Kikao cha wanaume tu: Ungefanyaje kwenye hali kama hii?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Unaishi mkoani Mara. Mwanamke mmoja ambaye mliwahi kuwa na uhusiano wa muda anakutafuta na anadai kuwa una mtoto naye. Amekuwa akikukamua pesa kila mwezi kwa madai ya matunzo ya mtoto. Huku ukiamini wewe ni baba halali, umekuwa ukitoa msaada kimya kimya.

Lakini, kwa kutaka kuthibitisha ukweli, unaamua kufanya upelelezi binafsi. Unatembelea shule anayosoma huyo mtoto na kugundua kuwa jina la baba katika cheti cha kuzaliwa si lako. Sasa unajiuliza: Je, kweli huyu ni mtoto wangu? Au natapeliwa?

👉 Ungechukua hatua gani ili kujinasua kwenye hali kama hii?

  1. Kumshtaki kwa udanganyifu?
  2. Kuomba vipimo vya DNA kabla ya kuendelea kutoa pesa?
  3. Kukaa kimya na kuendelea kusaidia tu kwa sababu ya mtoto?
  4. Kuwashirikisha wazazi wa pande zote kupata suluhu?

Tupia maoni yako, huenda ukamsaidia mtu mwingine anayepitia hali kama hii. 🧠📢
 
Kwanini utapeliwe kiboya hivyo? Kwamba umeshindwa hata kwenda kumuangalia huyo mtoto ili ujiridhishe?
 
Huyo mwanaume ni mpumbavu ! Unahudumiaje bila kujiridhisha mtoto ni wako ?

Ng'ombe za hivi zinatokaga wapi ?
😀 si unaweza ona mtu analinda hadhi yake au ndo huruma nk
 
Labda binti kaandika jina la baba yake(babu wa mtoto)
Au mbuzi nyingine ambayo nayo inaaminishwa kwamba mtoto ni wake kwa hiyo mwanamke anapokea matunzo double
 
Cheti Cha Kuzaliwa si uthibitisho tosha kuwa mtoto si wako .

Wanawake wahuni sana unaweza kuta mtoto ni wako ila kutokana na umbali mlionao akaamua mtoto huyo awe na wababa wawili kwa sababu za kiuchumi
Wapuuzi sana
 
Kwanini utapeliwe kiboya hivyo? Kwamba umeshindwa hata kwenda kumuangalia huyo mtoto ili ujiridhishe?
hivi kumuangalia tu inatosha? na kwanini mwanamke abadilishe jina kwenye cheti cha kuzaliwa
 
Nimevamia kikao chenu mambwa. 😹

*Endelea kuhudumia inawezekana aliweka jina lisilo lako kwasababu zake binafsi.
Aliona huna muelekeo akaamua kuweka la ukoo wake mama.

*Inawezekana hukumpa ushirikiano toka mwanzo akaamua kumpa mtu wa karibu ambaye ni msaada kwake ila ukweli anaujua mtoto ni wako.
 
Lakini si wanasema vipimo hata ungefanyaje utaambiwa ni wako japo jina sio lako
🧬 DNA ndo ita confirm either ni goli lako au la mtu mwingine, na chamsingi kabisa hapo inavyoonekana kwenye hiyo situation jamaa aliingia kichwa kichwa, kipindi hichi kubambikiziwa damu isiyo yako ni jambo la kawaida wapo watu wengi tena kwenye ndoa zao wanalea watoto ambao siyo damu zao, Cha msingi ni kutafuta pesa ya DNA test ili ujue umepata au umepatikana
 
wadau wanadai kwamba DNA labda ukapimie Kenya ndo itakuwa halisi ukipimia hapa nasikia lab tests zinakuja tu positive ni wako!! sijui kuna ukweli kiasi gani!
 
Ningemwambia mhusika aache utapeli atakuja kukamuliwa visivyokamulika.
 
Unaishi mkoani Mara. Mwanamke mmoja ambaye mliwahi kuwa na uhusiano wa muda anakutafuta na anadai kuwa una mtoto naye. Amekuwa akikukamua pesa kila mwezi kwa madai ya matunzo ya mtoto. Huku ukiamini wewe ni baba halali, umekuwa ukitoa msaada kimya kimya.

Lakini, kwa kutaka kuthibitisha ukweli, unaamua kufanya upelelezi binafsi. Unatembelea shule anayosoma huyo mtoto na kugundua kuwa jina la baba katika cheti cha kuzaliwa si lako. Sasa unajiuliza: Je, kweli huyu ni mtoto wangu? Au natapeliwa?

👉 Ungechukua hatua gani ili kujinasua kwenye hali kama hii?

  1. Kumshtaki kwa udanganyifu?
  2. Kuomba vipimo vya DNA kabla ya kuendelea kutoa pesa?
  3. Kukaa kimya na kuendelea kusaidia tu kwa sababu ya mtoto?
  4. Kuwashirikisha wazazi wa pande zote kupata suluhu?

Tupia maoni yako, huenda ukamsaidia mtu mwingine anayepitia hali kama hii. 🧠📢
Huu ujinga mnajifunzia wapi?
 
wadau wanadai kwamba DNA labda ukapimie Kenya ndo itakuwa halisi ukipimia hapa nasikia lab tests zinakuja tu positive ni wako!! sijui kuna ukweli kiasi gani!
Hamna, wengi tu nawafahamu walienda kupima DNA wakakuta watoto waliokuwa wanawalea sio wao
 
Back
Top Bottom