lakini pamoja na mambo hayo yote yanayoendelea kunaonekana kama Karume anamdharau sana JK, yaani kinachoonekana hapo ni kuwa kuna mambo ya upumbavu ambayo JK ameyafanya au anayafanya kwenye uongozi wake ambao moja kwa moja inaithathiri Zanzibar,
1) issue ya umeme kwa kweli inawaumiza sana Wazanzibar, hata kama sasa inawapasa kulipia, lakini ukiangalia mikataba mibovu iliyoingiwa na serikali ya Muungano kwa kweli Wazanzibar kama nchi ni kuwatwisha mzigo usiowafaa na usiowahusu
2) kwenye issue ya Mafuta nadhani kwa Wazanzibar wengi (Wapemba) nadhani hapo ndipo ugomvi mkubwa ulipo, kama Muungano wetu umekubali kuwe na nchi mbili Zanzibar na Tanzania?, na serikali ya Zanzibar ina wizara zake iweje mikataba ya mafuta isainiwe Kwenye serikali ya muungano bila kuwashirikisha serikali ya Zanzibar, kama umeshawapa wageni dhahabu bure Tanzania iweje uwape Mafuta ya zanzibar bure pia
kwa kweli Karume kukubaliana na Ahmadi, hata kama ungekuwa wewe ungekubali tu, hii nchi imekosa mwelekeo, Raisi yupo kama hayupo, hivyo kama Wanzanzibar hawakuungana sasa na kuwa wamoja itakuwa ngumu sana kwao pale serikali ya JK itakapopata pigo kuu, maana sasa inafikia point Mzee Mwinyi ndio anakuwa raisi wa nchii hii, NAona kuna watu humu jamviini wanasema bora raisi akae kimya hivyohivyo, hapana sio kukaa kimya, mambo yameshamfika shingoni sasa yeye kama mwenyekiti wa Chama, control ya chama hana kabisa anamsumbua Mzee wa watu (Mwinyi), ambaye sasa alikuwa anahitaji utulivu mkuu, na control ya chama hana kwa sababu ya kuendekeza ushwahiba kiasi cha kushindwa hata kuongea ukweli kwa rafiki zake
pamoja na Mwinyi na Msekwa pamoja na Shain kutoka Zanznibar, hayo ya Zanzibar hayajesha yakhe, kama shinikizo litakuwa kubwa kutoka CCM, kunauwezekano mkubwa wa kuanzishwa chama kingine ambacho kitaaccomodate Wazanzibar wote (CCM na CUF), kwa Maslahi ya nchi yao