Kikao cha Bunge cha Oktoba: Yaliyojiri

Kikao cha Bunge cha Oktoba: Yaliyojiri

What are you actually talking about?

Watu wanaamini Zitto alijumuishwa kwenye kamati ili asiendeleze kilio chake kuhusu Buzwagi ama kumnyamazisha kabisa. Naomba aonyeshe kuwa kama nia ilikuwa hivyo basi hicho chambo hakikumnasa.
 
Mkuu Pundit huna haja ya maelezo mengi kuhusu taratibu na sheria za bunge.

Sisi wa kizazi kipya vilevile ni wajanja wa mjini kwa hiyo tunajua kuwa kwa kuwa Zitto ni mbunge wa Upinzani basi akitoa report hapa itakuwa mtarafuku mkubwa kuwa kavujisha siri za bunge whether ni kweli au uongo sisi haituhusu tunajaribu tu kupunguza matatizo yanayoweza kumpata MH. Zitto sababu ya ujinga wa chama tawala.

Kwani Mwanahalisi wanakosa gani mpaka kufungiwa?? Exactly, ni hayo hayo tu.
 
Weka tu mambo hadharani ni zama za ukweli na uwazi haogopwi mtu hapa.
Kwani kuna tofauti gani leo na kesho??
Tusiwe waoga kwa kiasi hicho.
 
Zitto Itakuwa vyema kama ukisubiri Bunge Lijadili hiyo Ripoti ya Shelukindo kwanza...Chochote tofauti na hivyo itakuwa ni kukiuka ethics za kazi yako...Tunahitaji sana uwakilishi wako Bungeni haswa kwenye kipindi hichi ambapo mambo yanaonekana kwenda hovyo...Mpo Wachache Bungeni mnaowakilisha matakwa ya watu...usijipungeze na kuwaachia mzigo huo wenzio wachache..Uwepo wako Bungeni ni muhimu Mheshimiwa!!!

Mkuu Mwawado,

Saaafi sana, mimi sina cha kuongeza.
 
Mkuu Pundit huna haja ya maelezo mengi kuhusu taratibu na sheria za bunge.

Sisi wa kizazi kipya vilevile ni wajanja wa mjini kwa hiyo tunajua kuwa kwa kuwa Zitto ni mbunge wa Upinzani basi akitoa report hapa itakuwa mtarafuku mkubwa kuwa kavujisha siri za bunge whether ni kweli au uongo sisi haituhusu tunajaribu tu kupunguza matatizo yanayoweza kumpata MH. Zitto sababu ya ujinga wa chama tawala.

Kwani Mwanahalisi wanakosa gani mpaka kufungiwa?? Exactly, ni hayo hayo tu.

Hili nimelieleza vizuri.Ni muhimu kujua nani kashika makali na nani kashika mpini at least for the time being. Nisichoelewa ni hii complacency ya kukubali tu kwa sababu bunge lina kanuni zilizo oppressive, basi tusiseme kwamba hizi kanuni ziko secretive na oppressive.
 
Weka tu mambo hadharani ni zama za ukweli na uwazi haogopwi mtu hapa.
Kwani kuna tofauti gani leo na kesho??
Tusiwe waoga kwa kiasi hicho.

Kama hakuna tofauti kati ya leo na kesho, basi tusubiri kesho and play it safe. Usimning'inizie nyang'au mnofu wa nyama kwa kutumuia mkono wako, si ajabu ukapoteza nyama na mkono pia. Kama wasemavyo waswahili - kawia ufike.
 
Kwanza ahsante Mheshimiwa.

Lakini, ngoja kwanza!

Tuliambiwa Tume imempa Kikwete mapendekezo, Kikwete kampa ripoti Ngeleja, Ngeleja amrudishie mapendekezo.

Sasa who is who, Bunge ndio lina maamuzi au Rais?

