Kitu kingine nilichojifunza maishani ni swala la kukopesha ndugu na marafiki, I learned this the hard way, nimepoteza hela nyingi sana takribani milioni 9 kwa kusaidia ndugu ambao hawana shukrani, kuna huyo nilimpa milioni 5 hadi leo hajanilipa na hana mpango wa kunipa. Unaenda kudai hela mtu anakuchamba.
Namshukuru mungu nimewasamehe na sina kinyongo na ndugu yangu yeyote, kwa sababu naamini ndugu na rafiki ni watu muhimu sana maishani kuliko hata hela.
Kitu chingine ambacho vijana inabidi tujifunze ni kwamba, kuna kipindi flani katika maisha yetu, mungu hufungulia baraka zake, tunajikuta tunapata hela nyingi sana ambazo sometimes hajutui tuzipeleka wapi au tuzitumiaje.
Huu ni muda ambao inabidi tuwe makini sana kwasababu Lucifer(Ibilisi) hutumia nguvu sana kutuyumbisha na kutuingiza kweny mienendo isiyofaa ili tutumie hela vibaya kwa mambo ambayo siyo ya msingi kama pombe, ngono, kuzurura, mavazi expensive, na expenses zingine zisizo kuwa na umuhimu.
Hakika nakwambia ukiweza kutumia huu muda ambao kipato chako kipo stable na madili yanatiki vizur na kuepukana na zinaa, utakuja kuwa na uzee wa baraka sana, hutasumbuliwa na magonjwa, hutasumbuliwa na uchumi mbovu, utaweza kusaidia familia na ndugu zako wengine vizur, utakuwa baraka kweny ukoo wenu.
Sisemi uongo mm mwenyew ni mhanga wa kwenda viwanja, weekend hivi kama leo nisipoenda viwanja najihic kabisa mwili unauma, japokuwa situmii pombe wala kilevi chochote(kwanza siwez, siku ya kwanza kunywa pombe nilitapika sana)
Ewe kijana mwenzangu ukiona asaiv account yako inacheka basi jua muda wa kuwa makini sana.
Lucifer(Ibilisi) hataki tuwe matajiri, anajua tajiri anaweza kujiamulia maisha ya kuishi, maskini hawez, maskini hata akiambiwa sujudia sanamu nikupe millioni kumi anakubali kwasababu maskini anaamuliwa maisha ya kuishi.
Chingine jamani, tukumbuke kilimo na ufugaji, hasa tulioajiriwa, mkulima huwez kumwona anamlilia mwanasiasa amlipe mshahara, mkulima ana uhakika wa kula hata kama hana hela mfukoni, chochote unachofanya hata kama wewe ni rubani hakikisha unalima na kufuga(sio lazima uwe mkulima mkubwa hata ukiwa na bustani nzuri ya mbogamboga na kuku wa idadi flani inatosha), serikali haitabiriki tuachane na mambo ya kuwategemea wanasiasa hawa.
Mwakani mungu akinibariki naingia kweny kilimo na ufugaji rasmi.