SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

Screenshot_20230913-072231_WhatsApp.jpg

 
Tunachokijua
Usiku wa Septemba 9, 2023, tetemeko kuu la ardhi lilitokea nchini Morocco na kuharibu vibaya moja ya maeneo muhimu ya kihistoria katika milima ya Atlas ya Juu, msikiti wa ardhi na mawe uliojengwa na nasaba ya enzi za kati iliyoteka Afrika Kaskazini na Uhispania.

Vyombo vya habari vya Morocco viliripoti kuwa sehemu za Msikiti wa Tinmel zimeporomoka. Picha zinazosambaa mtandaoni zilionyesha kuta zilizoanguka, mnara ulioanguka nusu na marundo makubwa ya uchafu.

screenshot-2023-10-05-161114-png.2772728

Mwanaume akitembea karibu na Msikiti wa Tinmel, ambao uliharibiwa na tetemeko kuu la ardhi, huko Tinmel, Morocco, Septemba 11. REUTERS/Hannah McKay
Kikijibu swali la Reuters kuhusu uharibifu ulioripotiwa kwa Tinmel, chanzo cha Wizara ya Utamaduni ya Morocco kilisema Wizara imeamua kukarabati na kuurejesha msikiti huo na wangetoa bajeti ya kutosha kufanikisha kazi hiyo.

Msikiti wa karne ya 12 ulijengwa ambapo nasaba ya Almohad ilianzisha mji mkuu wake wa kwanza katika bonde la mbali la Atlas kabla ya kwenda kuteka Marrakech, kumtangaza kiongozi wake Khalifa, na kuandamana katika eneo hilo kwa kuchochewa na bidii ya kidini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni UNESCO limesema limesikia "uharibifu muhimu sana kwa Msikiti wa Tinmel", ambalo limeongeza kuwa lilipendekezwa kuorodheshwa kama eneo la Urithi wa Dunia, lakini likaongeza kuwa bado linasubiri kutuma timu kutathmini uharibifu huo.

Hadi Septemba 11, 2023, takriban watu 2,000 wamekufa katika tetemeko hilo la kipimo cha 6.8, ambalo ndilo lililoharibu zaidi eneo hilo tangu mwaka 1900. Lilipiga siku ya Ijumaa usiku, na kuharibu majengo ya jadi katika Atlas Kuu na kuanguka kwa nyumba za matofali na mawe katika vijiji vingi vinavyoonekana.

Tetemeko hilo pia lilisababisha uharibifu katika mji wa zamani wa Marrakech , eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, ambapo mnara ulipinduka na sehemu za kuta za jiji la kihistoria kuanguka pamoja na baadhi ya nyumba za jadi.

JamiiForums imebaini kuwa Madai ya msikiti kutokuharibiwa na tetemeko hayana ukweli, na hakuna taarifa zinazothibitisha jambo hili.
Kwa jamii ya waislamu haswa Kwa mataifa kama Libya unategemea Kijiji kizima kilikuwa na mskiti mmoja tu huo?
 
kawaulize wamisri wote leo watakuambia. hata mood aliamini hivyo kuhusiana na story ya firauni ambaye hadi leo mabaki yake yapo. firauni (farao) alikufa baada ya kuingia sehem maji yametenganishwa katikati ya bahari, waisrael walipovuka tu Musa akapiga maji kwa fimbo yakajirudi kama bahari tena na firauni akafia humo. mwili wake ulipopatikana ndio wakauhifadhi ili iwe kumbukumbu kwenu ninyi.
Acha uongo wewe.

Unafahamu kuwa Masoreti walikuja kuandika hizo hadithi upya kwa kuingiza majina na geography ya maeneo baadae.

Yaani hao wahusika halisi (Farao) wameandikiwa story za kutungwa tu.

Kwamba unasema farao alikufa kwenye maji!?
Where is your refference
 
Miezi michache imepita Tetemeko -uturuki ,likaenda piga Morocco,jana Libya imepigwa na mafuriko watu 2000 wamekufa na zaidi ya 10000 hawajulikani walipo,wengine wamesukumizwa baharini huko

Ni Mwendo wa Mapigo tu kwa Waarabu mpk wamrudie Mungu wa Kweli[emoji56]
Umesahau hata U.s.a nao juzi tu wamepigwa na tufani.acha kujitoa ufahamu kwa chuki zako.
 
Allahhumma amina
Bismillah Allahu akbar
La ilaha illa Allah Muhammed asul Allah
Ash-hadu an la ilaha illa Allah, Wa ash-hadu anna Muhammadan Rasulu-Allah
Translate Kwa kiswahili tafadhari kama ni ujumbe Kwa wote
 
Kwa Libya ni Yesu kalipiza. Unakumbuka walivyowachinja wale wakristo kutoka Ethiopia kwasababu walikataa kusilimu kufuata mila za kiarabu?
acha kuangamia
kwa kukosa maarifa ewe mgalatia
yesu aliyeshindwa kujiokoa kwenye mateso ya.msalabani leo aweze kuadhibu!
ewe mgalatia
uliyekosa akili ni
Nani
aliyekuloga?
 
Huyu kajitungia tu.

Atupe Source
Naona nyie amuangalia hata talifa zakimataifa hashimu haebara wa aljazeera mvona anali report tukio hili kala baada ya saa kwenye taarifa za habari akiwa eneo la tukio au hujui kiingereza kabisa, ila ungeona picha tu.
 
Kwamba wali weka matairi?
ndio. nafikiri waliamini ukiweka matairi eneo lenye historia ya tetemeko, likija mtikisiko wake jengo litakuwa linanesa na halitaanguka. kuna clip ilisambaaga sana kipindi kile hadi walivyokuwa executed, walikuwa wanakamata mmoja mmoja (tena ujue ni mabos mainjinia wenye pesa na makampuni), wanamrushia kwenye shimo, wanamshindilia risasi. waliuwa wengi kweli.
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

View attachment 2747461
Na wewe ukakubaliana na hizo propaganda? Imeelezwa kwenye chombo gani cha habari juu ya hilo jambo?
 
Kwa Libya ni Yesu kalipiza. Unakumbuka walivyowachinja wale wakristo kutoka Ethiopia kwasababu walikataa kusilimu kufuata mila za kiarabu?

yesu ana nguvu gani za kulipiza katundikwa msalaba na kijana moja tena mlemavu wa mguu kamkamata kampigilia msumari akawa anaomba msaada nisaidieni sirudii tena nimekoma halafu huyo ndie alipeze kisasi
 
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

View attachment 2747461
Nina swali mkuu
Mungu huyo aliesambaratisha majengo yote na kuua watu ndo huyo huyo aliebakiza mskiti?
 
Back
Top Bottom