Hii ilikuwa ripoti ya Rais, vipi Bunge likaamua mapendekezo tofauti na Ngeleja? Na Kikwete ?

Ya Ngeleja yaliishia wapi ?

Halafu kesho mnajadili ya Shelukindo au ya Bomani ? Tofauti zake nini ?

Kwa nini kuna mbili ?

Hii ya Shelukindo ilifanyiwa uchunguzi lini relative to ya Rais?

Na kwa nini ya Shelukindo ikawa "radical" kuliko ya kwako uliyoshiriki wewe mpinzani ?

Tunataka kufuatilia vitu vilipoishia ili tujue vinaenda wapi.

My head is spinning.
 
Worries as Bunge set to debate mining reports By Faraja Jube and Damas Kanyabwoya, Dodoma

Mining companies were in limbo yesterday as Parliament formally cleared the way for the tabling of the Mining Sector Review Committee's report that recommends drastic changes in the way the sector is managed.

MPs will now have an opportunity to discuss the report and adopt it as a binding legal document that will require the enactment of a new law to implement some of its recommendations.

However, as Parliament listed the report among business in the 13th seating that opens in Dodoma today, a top executive of a leading mining company told The Citizen the decision had left them even more confused.

Barrick Gold Tanzania Limited�s executive general manager, Mr Deo Mwanyika, said tabling the report in Parliament would heighten anxiety in the sector.

"As stakeholders, no one has formally given the report to us. We have asked for it, but our efforts have been fruitless. Thus for Bunge to discuss it only serves to create more uncertainty," he said.

He added that mining firms were initially informed that it was the President who would decided on what had been recommended in the report after going through it.

"It is now becoming more confusing. We were told that the Government is already implementing the report's recommendations, and now we hear that Parliament is to debate it."

"One of the recommendations, we are told, is to involve us in the formulation of a new mining policy. It is this kind of uncertainty that has seen the number of exploration projects decline," Mr Mwanyika said in a telephone interview.

He said many mining companies had slashed their exploration budgets because of the way the matter was being handled.

Mining companies have been jittery after the committee led by Judge Mark Bomani called for an overhaul of the mining sector and establishment of a minerals authority to oversee all mining ventures.

Other recommendations include reviewing of taxes and royalties paid by multinational companies and joint shareholding between the Government and investors in new mining projects.

The report did not feature in the 2008/9 budget proposals that Energy and Minerals minister William Ngeleja tabled in Parliament last July.

Mtera MP John Malecela, a former prime minister and vice-chairman of the ruling CCM, called for the tabling of the report in the last parliamentary session, saying it had raised pertinent issues that the august House needed to discuss and make recommendations.

Many MPs denounced what they said were "suspect mining contracts" and called for a thorough review or cancellation of some of the agreements.

The Bomani committee report raised eyebrows when one of the panelists declined to sign the final recommendations, arguing that they would create problems if implemented.

Other members were MPs Zitto Kabwe (Kigoma North, Chadema), Harrison Mwakyembe (Kyela, CCM), Ezekiel Maige (Msalala, CCM) and John Cheyo (Bariadi East, UDP) and Mr Peter Machunde of the Dar es Salaam Stock Exchange and Mr David Tarimo of PricewaterhouseCoopers.

Others were director of civil and international law in the Ministry of Justice and Constitutional Affairs Maria Kejo, chief legal officer at the Ministry of Energy and Minerals Salome Makange, commissioner for policy in the Ministry of Finance Mugisha Kamugisha and assistant director for human settlements in the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Edward Kihundwa.

The session due to end on November 7 will see the swearing in of the newly elected Tarime MP, Mr Charles Mwera of Chadema.

It will also ratify three declarations, including the European Union Parliament's declaration against albino killings in Tanzania.

The other two are South African parliament's declaration on xenophobic killings and the Tanzanian parliament's declaration on the expansion of Lake Manyara National Park.

