Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!

Kama Kikwete angekuwa na ubavu angewakamata wote Karume na Seif kwa uhaini. Wanachofanya ni uhaini. Lakini anao ubavu? Ultimately itabidi yeye ndiye ashtakiwe kwa kutoilinda katiba ya Mwungano wa Jamhuri ya Tanzania kama alivyoapa. In any case it is not as easy as it may look to the Zanzibaris.
 
I see!! This is very interesting; it can happen as everything is possible in Tanzania. Hiyo wala sikubishii. I am puzzled after learning this if it is true.
 
I see!! This is very interesting; it can happen as everything is possible in Tanzania. Hiyo wala sikubishii. I am puzzled after learning this if it is true.

Katika Rostam nimelisikia hapa JF ila nilisikia kuwa waliokuwa involve na Richmond wako katika dili hili la mafuta sasa mie nilikuwa nadhani Lowassa ila sijamrule out maana Rostam na Lowassa ni kama mtu na kaka yake. Tupe wewe data ulizonazo!!!
 

- Sawa saawa mkuu, anyways nitarudi in two hours hopefully na more dataz! ingawa mawasiliano hayapo poa sana!

Respect.


FMEs!
 


Iwapo haya kuhusu Rostam ni kweli...huenda ndio sababu alifanya kila awezalo ili JK awe Rais wa Jamhuri akijua kuwa hana "balls" za kumzuia siku ikifika.
 
Sijui yeye Karume analichukuliaje hili la kujificha kitoto ni bora angekuwa wazi awaeleze wenzake wamuelewe msimamo wake, huku kutoa visingizio itakuwa hivyo mpaka lini? Aina ya viongozi tulionao shida tupu!!
 
Sijui yeye Karume analichukuliaje hili la kujificha kitoto ni bora angekuwa wazi awaeleze wenzake wamuelewe msimamo wake, huku kutoa visingizio itakuwa hivyo mpaka lini? Aina ya viongozi tulionao shida tupu!!


Mkuu, Karume hajifichi...ujue kuwa inapokuja kwenye Siasa...Wazanzibari wapo mbali sana kulinganisha na Wabara. Hii ni plan ya Karume ambayo mimi naona inaenda vizuri sana; mpaka sasa ameshamdhalilisha JK na anaonekana Rais dhaifu sana inapokuja maswala ya Muungano.

Angalia historia ya Zanzibar toka enzi hizo, utaona kuanzia viongozi mpaka wapiga kura, wote miaka yote wana balls (msimamo) na hawana wasiwasi; wako tayari kwa lolote. Wameshaona JK ni dhaifu...wameshambana..hatoki.
 

Nimekupata sawia,hopefully kila mmoja yuko kwenye same page.....Kazi ipo.
 

kukacha kikao cha cc ni uhaini??
vyama vingi sasa hivi

muungwana keshaapa piga garagaza muungano hauwezi kumvunjikia mikononi mwake na hawezi ku swallow his pride,
binafsi nampa the benefit of doubt kwamba ataonyesha makucha yake for the first time
 
Mkuu, Karume hajifichi... Wameshaona JK ni dhaifu...wameshambana..hatoki.

JK pia amefail kujenga PR yake zanzibar...ili kuonesha nguvu ya muungano....nyerere hakuwa mjinga alipokuwa akiwapa ruzuku ya umeme......Juzi hapa zanzibar hadi saa mwezi wa tatu huu hawana umeme...JK ameshindwa kutuma msaada unaoeleweka kwenye sehemu ya muungano yenye taabu...hilo limeleta malalamiko kwa wananchi wa kawaida .... wameona kuwa serikali ya muungano haina faida wala msaada kwao.....Jk anapenda visasi ....alidhani kuwa kwa kujiweka mbali na suala la umeme angemkomoa karume ...but worse ni kuwa amedhalilisha uwezo wa serikali ya muungano kama BABA....
 
