Weka hisia pembeni!
Tunajadiliana kutaka kujua ni sababu au vigezo vipi vinavyomfanya nyerere aitwe baba wa Taifa.
Je,una sababu zozote (ukiachilia zilizotajwa) za kumuita nyerere baba wa Taifa?
AWE PONDA? Mimi nashangaa kikao kipi kiliwapa waislam idhini ya kuchinja? Au imeandikwa kwenye katiba ya wapi wachinje
Hakuna cha wivu hapa! Kikubwa ni kuwa wakristo mmeshindwa kuleta noja za msingi za kuutetea huo ubaba wa taifawa mchonga. Bado sijaona hoja za msingi za kumwita Nyerere kuwa baba wa taifa.
Naam, ndiyo sababu hata wewe ukiiona ndogo! sababu ndogo tu yaweza kuzua jambo kuu! unataka rejeo gani zaidi. taifa hili lilipata uhuru akiwa kiongozi mkuu kama baba! Lugha hukua na watu. pale wanapomheshimu humpa mtu jina zuri kwenye upungufu jina haliwi zuri. mfano wakati fulani walimwitaa Nyerere mchonga meno wakati huo hali ya maisha ilikuwa mbaya na yeye alikuwa mtawala. sijui wewe unataka mjadala ili asiitwe baba wa taifa! kwa sasa hilo haliwezekani hadi historia yake itakapoelezwa vinginevyo na watu wajue hivo wakatae. kupinda ukweli huu ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. bora kuleta mjadala tofauti
Weka hisia pembeni!
Tunajadiliana kutaka kujua ni sababu au vigezo vipi vinavyomfanya nyerere aitwe baba wa Taifa.
Je,una sababu zozote (ukiachilia zilizotajwa) za kumuita nyerere baba wa Taifa?
ukishajua itakusaidia nini?
nadhani umejibu taifa gani mwenyewe. jina si hoja labda unataka tujadili logic. pemgine unataka tuseme tanganyika, na zanzibar itoke hapo lakini tulikuwa na watanganyika na wazanzibar ambao ulifika wakati wakaitwa watanzania. sasa inakuwa vigumu kusema watanzania ni wazanzibar au ni watanganyika lakini kwa muungano ule watanganyika ni watanzania na wazanzibar ni watanzania pia. kwa hiyo tunapofikiria baba wa taifa tuna maana ya taifa la tanzania. ikiwa hakuna tanzania basi itabidi tuanzie mwanzo. hapo tunaweza kuwa na baba wa taifa la zanzibar na baba wa taifa la tanganyika. kwa kuwa zanzibar ina serikali, bendera na alama nyingine inaweza kuwa na baba kwa mtindo watakaoamua na kikao watakachokaa kupitisha hilo.Baba wa taifa gani?kama ni tanzani lini ilipata uhuru?
Kwa hiyo ni baba wa Taifa la Tanganyika (sijui kama hii nchi bado ipo)! maanake ukiitaja Tanzania tu utakuwa umeshaiingiza Zanzibar ambayo ilikuwa na rais wake hivyo kumfanya nyerere si muasisi pekee.
Hoja ya kuwa rais wa kwanza wa JMT imeshajadiliwa! peruzi huu uzi vizuri.
Na Karume naye hakuwaunganisha Watanzania bila kujali tofauti zao kiuchumi,kidini,kielimu na kikabila?kama unahitaji vigezo zaidi ni kwamba Mwalimu Nyerere aliweza kuwaunganisha watanzania bila kujali tofauti zao kiuchumi,kidini,kielimu na kikabila.hilo nalo linamfanya apewe heshima ya Baba wa Taifa!
hilo la mataifa mawili ni sawa.pengine ingefaa tuweke pembeni hiitafsiri ya lugha. neno baba likiwa na maana ya denotative ni mtu mzima mwanamume mwenye watoto/mtoto naye ataitwa tu baba na hao watoto. connotative meaning ya neno baba inaenda mballi ambapo hata baba au mama huweza kumwita mwanae baba. katika sehemu za kazi kama shule nk.kiongozi mkuu wa mahali huweza kuitwa baba kama ni mwanamume na mama kama ni mwanamke. neno baba hapa hutumika kama heshima tu na zaidi kuhusiana na hali ya baba kuwa mlezi, mlinzi wa familia. kwa hiyo baba wa taifa ni connotative zaidi ya denotative. hivo ndivo lugha ilivo. basi ikiwa kama kuna watu hawataki kumwita Nyerere baba wa taifa wana haki maana si sheria ndo maana haikupitishwa rasmi katika kikao. wengine humwita hivo wengine mwalimu. sioni kama kuna haja ya kujadili hili kwani si sera, si sheria ni hiari ya mtu tu. mambo ya kanisa hayana haja ya kutajwa katika hili. kama unapata kinyaa kumwita baba wa taifa acha!funguka zaidi!
Kwanza kuna mataifa mawili tofauti ndani ya Tanzania! hivyo utakuwa unamaanisha Tanganyika nchi ambayo mnaiua kimyakimya kama haijakufa kabisa.
Pili, je kiongozi mkuu huitwa baba? au ni mambo ya Kanisani mnayotaka kutuingiza wote?
Vizuri sasa umebakia ubaba wa Tanganyika!kwa hiyo tunapofikiria baba wa taifa tuna maana ya taifa la tanzania. ikiwa hakuna tanzania basi itabidi tuanzie mwanzo. hapo tunaweza kuwa na baba wa taifa la zanzibar na baba wa taifa la tanganyika. kwa kuwa zanzibar ina serikali, bendera na alama nyingine inaweza kuwa na baba kwa mtindo watakaoamua na kikao watakachokaa kupitisha hilo.
Karume anastahili kuitwa baba kwa upande wa Zanzibar kwa Tanzania yeye mwenyewe alimpa nafasi nyerere awe rais. ikiwa twatumia neno baba ni vigumu kusema Karume ni baba wa tanzania wababa wawlili inakuwaje? karume akiitwa baba kule zanzibar ni vema hata wabara watapaswa waheshimu hilo kwa vile aliandika historia ya zanzibar. angekuwa rais wa tanzania basi yeye ndiye andestahili kuitwa baba wa taifa la tanzania kwamaana hii.Na Karume naye hakuwaunganisha Watanzania bila kujali tofauti zao kiuchumi,kidini,kielimu na kikabila?
Mbona naye hamumuiti baba wa Taifa?
wanachi ndio wenye uamuzi. nyerere alikuwa anataka utanzania na asingeweza akautaka utanzania na akautetea utanganyika wakati huohuo. kwa vile sisi ndio tatakaoukataa utanzania ndio haohao tutakaoona kama tunaweza kumwita baba wa tanganyika au hapana.Vizuri sasa umebakia ubaba wa Tanganyika!
Unafikiri Watanganyika watamuita vipi nyerere baba wa Taifa la Tanganyika wakati alikuwa akifanya kila aina ya juhudi ili aifute Tanganyika?
Na Karume naye hakuwaunganisha Watanzania bila kujali tofauti zao kiuchumi,kidini,kielimu na kikabila?
Mbona naye hamumuiti baba wa Taifa?
jamii gani?Itasaidia jamii kujua kama kanisa lilipewa kipaumbele ili lije kutawala milele tanzania.