The Government will also table its statements on the Tanzania International Container Terminal (TICTS) contract extension saga and Tanzania Railways Limited (TRL).

Twelve bills are also expected to be tabled and 195 questions answered.

The bills which are for the first reading are the Standards Bill, 2008, The Tanzania Trade Development Authority Bill, 2008 and The Written Laws (Miscellaneous Amendment) Bill, 2008 while The Unit Title Bill, 2008 and The Mortgage Financing (Special Provisions) Bill, 2008 would be tabled right after the first reading.

About five bills will be tabled for discussion right after the second reading. They include the Hides, Skins and Leather Trade Bill, 2008, the Workers Compensation Bill, 2008, the Wildlife Bill, 2008, the Contractors Registration (Amendment) Bill, 2008, and the Political Parties (Amendment) Bill, 2008.

If time allows three additional bills, namely the Animal Welfare Bill, 2008, the Mental Health Bill, 2008, the Public Health Bill, 2008. About 195 main questions will be asked.

The parliament would also conduct elections for members of Open University of Tanzania and the Muhimbili University of Health and Allied Science Council.

After the end of the Parliamentary session on November 7 MPs would participate at a seminar organised by the Bank of Tanzania and the Treasury on the international financial crisis.
 
Zitto ameshukuru Kikwete kumteua Kamati ya Bomani wakati akiwa amesimamishwa Ubunge.

Asema sekta ya madini inachangia asilimia 44 ya mapato ya nje lakini inachangia asilimia 3 tu katika pato la Taifa.

Asema hii ni kwa sababu sekta ya madini iko mbali na sekta nyingine za kiuchumi.

Ataka sekta ya madini iwe na uhusiano na sekta nyingine nchini.

Athibitisha madai kwa kutumia ripoti ya hali ya umaskini ya mwaka 2007. Aonyesha jinsi foward na backward linkage inavyokosekana.

"Hatuwezi kufaidika na sekta ya madini kwa kodi peke yake. Njia pekee ni kuhakikisha sekta nyingine zinahusiana na sekta ya madini"

Atumia mfano wa umeme, 'tunaisaidia vipi TANESCO kuziba soko hili katika eneo la maziwa makuu na kwenye migodi ya nickel inafunguliwa'. Avujisha siri kuwa Rwanda imeshaliona hili soko Kabanga nickel na imeanza kuwekeza.

Aanika jinsi ambavyo mgodi wa Bulyankulu uliokuwa ukimilikiwa kwa STAMICO, waliuza hisa na mwekezeji akaweka milioni 20 na kuuza bei ya juu zaidi, wamepata ziada ya dola milioni 300 na zaidi huku serikali ikiwa haijapata chochote kwa kuwa mauzo yalifanyika Toronto.

Ataka uchunguzi wa kina wa mazingira ya kuuzwa kwa hisa hizo. Ataka pia uchunguzi ufanyike kwa mgodi wa Buhemba ambao mwekezaji amekimbia na fedha alizopewa bila hata kulipa wafanyakazi, asema kwamba hapa ndipo ufisadi wa Meremeta ulipo.

Kuna malalamiko Bulyankulu kuhusu watu wamefukiwa kwenye mashimo, hata Kamati ya Nishati ya Madini ifanye uchunguzi wa kiserikali na kuona hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa.

Asema inapokuja miswada ambayo ni technical sana kamati za bunge ziruhusiwe kuajiri consultants wa kufanya impact study kabla ya kupitisha kwa kuwa kwa kipengele kimoja cha sheria kilichopitishwa, Tanzania imepoteza zaidi ya dola milioni 800 kama mapato katika kipindi kifupi.

Asema hakuna haja ya kuangalia makosa ya nyuma ila kuna haja ya kuhakikisha taifa halifanyi makosa mengine kwa kuwa huko tunapokwenda Tanzania itakuwa na migodi mingi zaidi ya nickel, mafuta nk.

