kisikichampingo
Senior Member
- Oct 28, 2009
- 129
- 9
- All right, the more dataz ni kwamba Muungano uko kwenye life support, wanaomfahamu Karume kwa karibu sana wanadokeza kwamba hataki Muungano, wanasema hivi karibuni katika kikao kimoja cha Jumuiya, aliwakoromea sana Burundi na Rwanda, kwamba kwa nini wanataka kurudia makosa ya baba yake ya kujiingiza kwenye Muungano na mataifa makubwa, na kwamba baba yake alifanya makosa makubwa sana kujiingiza na bara kwa sababu siku zote miungano ya taifa kubwa na dogo, huishia kuumiza taifa dogo to the shock ya wasaidizi waliokua naye!
- The dataz ni kwamba katika moja ya kikao cha siri kati ya Seif na Karume, waliwekana sawa kwamba, wao wawili ndio Zainzibar ya sasa hakuna cha bara wala CCM, at one point Seif anasadikiwa kumuambia Karume, "..mimi nina umma na wewe una dola...sasa....wabara wa nini yakhe....!", wanaowafahamu wote wawili kwa karibu sana wanasema kwamba wote wawili wanaunganishwa na one principle ya kutoutaka muungano!
- NEC ya mwisho ilipoitishwa Karume hakuja kwa kisingizio cha kwenda kutibiwa nje, this time ameamua kuita kikao maalum huki visiwani siku ya kikao cha CC bara, pamoja na kwamba amearifiwa toka last weeek!
- The more dataz ni Kigogo mmoja wa CCM (jina tunatunza), aling'amua mapema kwamba huko visiwani kuna something fishy, akamfahamisha Muungwana na nini cha kufanya, yaani kumuita Karume mara moja Dodoma kwa siri na kumkalia kooni, Muungwana kwa kutotaka kuonekana anafuata fuata ushauri tu wa wengine na sio maamuzi yake mwenyewe, akaukataa ule ushauri na kuamua yeye binafsi kuitisha kikao cha CC na NEC kule Dodoma, Karume akachomoa na kwenda nje kutibiwa!
- Now to make this dataz story interesting, comes the main man the one and only Rostam in the picture!
......stay....tuned....!
Respect.
FMEs!
Hakuna kiongozi atakayezuia kuvunjika kwa muungano. Tanzania ya sasa haina viongozi design ya akina Nyerere, Kawawa, Hayati Karume na Thabit Kombo. Tanzania ya sasa inaongozwa na wasanii.
Hebu fikiria jinsi Amani na Seif walivyofanya mkutano wao wa siri bila kumhusisha Kikwete wala CCM!
Tuko pamoja mkuu lakini cha kukumbuka ni kwamba democracy isiyo na mipaka ina hatari zake.Hata viongozi wa dini hutumia rungu walilokabidhiwa mambo yanapokuwa magumu. Kama kila mtu ataachwa afanye kila analotaka kwa kisingizio cha democracy kumbe kazi ya kiongozi ninini?Bravo Kikwete!
Huendeshi nchi kwa mabavu wala hisia binafsi, huu ni mfano bora wa kuigwa na watawala wengine.
Urais si madaraka ya kutumia ubabe na ukandamizaji. Ninafurahi kuona kuwa Rais anaendesha nchi na kuhakikisha kila mtu ana pata fursa ya kutosha ya kuweka mawazo yake katika uso huu wa dunia (kama huitumii kikamilifu fursa hiyo basi anza sasa).
Juu ya mambo ya Zanzibar, rais si mwarobaini wa matatizo ya wazanzibar. Hatma ya matatizo ya Wazanzibari yapo mikononi mwao wenyewe. Zanzibar ina viongozi wengi tu tena wazuri sana na wanafanya maamuzi yenye maslahi kwa ajili ya wazanzibari wote. Historia ya visiwa hivyo na wananchi wake ni lazima ilindwe kwa gharama yeyote, na kinachoweza kuilinda historia hiyo ni kuwepo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar period
You are day dreaming!!Kisikichampingo, FMES na Wengine,
Naamini kwa asilimia 300 kuwa Muungano kamwe hautavunjika na hakuna kiongozi aliye na ubavu au uthubutu wa kufanya hivyo. Kwa upande mwingine ni muhimu JK akaendelea kukaa kimya.
- Haya mambo ni mazito sana, I hope Muungwana amepata message!
- Sasa dawa kikao kijacho cha CC, kifanyikie huko huko Visiwani tuone huu usanii wa hawa kina Karume! Halafu mbona hawasemi kuhusu kikao cha CC kilichopangwa hapa Dar!
Respect.
FMEs!
😛
You are day dreaming!!
Hayo maombi unayofanya ni mazuri lakini binafsi unafanya nini ili kuhakikisha muungano hauvunjiki? Hautavunjika hivihivi tu bila jitihada zozote za kuunusuru? JK aliahidi kwamba atashughulikia in person suala hili lakini utaona kwamba kwa sasa amekaa kimya, unadhani mambo bado yako sawasawa sawia na alivyokuwa anafikiri wakati anahutubia bunge pale Dodoma?
