Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ukiitazama hii vita katika jicho la kijeshi ni dhahiri urusi imefeli!
Imefeli kwa sababu imeshindwa kufikia malengo yake ya uanzishaji hii vita!
Lengo la Kijeshi la Urusi ilikuwa ni kuingia Kiev haraka, kukamata mji mkuu na kuuangusha utawala wa Zelensky. Lakini hadi leo hii takriban siku ya 60 ya kivita, Urusi imeshindwa kukamata Kiev, na majeshi yake baada ya kukutana na upinzani mkali yakakimbia(retreat) kutoka miji ya ndani na kurudi huko Mashariki ambako walikuwa wanapakalia toka mwaka 2014.
Urusi imepata hasara kubwa sana ya vifaa na askari. Vifaru vyake vilikuwa vikikaangwa kwelikweli na Javelin missiles, pamoja na drones za Bayraktaar.
Logistics za kupeleka chakula na silaha ndanindani kwa askari wake ilikuwa shida
Wakati huo vikwazo vikiendelea kuichakaza urusi kwelikweli.
Hadi hivi sasa Zelensky amefanikiwa kuilinda serikali yake, na kinachofuata sasa ni kuandaa operesheni kabambe ya kumtoa nyoka pangoni huko Mashariki, Hii itakuwa operesheni kali sana na ngumu sana lakini itawezekana.
Urusi ni Taifa kubwa lakini uchumi wake ni mdogo kuliko jimbo moja tu la Texas Marekani, haina fedha za kupigana hii vita kwa muda mrefu, itakachokifanya ni kutafuta kideal cha kizushi na Ukraine ili kuficha aibu ya uso wake!
Kikubwa nilichojifunza katika hizi vita, Moyo wa askari una nguvu kuliko silaha kali ktk mikono ya askari asiye na moyo wa mapambano!
Mafanikio ya kijeshi ya Urusi huko mashariki mwa Ukraine katika vita hii ya Sasa wala si jambo la ajabu maana warusi walishakuwepo huko toka mwaka 2014, hakuna kitu kipya!. Ni sawasawa na kupiga bomu mochwari na kisha kushangilia kuwa umeua!