Kikaangoni: Wengi hawajui kwanini naitwa Padri Mcharo, niulize chochote nikujibu

hahaha mcharo unanikosha na hayo maneno yako ya shombo yani
kama umezaliwa saluni! yani umenivunja mbavu hatari na komenti zako za nyuma
 
Mods tafadhalini piga ban huyu mtu mpaka abadili ID,

Kwa majibu yake ni kwamba hajawahi kuwa mkristo ila anafanya kusudi kudhalilisha ukristo.

cc: JamiiForums Moderator Paw Invisible


Dada yangu Jungle Warrior
Kwenye majibu ha maswali yenu nimesema hivi:
Nimeachana na dini ya binadam na kuhamia dini ya haki.
Sijataja dini ya mtu.
Sasa kama unakubali kuwa Ukristo ni ndio dini ya binadam mie hilo silijui.

Naitwa Mtumishi Mcharo
 
Sidhani kama kuna member humu ana kufikia kwa majibu machafu padri...
Ni hiyo dini mpya imekufunza hivo au tangu ukiwa padri ulikua hivo?
Hajawahi kuwa Padre huyu ni mmoja wa wale wenye kusambaza vitabu vya 'zijue haki zako' kama ni dawa yake ss inachemka
 
Hatimae nimepata maswali.
1. UDSM umesoma mwaka gani? Ulikua unasomea nini? Je unamiliki degree ngapi!? Ni kanisa katoliki lililokusomesha??
2. Una umri gani sasa?
3. Kwa sasa taaluma yako ni ipi??
4.Ulidumu kwenye huduma ya upadre kwa muda gani?


Asante dada rubii kwa umakini wako
UDSM ndipo nilipo hivi sasa, nachukua masters ya finance in OIL and GAS kwa scholarship ya kampuni ya STAT OIL.
Karibu UDBS dada yangu.

Umri wangu ni miaka kati ya 20 na 50
Kwa sasa taaluma yangu ni Project manager in IP Routing katika kampuni moja ya Waholanzi (mchongo huu niliupata tangu nasomea Theology pale Amsterdam)
IP Routing ni mambo ya Computer Networks

Kwa sasa nina degree mbili.
Theology (from Amsterdam Nethelands)
Computer Science (distance learning from Cambridge University)
MBA in Oil and Gas from UDSM (ON GOING)

Utumishi kwa ujumla (kuanzia masomo hadi Upadri wenyewe) nimedumu kwa takriban miaka 13
 
Wanasema ukislimu unapewa hiyo mifugo


Sio kweli kabisa.
Hayo ni maneno ya Makafiri tu.
Mie niliposilimu cha kwanza kabisa kupewa ilikua Juzuu Amma.
Nikaanza kujifunza Alif Be Te The Jim from the scratch. Dogo mmoja wa jirani yangu (alikua darasa la nne) ndio akaanza kunipiga msasa maana nilikua naona aibu kwenda madrasa kubwa zima na mindevu.
 
Sijakuelewa kabisa.
Swali lako halina kichwa, miguu wala matako.
Uliza vizuri dada cocochanel

Mashaka au uoga ulikujaaa kwa kuona umesomea yoteee na kuishia kuyaishi na ulipoishia katika dini hiyo wakati huo?

Kiswahili kigumu pia jamani.

OK, ninauliza kwamba je ni mashaka au uoga ulikujaa moyoni mwako hadi ukaamua kuachana na ukiristo, kwa sababu uliyasomea na haukuishi inavyotakiwa kidini au nini zaidi?

Ukiachama na hamu ya mwili kwa uliyofanya naamini kuna mengine yalikuondoa. Sorry kama umeeleza naona uzi wako umekimbia sana na sijausoma wote.
 
Naomba kuongezea swali hapo. Alirudisha vitu vyote kwa hiyari yake au alijimilikisha?


Kurudisha kutoka wapi.
Sikurudisha hata kimoja.
Bali niliondoka na bad langu la nguo na kuacha kila kitu pale pale Parokiani Itigi.
Kitu pekee nilichosepa nacho ni simu ya mkononi nilonunuliwa Tel Aviv mwaka 2011
 
Ukikutana na waumini wako bado unasalimiana nao vizuri? Kuna wanaokukimbia? **** wanaokusema vibaya ukisikia? Kuna walioelewa na kukutakia kila la kheri? Familia yako je? Ma padri wenzako wamekutenga au bado mnawasiliana?
 
Kwa sasa una miaka 28. Sina swali.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Vipi nafasi za kazi katika ile kampuni yenu na weupe?


Bado zipo pale pale.
Sema mchakato ulisimama kutokana na kazi ya ku review company policies.
Soon nitakuja ku re-advertise hapa sababu wale walikua nominated mwanzo wengi washagive up. Zoezi litaanza upya.
Stay tuned boss!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…