Habari Wana Jamii, Habari Wana Soka.
Leo ni "Afe Kipa, Afe Beki - Bukta Chanika, Boxa Vuuka - Lazima Kieleweke" limeanza amsha amsha na kuwekwa wazi kwa team vichwa ngumu barani ulaya, zilizoamua kusaliti kambi na kuanzisha League yake, hii ni baada ya kuona
"UEFA & FIFA" ni wahuni na wapangaji wa matokea ya mechi juu ya meza kwa kushinikizwa na makampuni ya kucheza kamali (Betting Companies).
Team zitakazo shiriki michuano hio zitapewa € Billion 3.5 kwaajili ya kujiwekeza katika maswala mbali mbali ya team zao (Kama kuboresha viwanja n.k), nia na madhumuni ni kuwapa mashabiki wa mpira mechi zilizo bora na kali kuliko zinazochezwa katika
"UEFA & EUROPEAN LEAGUE" kwa sasa hivi. Mechi ambazo pia zitachezwa katikati mwa week kama zilivyo za UEFA hivi sasa, na weekend kuachia dirisha za mechi za ligi za ndani kama ilivyo.
Ligi itahusisha team 20, 15 ambazo ni timu mama za league na nyingine kupita kwa vigezo vya nafasi watakazopata katika misimamo ya ligi za ndani.
Leo mara baada ya kutangazwa rasmi kwa kuanzishwa League hio ambayo inaonekana kuwa
"TISHIO KUBWA KUWAHI KUTOKEA" hasa kwa UEFA & FIFA, taharuki imetanda baada ya tamko kutoka kwa UEFA & FIFA kukemea na kulaani kwa kuanzishwa kwa michuano hio.
Licha ya tamko la UEFA & FIFA kulaani kitendo hicho na kukiita ni ha
"KIHUNI KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA SOKA", walienda mbali na kusema kwamba
"TEAM YOYOTE ITAKAYOSHIRIKI MICHUANO HIO BASI ITAFUNGIWA KUSHIRIKI UEFA, EUROPA NA LEAGUE ZA NYUMBANI KWAO (National League)", na kuendelea kusema kwamba wachezaji watakao shiriki michuani hio watafungiwa kushiriki
"WORLD CUP na EUROPE CUP".
Jambo hili limepelekea UEFA kuahirisha kwa muda usiojulikana mechi zilizosalia za Michuano ya UEFA, ambazo ni
"MANCHESTER CITY VS PSG" na
"CHELSEA VS REAL MADRID". Na kusema wataitisha kikao cha dharura na kujadiliana kumpa ushindi wa mezani PSG kwenye michuano ya
"UEFA CHAMPIONS LEAGUE".
Mwenyekiti wa michuano hio mipya ya
"EUROPEAN SUPER LEAGUE", anaeitwa na kutambulika na
"UEFA & FIFA" kama mhuni mkuu Bwana Fiorentino Pérez nae hakusita kutoa tamko ya kwamba
"MKIWAFUNGIA WACHEZAJI WETU KUCHEZA WORLD CUP QATAR, SIO TATIZO KUBWA KWETU KABISA, KWANI TUTAANZISHA NA WORLD CUP YETU".
Team zenyewe ni 12, ambazo zinatambulika kama
"WAASISI WA EUROPEAN SUPER LEAGUE", ni;
1) AC Milan (Italy).
2) Arsenal (England).
3) Atletico Madrid (Spain).
4) Chelsea (England).
5) Barcelona (Spain).
6) Internazionale - Inter Milan (Italy).
7) Juventus (Italy).
8) Liverpool (England).
9) Manchester City (England).
10) Manchester United (England).
11) Real Madrid (Spain).
12) Totenham Hotspurs (England).
Wadau wa soka na kubeti, nimewaita tujadiliane
Karibuni kutoa mitazamo yenu na updates kuhusu swala hili.
View attachment 1757074View attachment 1757075