SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

Screenshot_20230913-072231_WhatsApp.jpg

Tunachokijua
Usiku wa Septemba 9, 2023, tetemeko kuu la ardhi lilitokea nchini Morocco na kuharibu vibaya moja ya maeneo muhimu ya kihistoria katika milima ya Atlas ya Juu, msikiti wa ardhi na mawe uliojengwa na nasaba ya enzi za kati iliyoteka Afrika Kaskazini na Uhispania.

Vyombo vya habari vya Morocco viliripoti kuwa sehemu za Msikiti wa Tinmel zimeporomoka. Picha zinazosambaa mtandaoni zilionyesha kuta zilizoanguka, mnara ulioanguka nusu na marundo makubwa ya uchafu.

screenshot-2023-10-05-161114-png.2772728

Mwanaume akitembea karibu na Msikiti wa Tinmel, ambao uliharibiwa na tetemeko kuu la ardhi, huko Tinmel, Morocco, Septemba 11. REUTERS/Hannah McKay
Kikijibu swali la Reuters kuhusu uharibifu ulioripotiwa kwa Tinmel, chanzo cha Wizara ya Utamaduni ya Morocco kilisema Wizara imeamua kukarabati na kuurejesha msikiti huo na wangetoa bajeti ya kutosha kufanikisha kazi hiyo.

Msikiti wa karne ya 12 ulijengwa ambapo nasaba ya Almohad ilianzisha mji mkuu wake wa kwanza katika bonde la mbali la Atlas kabla ya kwenda kuteka Marrakech, kumtangaza kiongozi wake Khalifa, na kuandamana katika eneo hilo kwa kuchochewa na bidii ya kidini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni UNESCO limesema limesikia "uharibifu muhimu sana kwa Msikiti wa Tinmel", ambalo limeongeza kuwa lilipendekezwa kuorodheshwa kama eneo la Urithi wa Dunia, lakini likaongeza kuwa bado linasubiri kutuma timu kutathmini uharibifu huo.

Hadi Septemba 11, 2023, takriban watu 2,000 wamekufa katika tetemeko hilo la kipimo cha 6.8, ambalo ndilo lililoharibu zaidi eneo hilo tangu mwaka 1900. Lilipiga siku ya Ijumaa usiku, na kuharibu majengo ya jadi katika Atlas Kuu na kuanguka kwa nyumba za matofali na mawe katika vijiji vingi vinavyoonekana.

Tetemeko hilo pia lilisababisha uharibifu katika mji wa zamani wa Marrakech , eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, ambapo mnara ulipinduka na sehemu za kuta za jiji la kihistoria kuanguka pamoja na baadhi ya nyumba za jadi.

JamiiForums imebaini kuwa Madai ya msikiti kutokuharibiwa na tetemeko hayana ukweli, na hakuna taarifa zinazothibitisha jambo hili.
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

View attachment 2747461
Nimefuatilia kwenye blogs na vyanzo vingine sijaipata habari hii. Naomba mtoa thread Covax aweke source.

Otherwise itakuwa picha ya kuokoteza na kuwekewa maneno tu
 
Wewe umehamisha mada sisi wa sabato tumekukosea nini?? Wakati wote tunaamini yesu yule yule isipo kua nyie Roma mnaabudu sanamu lake na la Maria sisi hapana hata hatuvai rozari au kunywesha watu pombe kanisani.
Aliyebariki maji yakawa divai alikosea? Someni neno mlielewe... acheni tabia ya kung'ang'ania msitari Mmoja na kuona umelielewa neno.

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Mungu wa kweli hawezi Fanya jambo ovu kama Hilo! Na hawezi kulazimisha watu wamwabudu kinafiki ,,yaani wamwabudu Kwa kuwatiisha

Angetaka hivyo angetufinya wote ,acheni kumchafua mungu.. we are under Satan rule as God of this kingdom , Kila kitu kinachotokea kipo sisi na shetan tunawajibika baada ya Ile dhambi ya wazazi wetu WA kwanza pale Eden
Naamini huwezi ukawa mkristo... ikiwa ni mkristo itasikitisha !!