Amalizia kwa kuzungumzia madhara ya ring fencing katika mgodi wa TULAWAKA

Akatisha kutokana na muda wa kuchangia bungeni kumalizika

PM
 
Habari ndiyo hiyo!



Madini yakiisha, hayaoti
 
Zitto ameshukuru Kikwete kumteua Kamati ya Bomani wakati akiwa amesimamishwa Ubunge.

Asema sekta ya madini inachangia asilimia 44 ya mapato ya nje lakini inachangia asilimia 3 tu katika pato la Taifa.

Asema hii ni kwa sababu sekta ya madini iko mbali na sekta nyingine za kiuchumi.

Ataka sekta ya madini iwe na uhusiano na sekta nyingine nchini.

Athibitisha madai kwa kutumia ripoti ya hali ya umaskini ya mwaka 2007. Aonyesha jinsi foward na backward linkage inavyokosekana.

"Hatuwezi kufaidika na sekta ya madini kwa kodi peke yake. Njia pekee ni kuhakikisha sekta nyingine zinahusiana na sekta ya madini"

Atumia mfano wa umeme, 'tunaisaidia vipi TANESCO kuziba soko hili katika eneo la maziwa makuu na kwenye migodi ya nickel inafunguliwa'. Avujisha siri kuwa Rwanda imeshaliona hili soko Kabanga nickel na imeanza kuwekeza.

Aanika jinsi ambavyo mgodi wa Bulyankulu uliokuwa ukimilikiwa kwa STAMICO, waliuza hisa na mwekezeji akaweka milioni 20 na kuuza bei ya juu zaidi, wamepata ziada ya dola milioni 300 na zaidi huku serikali ikiwa haijapata chochote kwa kuwa mauzo yalifanyika Toronto.

Ataka uchunguzi wa kina wa mazingira ya kuuzwa kwa hisa hizo. Ataka pia uchunguzi ufanyike kwa mgodi wa Buhemba ambao mwekezaji amekimbia na fedha alizopewa bila hata kulipa wafanyakazi, asema kwamba hapa ndipo ufisadi wa Meremeta ulipo.

Kuna malalamiko Bulyankulu kuhusu watu wamefukiwa kwenye mashimo, hata Kamati ya Nishati ya Madini ifanye uchunguzi wa kiserikali na kuona hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa.

Asema inapokuja miswada ambayo ni technical sana kamati za bunge ziruhusiwe kuajiri consultants wa kufanya impact study kabla ya kupitisha kwa kuwa kwa kipengele kimoja cha sheria kilichopitishwa, Tanzania imepoteza zaidi ya dola milioni 800 kama mapato katika kipindi kifupi.

Asema hakuna haja ya kuangalia makosa ya nyuma ila kuna haja ya kuhakikisha taifa halifanyi makosa mengine kwa kuwa huko tunapokwenda Tanzania itakuwa na migodi mingi zaidi ya nickel, mafuta nk.Amalizia kwa kuzungumzia madhara ya ring fencing katika mgodi wa TULAWAKA

Akatisha kutokana na muda wa kuchangia bungeni kumalizika

PM

je adhabu ya waliotufikisha hapa ni ipi na taadhari walipewa? maana wakati makosa yana fanyika wadau walipinga mikataba hii.nao walijua, kwa maana nyingini walifanya kwa makusudi , na si kutokana na kutokujua.
 
Mh. Zitto lazima uangalie nyuma sababu contract zilizosainiwa zinaangalia mbele 20yrs from now, so lazima ufanyike utaratibu wa kurekebisha hizo contracts as a right of any free country for the benefits of the citizens.
 
Date::10/29/2008
Mbunge Mkono aitishia kuikataa ripoti ya kamati ya Kikwete
Na Daniel Mjema,Dodoma
Mwananchi

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ameikataa ripoti ya kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kupitia sekta ya madini nchini, chini ya Jaji Mark Bomani hadi atakapopata maelezo ya kutosha kuhusu mgodi wa Buhemba na kampuni za Meremeta na Tangold.

