SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

Screenshot_20230913-072231_WhatsApp.jpg

Tunachokijua
Usiku wa Septemba 9, 2023, tetemeko kuu la ardhi lilitokea nchini Morocco na kuharibu vibaya moja ya maeneo muhimu ya kihistoria katika milima ya Atlas ya Juu, msikiti wa ardhi na mawe uliojengwa na nasaba ya enzi za kati iliyoteka Afrika Kaskazini na Uhispania.

Vyombo vya habari vya Morocco viliripoti kuwa sehemu za Msikiti wa Tinmel zimeporomoka. Picha zinazosambaa mtandaoni zilionyesha kuta zilizoanguka, mnara ulioanguka nusu na marundo makubwa ya uchafu.

screenshot-2023-10-05-161114-png.2772728

Mwanaume akitembea karibu na Msikiti wa Tinmel, ambao uliharibiwa na tetemeko kuu la ardhi, huko Tinmel, Morocco, Septemba 11. REUTERS/Hannah McKay
Kikijibu swali la Reuters kuhusu uharibifu ulioripotiwa kwa Tinmel, chanzo cha Wizara ya Utamaduni ya Morocco kilisema Wizara imeamua kukarabati na kuurejesha msikiti huo na wangetoa bajeti ya kutosha kufanikisha kazi hiyo.

Msikiti wa karne ya 12 ulijengwa ambapo nasaba ya Almohad ilianzisha mji mkuu wake wa kwanza katika bonde la mbali la Atlas kabla ya kwenda kuteka Marrakech, kumtangaza kiongozi wake Khalifa, na kuandamana katika eneo hilo kwa kuchochewa na bidii ya kidini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni UNESCO limesema limesikia "uharibifu muhimu sana kwa Msikiti wa Tinmel", ambalo limeongeza kuwa lilipendekezwa kuorodheshwa kama eneo la Urithi wa Dunia, lakini likaongeza kuwa bado linasubiri kutuma timu kutathmini uharibifu huo.

Hadi Septemba 11, 2023, takriban watu 2,000 wamekufa katika tetemeko hilo la kipimo cha 6.8, ambalo ndilo lililoharibu zaidi eneo hilo tangu mwaka 1900. Lilipiga siku ya Ijumaa usiku, na kuharibu majengo ya jadi katika Atlas Kuu na kuanguka kwa nyumba za matofali na mawe katika vijiji vingi vinavyoonekana.

Tetemeko hilo pia lilisababisha uharibifu katika mji wa zamani wa Marrakech , eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, ambapo mnara ulipinduka na sehemu za kuta za jiji la kihistoria kuanguka pamoja na baadhi ya nyumba za jadi.

JamiiForums imebaini kuwa Madai ya msikiti kutokuharibiwa na tetemeko hayana ukweli, na hakuna taarifa zinazothibitisha jambo hili.
Kwa Libya ni Yesu kalipiza. Unakumbuka walivyowachinja wale wakristo kutoka Ethiopia kwasababu walikataa kusilimu kufuata mila za kiarabu?
Sidhani kama ni kweli hiyo ni Imani yako dunia nzima imejaa majanga hiyo ni kawaida Africa tuko kwenye hali ya majanga January hadi December sijui kama kweli ni mpago wa yesu kutuadhibu kama unavo taka kutuaminisha.
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.View attachment 2747461
Unashangaa hilo?Subiri yatakayowakuta ninyi CCM!
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.View attachment 2747461
Sasa kama issues ni Imani Sasa yatakuwa yana faida gani kama yamewaangamiza waumini wote na mjenzi wa msikiti?
 
Wasabato na wavaa kobazi hizi ndo sehemu wanazopenda kuchukulia point tatu za bureeee.......
Wewe umehamisha mada sisi wa sabato tumekukosea nini?? Wakati wote tunaamini yesu yule yule isipo kua nyie Roma mnaabudu sanamu lake na la Maria sisi hapana hata hatuvai rozari au kunywesha watu pombe kanisani.
 
😁😁😁Oky nimekusoma kijana wa mnyazi mungu
 
Sidhani kama ni kweli hiyo ni Imani yako dunia nzima imejaa majanga hiyo ni kawaida Africa tuko kwenye hali ya majanga January hadi December sijui kama kweli ni mpago wa yesu kutuadhibu kama unavo taka kutuaminisha.
Nimecheka sana hapo SIJUI NI MPANGO WA YESU KUTUADHIBU. 😆😆😆😆

Huko sahihi kabisa nikikumbuka vimbunga na moto kila siku marekani na canada.
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.View attachment 2747461
Mungu wa kweli hawezi Fanya jambo ovu kama Hilo! Na hawezi kulazimisha watu wamwabudu kinafiki ,,yaani wamwabudu Kwa kuwatiisha

Angetaka hivyo angetufinya wote ,acheni kumchafua mungu.. we are under Satan rule as God of this kingdom , Kila kitu kinachotokea kipo sisi na shetan tunawajibika baada ya Ile dhambi ya wazazi wetu WA kwanza pale Eden
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.View attachment 2747461
Nimemkumbuka yule nabii Alie sema mwakani mwezi April na may 2024...

Watu waondoke dar es salaam maana mji utapigwa na mafuriko naanza ku connect dots
 
Back
Top Bottom