sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Maskini vijana wa watu wakishinda bss tukiwaona mtaani bado hali zao za uchumi zimeyumba zinaanza stori kwamba wamefanyia hela umalaya, ulevi au starehe za kipuuzi, Kumbe hakuna kitu kama hicho, Vijana waambulia kupewa milioni 1 tu😱😱
Jumanne Iddi, Walter Chilambo, Ramadhan, Kayumba: wote kusema kweli uchumi na muziki vyote vimeyumba, wengine wamerudi mtaani utawaonea Huruma.
Inasemekana kwamba katika ile milioni 50 mshindi anapewa milioni 29 cash na milioni 30 inapigwa na kina Rita kwa kisingizio cha kipuuzi cha kumwendeleza msanii kitu ambacho hawajawahi kukifanya. Hio milioni 20 hapo unapewa milioni 1 tu, na ndo imetoka hiyo na ushahidi ni huyu kijana ambaye kushinda 2019 kawawashia moto hawa matapeli wanaojifanya wanaishi maisha ya juu huko Insta kumbe ni matapeli wa hali ya juu.
Ningependa kujua nini kilimkuta Jumanne Iddi, Walter, Ramadhan na Kayumba ambaye hana mbele wala nyuma kimuziki. Kuna kila ishara hapa walipata tu milioni 2 au pungufu na umaarufu uliogeuka kuwa mzigo.
Yani nimegundua kwanini walikuwa wanawaengua mapema wale vijana ambao walionekana kuwa na msimamo flani hivi wa kujiamini na kuwafanya kina Kayumba (aka katoto) washinde, huenda walikuwa wanataka watu ambao ni rahisi kuwa control washinde.
Mwaka huu hizo hela mtazitapika tu.
Nay Wa mitego aliwahi kuimba hili akaonekana muongo ila leo ukweli umedhihirika nae akatoa mawili matatu.