“Nilidhani Ripoti ya kamati hii ya rais ingetupa tatizo hasa la Buhemba, lakini nayo inakuja na maelezo kuwa haikupata maelezo ya kutosha kutoka serikalini…sasa kama Tume ya Rais inashindwa kupata ripoti, mimi Mbunge itakuwaje,” alihoji.

Mkono alisema fedha zilizoibwa Buhemba ni nyingi kuliko za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na kusisitiza kuwa hataunga mkono hoja hiyo hadi apatiwe majibu kuwa kampuni ya Tangold inamilikiwa na nani kama iko nchini Mauritius .

“Kuna wenzetu hapa wakiwa Bungeni walipiga kelele sana, lakini wakiwa ndani (Tume ya Rais) wanakaa kimya wamepewa nini hawa…au tuko hapa kuleta usanii," alihoji Mkono na kushangaa kutoona machahari ya Zitto Kabwe katika suala la Buhemba.

Mkono, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema ni lazima kampuni za Tangold na Meremeta zichunguzwe huku akionyesha kushangazwa na namna mgodi wa Buhemba ulivyoachwa mashimo matupu huku dhahabu ikiwa imechukuliwa.

Awali katika mchango wake wa asubuhi, Kabwe alihoji namna mwekezaji wa mgodi huo alivyowekeza Dola 20 milioni za Kimarekani (zaidi ya Sh22 bilioni za Tanzania), lakini akaiuza kwa mwekezaji mwingine kwa dola 300 milioni za Kimarekani.

Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka(CCM) alishangaa kutofanyiwa kazi kwa ripoti ya Jenerali Mboma ambayo ilichunguza mgogoro kati ya wachimbaji wadogo na kampuni ya Tanzanite One.

Akionyesha kukerwa na uundwaji wa kamati na tume kila mara, alisema binafsi asingeshauri kuundwa kwa kamati au tume nyingine kabla ya kuzifanyia kazi taarifa za kamati zilizotangulia kama ile ya Jenerali Mboma, ambayo imewekwa kabatini.

Alishangaa serikali kupokea mrabaha wa dola 1.4 milioni za Kimarekani kwa miaka 10 kutoka kampuni ya Tanzanite One akisema huo ni wizi kwa sababu kampuni hiyo imekuwa ikipata mapato makubwa ukilinganisha na kile ilicholipa serikalini.

Katika hatua nyingine, Bunge limemshauri Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi mazito kwa maslahi ya nchi, ikiwemo kusitisha utiaji saini wa mikataba mipya ya madini hadi sheria mpya itakapopitishwa na chombo hicho.

Mbali na suala hilo, Bunge limependekeza kufanyika kwa uchunguzi maalumu wa jinsi serikali ilivyouza hisa zake zake za migodi mitatu na mahali fedha zilipotumika na taarifa ziwasilishwe Bungeni.

Hisa ambazo serikali iliziuza ni zile zilizokuwa katika migodi ya Kiwira, Bulyanhulu na Mwadui na pia serikali imeshauriwa kusitisha uuzaji wa hisa zake katika migodi mingine ikiwamo ya Buckreef Gold Mine, Kiwira Coal Mine na Williams Diamonds Ltd.

Kadhalika Bunge limependekeza kuwa asilimia 70 ya fedha zote zinazotokana na mauzo ya madini nje ya nchi zirejeshwe nchini kwa matumizi ya ndani badala ya makampuni kuzitumia nje ya nchi.

Mapendekezo hayo yamo katika taarifa ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu taarifa ya Kamati ya Rais ya kuishauri serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini iliyowasilishwa Bungeni jana.

Taarifa hiyo ya kamati, ambayo inaonekana kuwa msumari wa moto kwa wawekezaji wa kigeni na kuwarejeshea Watanzania matumaini, iliwasilishwa bungeni na mwenyekiti wake, William Shelukindo.

