DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Katika mkutano huo wa kampeni, Dkt. Godwin aliwaeleza wananchi kuhusu kazi kubwa na mafanikio yaliyofanywa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu na maji ni ushahidi wa uongozi thabiti wa Dkt. Samia.
Wananchi wa Mji Mwema walionesha ushabiki na imani kubwa kwa CCM, wakiahidi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuendeleza kasi ya maendeleo iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya sita.