Naamini jibu ni hapana.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Amani Abeid Karume na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dk. Ali Mohamed Shein wakipiti makabrasha ya ajenda mbalimbali, kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika CCM Kisiwandui mjini Zanzibar jana. (Picha na Amour Nassor)
Picha kwa hisani ya Father Kidevu.
Rostam jina lake linaingiaje hapa? is he the hot issue being discussed? Au hapa JF kuna watu ambao akili zao hazitulii bila kutaja Rostam? Katika hili la Muungano Rostam si lolote wala chochote, ukija kwenye fedha za uchaguzi, basi hapa atkuwa papa!
Kaka kama utabiri wako ukitimia, hayo ya Zanzibar itakuwa sio uongozi wa SMZ tena, bali litakuwa duka la marehemu Karume Sr. Na kwamba aliwaachia urithi watoto wake!!Jayfour_King,
Wala sioti Mkuu na huo ndiyo ukweli. Naomba kurudia tena, Kamwe Muungano hautakaa uvunjike. Hivi Seif kusema Karume aongezewe muda ni tatizo? Zanzibar tatizo lake kubwa ni kuwepo uchaguzi ulio huru na wa haki na hapo ndiyo penye tatizo. Hali ya kisiasa Zanzibar si mbaya kama ambavyo tunajaribu kuonyesha hapa. Tukumbuke katika kikao cha jana Rais AAK ameweka wazi kuwa hataongeza hata siku moja.
Binafsi nawapenda sana watu wa Unguja na Pemba. Huo ndiyo mchango wangu mkuu katika kuhakikisha Muungano wetu hauvunjiki kamwe.
Kwangu mimi pia sioni haja ya kuwa na Serikali ya mseto kama uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki. Kwa upande mwingine kuna uwezekano mkubwa sana kwa Ali Abeid Karume (AAK, Jr) kuwa Rais mpya wa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. AAK (Ali) yeye aliisha weka wazi kuwa akiwa Rais wa Zanzibar kitu cha kwanza atakachofanya ni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hili naliafiki na ninaamini ndiye Rais ajaye wa visiwa vya Unguja na Pemba.
lakini pamoja na mambo hayo yote yanayoendelea kunaonekana kama Karume anamdharau sana JK, yaani kinachoonekana hapo ni kuwa kuna mambo ya upumbavu ambayo JK ameyafanya au anayafanya kwenye uongozi wake ambao moja kwa moja inaithathiri Zanzibar,
1) issue ya umeme kwa kweli inawaumiza sana Wazanzibar, hata kama sasa inawapasa kulipia, lakini ukiangalia mikataba mibovu iliyoingiwa na serikali ya Muungano kwa kweli Wazanzibar kama nchi ni kuwatwisha mzigo usiowafaa na usiowahusu
2) kwenye issue ya Mafuta nadhani kwa Wazanzibar wengi (Wapemba) nadhani hapo ndipo ugomvi mkubwa ulipo, kama Muungano wetu umekubali kuwe na nchi mbili Zanzibar na Tanzania?, na serikali ya Zanzibar ina wizara zake iweje mikataba ya mafuta isainiwe Kwenye serikali ya muungano bila kuwashirikisha serikali ya Zanzibar, kama umeshawapa wageni dhahabu bure Tanzania iweje uwape Mafuta ya zanzibar bure pia
kwa kweli Karume kukubaliana na Ahmadi, hata kama ungekuwa wewe ungekubali tu, hii nchi imekosa mwelekeo, Raisi yupo kama hayupo, hivyo kama Wanzanzibar hawakuungana sasa na kuwa wamoja itakuwa ngumu sana kwao pale serikali ya JK itakapopata pigo kuu, maana sasa inafikia point Mzee Mwinyi ndio anakuwa raisi wa nchii hii, NAona kuna watu humu jamviini wanasema bora raisi akae kimya hivyohivyo, hapana sio kukaa kimya, mambo yameshamfika shingoni sasa yeye kama mwenyekiti wa Chama, control ya chama hana kabisa anamsumbua Mzee wa watu (Mwinyi), ambaye sasa alikuwa anahitaji utulivu mkuu, na control ya chama hana kwa sababu ya kuendekeza ushwahiba kiasi cha kushindwa hata kuongea ukweli kwa rafiki zake
pamoja na Mwinyi na Msekwa pamoja na Shain kutoka Zanznibar, hayo ya Zanzibar hayajesha yakhe, kama shinikizo litakuwa kubwa kutoka CCM, kunauwezekano mkubwa wa kuanzishwa chama kingine ambacho kitaaccomodate Wazanzibar wote (CCM na CUF), kwa Maslahi ya nchi yao

Na huo ndio mwanzo wa matatizo yetu, kiongozi ukiwa unaboronga boronga, na wasaidizi wako na wale wanaoitakia mema nchi wanakushauri kwa nia njema nawe unawapuuzia huku nchi inakwenda mrama wewe unatabasamu na kutalii tu,WATAKUDHARAU,tena sio kwa siri, bali hata hadharani.lakini pamoja na mambo hayo yote yanayoendelea kunaonekana kama Karume anamdharau sana JK,