Kutokana na Tume ya Jaji Mark Bomani kubaini mapungufu na udanganyifu mkubwa katika sekta ya madini, Bunge limependekeza kufutwa kwa msamaha wa ushuru wa mafuta kwa wawekezaji hao.

Sheria ya kodi ya zuio (Withholding Tax) inataka malipo yote yanayofanywa na kampuni za madini kwa kampuni za ndani na za kigeni zinazotoa huduma za menejimenti na utawala, zikatwe kodi hiyo.

Hata hivyo Shelukindo alisema Tume ya Jaji Bomani imegundua kuwa kampuni za ndani zinatakiwa kukatwa asilimia 5 wakati za kigeni ni asilimia 15, lakini baadhi ya kampuni zenye mikataba zinakata asilimia 3.

“Kamati yangu inakubaliana na kamati ya rais kuwa huu ni ukiukwaji wa utawala wa sheria, Mikataba ya kibiashara inajidhihirisha kuwa na nguvu zaidi ya sheria ya nchi…hii haikubaliki kabisa,” alisema Shelukindo.

Shelukindo alisema kwa kuwa suala la mikataba ya madini limeonekana kugubikwa na matatizo makubwa ya usiri, utata na vipengele vinavyokiuka sheria za nchi na hivyo sheria ya madini ya mwaka 1998 iandikwe upya.

Ili kuondoka na na wawekezaji uchwara, kamati hiyo imependekeza kuwa kwa kuanzia, ili kampuni iweze kuwa na mkataba na serikali, ni lazima uwekezaji wake uanzie dola 600,000 za Kimarekani.

Kamati hiyo imeonyesha kushangazwa na hatua ya serikali kurudisha kipengele kimoja cha kodi kinachompa mwekezaji unafuu wa ziada wa asilimia 15 kwenye gharama za uendelezaji migodi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kifungu hicho kinachotoa unafuu huo wa kuikamua nchi kilifutwa mwaka 2001, lakini mwaka uliofuata kifungu hicho kikarejeshwa tena kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2002.

“Maelezo ambayo kamati ya Rais iliyapata ni kwamba serikali ilishinikiza kukirejesha tena kifungu hicho. Haya hayafurahishi kuyasikia na tunaungana na mapendekezo ya tume kuwa kifutwe mara moja,” alisisitiza Shelukindo.

Kuhusu mikataba mipya ya madini, kamati hiyo imependekeza mikataba hiyo iwe wazi kwa wananchi na ipatikane katika ofisi za mikoa, wilaya na halmashauri ambazo zina migodi hiyo.

Pia kamati hiyo ipendekeza kupunguzwa kwa uhai wa mikataba ya madini kutoka miaka 25 ili itoe fursa ya kupitiwa kila baada ya miaka mitano kwa lengo la kuongeza ufanisi kulingana na mabadiliko yatakayojitokeza katika uchumi wa nchi na dunia kwa ujumla.

Awali kabla ya kuwasilisha kwa taarifa hiyo ya kamati, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwasilisha muhtasari wa taarifa ya Tume ya Jaji Bomani ikianisha mapungufu kibao katika sheria na sera za madini.

Ngeleja alisema kulingana na ripoti hiyo,sekta ya madini inakabiliwa na changamoto, ikiwemo mchango wake mdogo katika pato la taifa, madini kuendelea kuuzwa yakiwa ghafi na uchimbaji duni wa wachimbaji wadogo na kupendekeza kufanyiwa marekebisho kwa sheria na sera hizo.

Waziri Ngeleja alisema kutokana na kutolewa kwa taarifa hiyo, tayari kikosi kazi kimeundwa ili kuangalia namna bora ya kutekeleza mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo ya Tume ya Rais.

Awali wabunge walipendekeza uchimbaji wa madini ya vito yakiwemo madini adimu ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee ufanywe kwa asilimia 100 na Watanzania na sio wawekezaji kutoka nje.

Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki,Anna Kilango Malecela(CCM) alienda mbali na kuitaka Serikali ivunje mkataba na kampuni ya Tanzanite One ya Mererani hata kabla ya muda wa kisheria wa mkataba kumalizika.

Akichangia ripoti ya kamati ya Rais ya kuishauri serikali kuhusu usimamizi wa Sekta ya Madini Bungeni jana, Kilango wachimbaji wadogo wanao uwezo wa kuchimba madini ya vito kwa kutumia mitambo midogo.

Ingawa Kilango hakuitaja Tanzanite kwa jina Bungeni lakini katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana alisema kampuni aliyokuwa akiilenga ni Tanzanite ambayo zamani ikifahamika kama Afgem.

“Nimefanya utafiti wangu na kugundua kuwa leseni yao (Tanzanite One) inamalizika mwaka 2012 mimi naona huko ni mbali ukilinganisha na hasara tutakayopata tusitishe leseni yao sasa”alisema Kilango.

Kilango alisema uchimbaji wa madini ya vito kwa kutumia mitambo mikubwa sio endelevu na kuonya kuwa kiasi cha madini kinachochimbwa na kuhifadhi nje ya nchi ni kikubwa huku Tanzania ikiachiwa mashimo.

Mbunge huyo ambaye ni mmoja wa Wabunge Machachari alisema ni vyema Serikali ikasitisha mkataba huo sasa na kulipa fidia ambayo inaweza kuwa ndogo ukilinganisha na madini mengi yanayochimbwa.

Alionya kwa vile kampuni hiyo sasa inafahamu kuwa uchimbaji wa madini ya Vito utafanywa na Watanzania kwa asilimia 100 wanaweza kuchimba kwa nguvu ili kufikia 2012 madini ya Tanzanite yawe yamekwisha.

“Siku zote kutoa maamuzi magumu ndio kuendelea na huu ni uamuzi mgumu lakini tumwambie Rais kuwa sisi Wabunge tunamuunga mkono na tuko tayari kuchangia fidia kusitisha mkataba huu”alisema.

Mbunge wa Busega,Dk. Raphael Chegeni (CCM) alishangaa Tanzania kuwa nchi ombaomba wakati imebarikiwa rasilimali kubwa ya madini akitaka serikali ianye maamuzi magumu kwa maslahi ya Watanzania.

“kule kwetu kuna dhahabu hebu niambieni ni wapi katika nchi mgeni anamiliki mgodi kwa asilimia 100,ni lazima tubadilike na suala la umiliki wa migodi ya madini litazamwe upya”alisema Dk. Chegeni.

Dk. Chegeni aliunga mkono mapendekezo ya kamati ya Jaji Bomani ya kutaka wawekezaji wa kigeni wanaokuja nchini wakijifanya wawekezaji na kuvuna rasilimali za Tanzania na kuondoka kama hazina mwenyewe.

“wawekezaji brief case(wa mifukoni) hatuwataki wanaokuja wawe na mtaji ili kuwaengua wawekezaji uchwara…yaani wanafanya Tanzania kama shamba la Bibi wanakuja wanachukua wanaondoka”alisema.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Kabwe Zitto,(CHADEMA) alihoji inakuwaje madini yanachangia asilimia 40 ya mapato ya mauzo nje ya nchi lakini hapa nchini yanachangia asilimia 3 tu ya pato la Taifa.

Kabwe alitaka kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ichunguze madai ya kufukiwa kwa wachimbaji wadogo katika mgodi wa Bulyahulu akisema kamati ya Rais chini ya Jaji Bomani ilipokea malalamiko hayo.

Akiwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,William Shelukindo alipendekeza utaratibu wa kusafirisha madini ghafi nje ya nchi kwa ajili ya usafishaji na ukataji ufutwe.