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
We jamaa unafikiri Mungu ni mtu siyo!?..na Wala hujui mipango yake na binaadam,elimu Haba udhia!!

Mimi nafikiri story zote za an imaginary being sitting in the clouds ni story za kusadikika. Wewe na akili yako unadhani mungu anakaa in the clouds anaangalia nyie mnavyokufa na kuteseka tu, hiyo ndo furaha yake sio.
 
Kakuambia nani yupo mawinguni!?..mawingu hayazidi kilomita moja toka ardhini,ndiyo maana nikakwambia huna elimu ya Mungu,upo chini ya half-baked,yaani ni mbumbumbu,ungeacha ujuaji ukajifunza kwanza
 
Kakuambia nani yupo mawinguni!?..mawingu hayazidi kilomita moja toka ardhini,ndiyo maana nikakwambia huna elimu ya Mungu,upo chini ya half-baked,yaani ni mbumbumbu,ungeacha ujuaji ukajifunza kwanza

😂😂 carry on na Imani za Mungu wako mpenda vifo na mateso regardless ya anapoishi. I, for one, am good 👍
 
kawaulize wamisri wote leo watakuambia. hata mood aliamini hivyo kuhusiana na story ya firauni ambaye hadi leo mabaki yake yapo. firauni (farao) alikufa baada ya kuingia sehem maji yametenganishwa katikati ya bahari, waisrael walipovuka tu Musa akapiga maji kwa fimbo yakajirudi kama bahari tena na firauni akafia humo. mwili wake ulipopatikana ndio wakauhifadhi ili iwe kumbukumbu kwenu ninyi.
Ns wewe umeamini yote hayo
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

View attachment 2747461
Nyumba za kuishi za Udongo za Mskiti matofali ya kuchoma na sementi juu
 
Shida ya Africa kaskazini nyumba zao si imara wanajenga ilimradi
Wanazipamba nje lakini uhalisia si nyumba
Hili janga litaikumba siku moja Zanzibar Bagamoyo
Mungu awafanyie wepesi kwa majanga haya
Earthquake Floods dah mwisho wa Ulimwengu au
Unajua maana ya ulimwengu?
 
Hili linajionesha bayana watu wa eneo hilo walifanya machukizo sana kwa mwenyenzi mungu, walimchukiza sana mungu kwa kudharau watu na kuwa wabinafsi wao kwa wao, linawezekana alijenga msikiti alimcha mungu na kutoa vile alivojaliwa.

Zinaa ziliwazidi, fitina, roho za husda, wivu, ubinafsi na choyo, dharau na kiburi, mengine watamalizia waislamu......mimi si muislam ila hili linaonesha jamii hiyo ilikuwa ni waja wa mungu walio kiremiwa vizuri sana na walipata tawala za juu za kifalme kwa wakirstu tunaamini hivo ila sasa tamaa za dunia ziliwazidi wakaona mungu kwao ni ziada.
Hehehe
 
Miezi michache imepita Tetemeko -uturuki ,likaenda piga Morocco,jana Libya imepigwa na mafuriko watu 2000 wamekufa na zaidi ya 10000 hawajulikani walipo,wengine wamesukumizwa baharini

Ni Mwendo wa Mapigo tu kwa Waarabu mpk wamrudie Mungu wa Kweli😇
Wee na Libya tena?
 
Je, hicho kijiji hakikuwa na kanisa ?
Je, vitabu vya Mungu havikuwepo?
 
Kwa Libya ni Yesu kalipiza. Unakumbuka walivyowachinja wale wakristo kutoka Ethiopia kwasababu walikataa kusilimu kufuata mila za kiarabu?
Hilo silijui lakini dini ya kulazimishana mpaka kuchinjana kwa dunia ya Leo yenye uelewa,inatia shaka sana.Maana kama dini yako ni nzuri huwezi mchinja mtu asopenda vitu vizuri.
 
Kijiji chote kina msikiti huo mmoja? If not, kipi kimetokea Kwa misikiti mingine.
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

View attachment 2747461
Huu msikiti na aliyejenga mbona hawajasalimika? Au walitenda dhambi?

F5mw6UNWIAAM6kD.jpeg

Back
Top Bottom