Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

Swali:Je hatujawahi kuwa na 'mama wa taifa'?

Na kama 'mama wa taifa yupo/walikuwepo,anaitwa/wanaitwa nani? kina nani ni 'watoto wa taifa'?

Kanisa lina taratibu na vigezo vyake katika kuwatangaza watakatifu.Hakuna siasa kule bali ni roho mtakatifu huongoza libeneke zima.

Si kila jambo linahitaji kikao.

Kwani wewe ulimuita babako 'baba' au mamako 'mama' baada ya kikao na wewe kuafiki hivyo?

Nyerere ni baba wa Taifa.Itabaki hivyo siku zote.

Mkapa hawezi kuwa hata shemeji/mjomba wa taifa-Never!!!!

Jibu zuri sana! Haa haaa haaaa haaaa hapo kwa mkapa umeniacha hoi!kwii kwiii kwiii kwiii kwi kwi.
 
Kwa hiyo ni baba wa Taifa la Tanganyika (sijui kama hii nchi bado ipo)! maanake ukiitaja Tanzania tu utakuwa umeshaiingiza Zanzibar ambayo ilikuwa na rais wake hivyo kumfanya nyerere si muasisi pekee.

Hoja ya kuwa rais wa kwanza wa JMT imeshajadiliwa! peruzi huu uzi vizuri.
Sideeq, kumbuka kuwa wavumao baharini ni papa kumbe na wengine wamo. bas katika kundi kubwa la watu lazima atangulie/atangulizwe mmoja huyo ataitwa kiongozi atapewa hata sifa anbazo pengine asingestahili kama angekuwa mtu wa kawaida. hata aweza kulaumiwa kwa jambo alilotenda wa chini yake. basi hi heshima alipewa kwa sababu alikuwa mbele. ni bahati kuwa mbele na ni haki kupata kile aliyepo mbele hustahili. nyerere aliitwa baba wa taifa kwa sababu alikuwa mbele/kiongozi hii haina maana kuwa angekaa mwingine hiyo nafasi yake huyo mtu asingeitwa baba wa taifa. hiyo si nafasi ya nyerere kama mtu aitwae hivo bali kama kiongozi aliyetangulia wengine wote. zaidi watu waliona alistahili kwani walimpimama kwa uadilifu, kazi na uaminifu na kwapenda watu wake kama baba. ni watu walipima hivo. yeyote anayeona watu walikosea anaweza kuja na hoja ya kupinga mawazo hayo na kuonyesha jisnsi nyerere asivyostahili ubaba wa taifa. ajenge hoja zake objectively si kwa ushabiki wa siasa au dini au rangi bali kwa vigezo vinavyopimika
 
Hakuna cha wivu hapa! Kikubwa ni kuwa wakristo mmeshindwa kuleta noja za msingi za kuutetea huo ubaba wa taifawa mchonga. Bado sijaona hoja za msingi za kumwita Nyerere kuwa baba wa taifa.

Heeeh! kumbe hoja ni ukristo vs uislam? sio ubaba wa taifa tena?.

Nyie watu kweli akili zenu zimefubaa yani kila kitu lazma mkitazame kwa macho ya dini.
 
Ni kile kikao kilichomchagua kuwa Rais wa TANU na kumpitishha kuwa mgombea wa Urais kuelekea Uhuru na hivyo kumfanya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Tanzania. Ukimsoma Kambona anamuita Baba wa Taifa na wazee wengi na wananchi wa miaka ya mwanzo wa Uhuru walimtambua hivyo. HIli la kuwa ni "Baba wa Taifa' halikuja baada ya kufa au kutoka kwenye urais kama wengine wanavyoamini; lilikuwepo tangu mara baada ya Uhuru alitambulika hivyo.
 
angekuwa rais wa tanzania basi yeye ndiye andestahili kuitwa baba wa taifa la tanzania kwamaana hii.
Tutamwita vipi mtu baba wa Taifa kwa ajili ya kuwa rais wa kwanza wa nchi mbili alizoziunganisha bila ya ridhaa au kushirikisha wananchi? ...hii haikubaliki.
 
Ni kile kikao kilichomchagua kuwa Rais wa TANU na kumpitishha kuwa mgombea wa Urais kuelekea Uhuru na hivyo kumfanya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Tanzania. Ukimsoma Kambona anamuita Baba wa Taifa na wazee wengi na wananchi wa miaka ya mwanzo wa Uhuru walimtambua hivyo. HIli la kuwa ni "Baba wa Taifa' halikuja baada ya kufa au kutoka kwenye urais kama wengine wanavyoamini; lilikuwepo tangu mara baada ya Uhuru alitambulika hivyo.
...ndio baada ya uhuru zikatolewa nembo zenye kuonyesha picha ya Yesu na Maria!

