Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Kikao cha mwisho tulikubaliana kuwa bwawa likikamilika hatutahangaika tena kuhusu umeme, zaidi tutakuwa na umeme wa kutosha hadi tutauza kwa majirani. Ghafla mama akiwa Same amesema itabidi tununue umeme Ili kuzuia umeme kukatika Kanda ya kaskazini.
Kwaiyo mheshimiwa Samia tukuamini kwenye lipi?
Je tuamini bwawa litamaliza tatizo la umeme au tuamini mpango wako mpya wa kununua umeme nje ndo utamaliza tatizo la umeme kaskazini?
Je swala la sisi Tanzania kuuza umeme ndo limekufa hivo au sisi ndo hatukuelewa vizuri uliposema tutauza umeme nje? au ulimaanisha baada ya bwawa kukamilika tutanunua umeme nje ?
Mtangulizi wako alikuwa bingwa wa kusema na KUTEKELEZA, wewe ni bingwa wa kusema na kuja kubadilisha ulichokisema baadae.
Hizi hotuba hawa jamaa wanakuchomekea tu unakuja kukutana nazo wakati wa kusoma tu au umedhamiria tu kutudanganya danganya kama watoto?
Mama Samia kuwa makini, watanzania tunakuangalia tu ila tushakuelewa kuwa wewe ni bora liende, maana haiwezekani tupambane kuzalisha umeme megawatt 2000 alafu Leo uje utuambie eti unapanga kununua tena umeme, isije ikawa washakuchomekea Ile mipango ya RICHMOND, ESCROW NA MEREMETA. Mambo ya kusema nyeupe Leo kesho unasema nyeusi yanatutia mashaka.
Je tutauza umeme, au tunauziwa umeme

Attachments
-
IMG-20250310-WA0023.jpg128.6 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0018.jpg51.6 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0014.jpg99.9 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0013.jpg88.3 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0006.jpg76.8 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0003.jpg47.6 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0002.jpg85.4 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0004.jpg13.3 KB · Views: 1 -
IMG-20250310-WA0000.jpg107.8 KB · Views: 1