Mkuu Mkandara,
Hao Mwakyembe na Sitta wako tayari kutumia greda kukwangua chochote kinachozuia ambitions zao.
Hata siku moja huwezi kuwa mpiganaji wa wananchi huku unatafuna wananchi hao hao.
Wengine tumeonja joto ya jiwe ya mbinu na siasa chafu za hao wapiganaji wenu.
Leo hii Mkandara ukiamua hata kwa kujaribu kugombea jimbo la Sita au yule Sendeka, utaipata joto ya jiwe ya hao wapiganaji wenu. Ghafla utakuwa umetumwa na Lowassa hata kama maishani mwako hujawahi kuonana na Lowassa. Ghafla utakuwa umepewa bilioni moja hata kama mfukoni unahangaika hata kupata laki moja ya kumsaidia campain manager wako.
Mtu anayeweza kukaa na kupanga jaribio la kuuawa na kuudanganya umma mzima huku anajua ni uongo, ni mtu wa kumwogopa sana maana akiwa na nafasi sidhani kama ataogopa kukuweka ndani au kukumalizia mbali ili kusafisha njia yake.
Mtu ambaye yuko tayari kuangamiza wapinzani wake kwa njia zozote zile haramu hata siku moja hawezi kuwa mpiganaji wa wananchi.
Mimi naamini usafi lazima uanzie kwangu; lazima nijisafishe mimi kwanza kabla hata ya kujaribu kumsafisha mkandara.
Usipoamini katika sheria na uongozi wa haki, hata siku moja usitegemee utaweza kuwa polisi wa kusimamia sheria na haki nyumbani kwa mtu mwingine.
Haya yanayotokea sasa ni vizuri yatokee ili kila mtu aone CCM ilipofikia na aina ya watu walioko huko ndani. Kizuri zaidi inaonyesha mahali ambapo Watanzania tumefikia na bila kubadilika tusigemee maendeleo yoyote ya maana.
Kundi la Sitta walimpata Lowassa na kundi lake kwenye Richmond na mimi naamini ilikuwa nafasi nzuri ya kuisafisha serikali. Lakini kilichowaponza ni furaha ya kupata nafasi ya kumdhuru mbaya wao, wakasahau kuwa waangalifu na kuhakikisha katika hiyo assasination wanakuwa fair na wanawapa nafasi ya kutosha hao watuhumiwa kuweza kujitetea. Kila mtu anajua Karadzicz kule Serbia aliua wabaya wake lakini dunia inampa kila nafasi ya kujitetea hata kama ni obvious kwa kila mtu kwamba jamaa hawezi kushinda case. Wahandisi tunasema garbage in garbage out. Ukiharibu process ya kitu chochote, mwisho wake unapata madudu.
Hata wananchi wa vijijini tayari wanaanza kuelewa nani anasema ukweli, nani ana nia ya dhati kutetea maslahi yao, nani wanaimba ngonjera na wote tutajua ukweli hapo 2010.
Rev. Kishoka,
Mkuu twende mbele turudi nyuma kidogo..
Hivi mnawafikiria CCM wajinga kiasi gani vile.. Yaani hawa wapiganaji kama sii lolote sii chochote iweje hili swala la Richmond limewakuna Mafisadi kiasi hicho.. imefikia hata watu kutukanana matusi ya nguoni, kumbuka ugonvi wa mkutano wa Kamati kuu ya chama, lugha zilizotoikea pale..Leo hii wewe mkuu wangu unazungumza LUGHA ya Sophia Simba, wewe mchungaji unakubaliana na kina Sophia kwamba hata kina Sitta ni mafisadi ktk utetezi wa mtu Fisadi..
Mkuu wangu yawezekan Sitta fisadi lakini kesi moja baada ya nyingine, Marekani walikwenda Afghanstan kwa sababu ya 9/11 na dunia tulikuwa nyuma yao, sasa kama tungeanza kusema marekani nao ni Materrorist size yao kweli hali ya maisha yetu Ulaya ingekuwa hivi..Sote kwa ujumla tulilaaani terrorism kwa sababu sote tulikuwa hatarini na kama tungeshangilia hayo matokeo yake kina Osama wangepiga miji yote ya Marekani na nchi zote za Ulaya kwa sababu sisi tumewapa nguvu.
Ndicho mnachokifanya hapa..mnashindwa ku take a stand badala yake mnakumbwa ktk kiza kinene cha mbinu za mafisadi.. Ikiwa Mwakyembe na Sitta ni mafisadi kwa nini kesi zao hazifikishwi bungeni au mahakamani... Kama iliwezekana kuchukuza BoT, EPA, Richmond na mashirika mengine iweje shida kuwafikisha mahakamani watu hawa badala yake zinapigwa simu za kuhoji wabunge na posho zao.
Of all Ufisadi jamani posho imekuwa kitu cha kujibu mapigo!
Mkuu wangu Uhasibu nimeufanya na naelewa wazi kabisa malipo yoyote yale ya serikali yanapitishwa vipi..Mbunge hawezi kuilazimisha wizara kutoa posho isipokuwa serikali yenyewe iliweka posho hizo ktk kifungu cha matumizi toka mwanzo, besides kuchukua posho mbili sioi crime hata kidogo maadam invoice na cheki vimepitishwa kisheria na maofisa wanaotakiwa kupitisha. sana sana mbunge huyoi atatakiwa kurudisha fedha alizopewa zaidi, kama hana atakatwa ktk mshahara au posho zijazo lakini posho mbili sio swala la RUSHWA hata kidogo kwani lipo ktk kifungu cha matumizi ya wizara, shirika au taasisi. Kama kuna kukamata mtu basi yule aliyepitisha matumizi hayo ndiye wa kushinkwa koo..
Pili, hapakuwa na sababu kabisa ya Hosea kwenda Bungeni wakati wa bunge ati kumwona Spika..Mkuu wangu, vita hii isingekuwa kubwa hivi kama kweli hawa wote lao ni moja..