“suala hili limezua mjadala sana kiasi cha kamati yangu kuhoji kama ni kweli Taifa letu halina uwezo wa kufanya shughuli hizi hapa nchini”alisema Shelukindo ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli.

Shelukindo aliliomba Bunge kuiagiza serikali kupeleka Bungeni muswada wa sheria ndani ya mwaka mmoja ambao utazuia usafirishaji wa madini ya vito ghafi, yakiwamo madini ya Tanzanite ambayo yanachimbwa Tanzania pekee.

Aliitaka serikali kulipa uzito suala hilo ili kujenga ajira nchini na hivyo kubakiza kiasi cha fedha ambazo zinapatikana kwa shughuli za madini hapa nchini kwani pia itasaidia kujua kiasi hali cha madini kinachosafirishwa ikiwa ni pamoja na kuyaongezea thamani.

Alisema kamati yake pia imeguswa na suala la upendeleo wa ajira katika makampuni ya kigeni ya madini kati ya Watanzania na wageni na kuitaka serikali izipitie upya sheria za kazi na pale anapohitajika kuajiriwa mfanyakazi wa kigeni basi iwe ni kwa utaalamu ambao haupo nchini.
 
Nimekaa hapa sina mbavu! magoli mengine hata refarii anaweza kupiga kipenga hata kabla mpira haujagusa nyavu kwani golie hayupo langoni!
 
Huyu Nkono amesema akiwa na akili timamu au?
Sema hapa sioni kama kuna kitu ktakachofanyika,kama kawaida yetu tu mwaka huu mwaka ule mpa dunia iishe.
 
Kwanza Mkono kajiuzulu kuwa mwanasheria wa kampuni za madini? Tutajuaje kwamba hataki hizi habari kwa manufaa ya wateja wake ambao baadhi yao ni makampuni makubwa ya madini nchini?


Hakuna sala la "conflict of interest" hapa?
 

"Kuna wenzetu hapa wakiwa Bungeni walipiga kelele sana, lakini wakiwa ndani (Tume ya Rais) wanakaa kimya wamepewa nini hawa…au tuko hapa kuleta usanii," alihoji Mkono na kushangaa kutoona machahari ya Zitto Kabwe katika suala la Buhemba.

Mkono, you are right. Huyu Zitto hapa anatufanyia usanii.

Anakuja na maswali mapya (au sijui mazee) kuhusu sekta ya madini na madai mengine kwamba Bunge liunde tume. You just got off a Tume Zitto!!!

Kwanini hizo issue zake Zitto hakuzi address kwenye tume yake?

Bongo bwana!
 
Mkono, you are right. Huyu Zitto hapa anatufanyia usanii.

Anakuja na maswali mapya (au sijui mazee) kuhusu sekta ya madini na madai mengine kwamba Bunge liunde tume. You just got off a Tume Zitto!!!

Kwanini hizo issue zake Zitto hakuzi address kwenye tume yake?

Bongo bwana!

nadhani kama zitto angeyasema hayo aliyoyazungumza bungeni jana bila shaka kwenye ripoti yangeonekana.lakini pia inawezekana aliyazungumza huko kwenye tume aliyoshirikishwa na ameamua kuyasema kwa faida ya wabunge na watanzania kwa ujumla.
ili kujua yale yote yaliyojadiliwa na kupendekezwa na kamati ya bomani, tunamuomba mh.zitto atuwekee hapa hiyo ripoti pamoja na ripoti ya shelukindo aliyoitaja kuwa ni radical.tukizipata hizo ripoti tukazisoma ndipo tutaweza kuwa na mjadala mzuri zaidi kuliko hivi sasa.tafadhali mh.zitto au member yeyote mwenye hizo ripoti atuwekee hapa tuweze kuzijadili.
 
Paparazi, hiyo ripoti mbona hujatuletea, umeeleza maneno ya Zitto tu!
 
Back
Top Bottom