Any way huu ndio mtikisiko tulikuwa tunasubiri kuelekea uchaguzi
 


Nakubaliana kabisa na uliyoyaandika. Kikao cha kamati kuu kinaweza kuitishwa tena haraka iwezekanavyo ili kujadili maamuzi ya CCM Zenj kuhusiana na Karume kuendelea katika awamu ya tatu na Karume mwenyewe kufanya hila kwa kutohudhuria ili kumkwamisha Kikwete na kamati kuu. Katika kikao hicho ambacho kinaweza kuitishwa tena maamuzi mazito dhidi ya Karume na CCM Zenj yanaweza kuchukuliwa. Je, Karume na CCM Zanzibar watayaheshimu maamuzi hayo na kuyatekeleza? Kama wakiamua kuyadharau maamuzi hayo na kutoyafanyia kazi nini kitafuata? Je, Karume atafukuzwa CCM? Je, Kikwete atatangaza hali ya hatari Zanzibar na hivyo kuviweka Visiwa hivyo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi? Tusubiri tuone kizungumkuti hiki kitakavyoendelea. Wazanzibar wanaelekea wameshaamua liwalo na liwe na kama wakiendelea na msimamo wao bila kuwasikiliza wenzao wa Bara basi Kikwete ana kazi nzito sana katika siku za usoni.
 
1. Kumbe uongozi ni zaidi ya kuuza sura! Haya yanayotokea hapa yanaonyesha jinsi uongozi unavyotaka mtu vigilant. Asiyelala maana anaogopa kuuwawa. Kama tuna machozi basi tujiandae kujililia wenyewe.
2. Wakati tunawalea na kuwafuga "watu wanaoweza kufanya lolote kuvuruga nchi, tulitegemea nini? Tunavuna tunayoyapanda. Dunia hii na mambo yake sio rahisi kama kuweka number kwenye formula ya kutafuta accerelation
 
Nimesikia habari nyepesi toka dar eti usalama wa taifa unaanza kutufatilia JF kwa kuchochea vurugu na upotezaji wa amani ni kweli jamani au??? mwenye data atupe Field Marshall hebu ifatilie mkuu
 
kukacha kikao cha cc ni uhaini??
Vyama vingi sasa hivi

muungwana keshaapa piga garagaza muungano hauwezi kumvunjikia mikononi mwake na hawezi ku swallow his pride,
binafsi nampa the benefit of doubt kwamba ataonyesha makucha yake for the first time


at this point mezani anaonekana kushindwa...labda tuseme atatumia ubabe ...ambao utasababisha umwagaji damu...maana kujiapiza kwa namna hiyo bila kuchukua hatua za kiutawala ...kutalazimu kutumia nguvu za kijeshi ....jambo ambalo wananchi hatuwezi kukubali....ni ndugu sisi ati!!.......

jk akishindwa hili atakuwa ameenda kinyume na kiapo..chake...
 
Nimesikia habari nyepesi toka dar eti usalama wa taifa unaanza kutufatilia JF kwa kuchochea vurugu na upotezaji wa amani ni kweli jamani au??? mwenye data atupe Field Marshall hebu ifatilie mkuu


LOL....
wapi na wapi na usalama wa Taifa au usalama wa wana siasa, waende pia kule zenji kwenye jamvi letu la Mzalendo.net waone amani iaavyoelekea kuvunjika.
 

Jasusi,

Unakumbuka Nyerere alivyomfanyia Jumbe katika "machafuko ya hali ya hewa" ya ZNZ early eighties?

Jumbe alitaka kuleta uhaini wa kuvunja muungano, Nyerere akacheza deal na Hamadi, sekretari wa Jumbe akachukua makabrasha yote, Jumbe akapewa ultimatum kujiuzulu.

Kikwete hana intellect wala courage ya kufanya kitu kama hicho, ambacho anatakiwa kufanya kama kweli anataka kuunusuru muungano huu.

This is nothing new, Kikwete cannot say that this is unprecedented and that he is in uncharted waters.

Personally, nafikiri ipigwe referrendum na muungano ukishindwa kupata simple majority on both sides uvunjwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…