Rootselaar alizaliwa akiwa mwanamume wa kibaolojia lakini akatambuliwa kama mwanamke.

"Ninaweza kusema kwamba Jesse alizaliwa kama mwanamume wa kibaolojia ambaye takriban miaka sita iliyopita alianza kubadilika kuwa mwanamke," Dwayne McDonald, naibu kamishna wa Polisi wa Kifalme wa Canada (RCMP), alisema.

Tukio la ufyatuaji risasi lilitokea katika nyumba iliyo karibu, kisha mshukiwa akaenda shule, McDonald alisema.

Waliouawa katika shule hiyo ni mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 39, wanafunzi watatu wa kike, wote wakiwa na umri wa miaka 12, na wanafunzi wawili wa kiume, mmoja wa miaka 12 na mwingine 13.
1788270440414.png
 
Baad ya kufikisha miaka 18 akaenda dukan kuchukua. Mashine dah, alikuwa labda Tatizo la Afya ya akili
 
Transgender huyo na huenda familia ilimnyanyapaa. Kuna mengi yanaendelea behind closed doors. Dysfunctional families ndo mwanzo wa majambazi na wauwaji..
 
Ila inatia uchungu,unajijua kabisa mimi ni mwanaume halafu ghafla unaanza kubadilika kuwa mwanamke...
 
"Ninaweza kusema kwamba Jesse alizaliwa kama mwanamume wa kibaolojia ambaye takriban miaka sita iliyopita alianza kubadilika kuwa mwanamke," Dwayne McDonald, naibu kamishna wa Polisi wa Kifalme wa Canada (RCMP), alisema.
1000079638.jpg
 
Hakupaswa kubadili gender hapo ndio shida ilipoanzia
 
Back
Top Bottom