Kumaanisha kuwa Uhuru wa nchi hii uliletwa na Yesu, taifa likatafutiwa baba kama vile Wakristo walivyo na baba askofu!
 
Udini uliopo nchini umeasisiwa na nyerere (hili limeshajadiliwa sana hapa)Ni sehemu gani ya Tanganyika ambayo nyerere aliikuta katika ubaguzi wa kikabila na kuufuta?

Kusema kuwa nyerere amefuta ubaguzi wa kikabila,ameleta amani Tanganyika ni kuwadharau na kuwakejeli mababu zetu ambao walikuwa wakiishi bila ya vita na ubaguzi wa kikabila kabla hata wahamiaji kama wazazi wa nyerere hawajahamia katika nchi hii.Orodha ya ufisadi wakati wa nyerere ni ndefu! unazitaja Epa,richmond n.k kutokana na Dunia ya leo (ya uwazi),lakini yote haya yalifanyika wakati wa nyerere...inakutosha tu kuwa mafisadi tulio nao ni product ya nyerere.

...Kwa mara nyingine tena tunaona hoja za nyerere kuwa baba wa Taifa zikifeli!
kaka jibu ni kwamba,ulevi wa dini umekuelemea ebu kalale kidogo!
 
Kuna ulevi wa aina nyingi, kuna ulevi wa pombe, madawa ya kulevya na bangi. Lakini hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa dini. Mtoa mada umelewa udini. Jaribu kumpuzika kwa muda huenda ukapungua na si kuondoka.
 
Hakuna cha wivu hapa! Kikubwa ni kuwa wakristo mmeshindwa kuleta noja za msingi za kuutetea huo ubaba wa taifawa mchonga. Bado sijaona hoja za msingi za kumwita Nyerere kuwa baba wa taifa.

mwanzo nilifikiri una hoja ya msingi kujadili kuhusu u-baba wa taifa Mwl. JK Nyerere,kilichonishtusha ni kubaini hoja iko kidini zaidi,Nyerere ata mbatize leo mmuite mbweha wa taifa haathiriki na chochote,ita jina unaloona ukimuita wewe roho yako itaswafika.
 
Nina swali kwa mleta uzi huu.ukilijibu basi na wewe utakuwa umejijibu mwenyewe.HIVI NI KIKAO GANI KILIAMUA BABA YAKO AITWE BABA YAKO?
 
Mwalimu Nyerere kama Rais wa kwanza wa Tanganyika alikabidhiwa nchi na mkolon mwingereza mwaka 1961 ,nchi ikiwa ya 1 kwa uzalishaj na uzaji wa katan dunian.pia nchi maarufu kwa uzalishaji na uzaji wa kahawa,korosho na raslimal nying sana .Lakini mwaka 1985 kaacha nchi hohehahe,miongon mwa nchi maskin zaid dunian,pia nchi inayotegemea misaada kuliko nchi nyingine,huduma za kijamii zikiwa duni sana.
 
Mods iondoeni hii ipeleke kule kwenye mjadala wa uchochezi wa Mohamed Said,

Huko ndiko mijadala kama hii inastahili!
 
Mods iondoeni hii ipeleke kule kwenye mjadala wa uchochezi wa Mohamed Said,

Huko ndiko mijadala kama hii inastahili!

Acha ushamba wewe! Kama hupendezwi na tathmini yake pita tu, Uchochezi kutoa maoni yake? Hata wewe ukileta comments zako kuhusu Jk wapo wataosema Uchochezi hapa ni sehemu watu wanapata fursa ya kusema wanachokiamini kama hukubaliani nacho jenga hoja sio kuomba mods wafute au wahamishe.Kaanzishe jukwaa lako la kujadili unachokipenda penda yako. Ukikereka akijadiliwa Nyerere jua pia wapo wanaokereka akijadiliwa Mwinyi,Mkapa au Kikwete.Ungejifunza Lesson ya kuanguka Ukuta wa Berlin 1989 usingekuwa Block mind kwa Namna unavoonekana, Mwl Nyerere mwenyewe anakiri hakuongoza serikali ya Malaika na anasema yapo makosa waliyofanya na hajawahi kukutazeni msiyazungumze, anakosolewa liwe funzo kwa wengine kwa mabaya yake kama vile tunavomkumbuka kwa Mazuri yake watu waige!
 
Mwalimu Nyerere kama Rais wa kwanza wa Tanganyika alikabidhiwa nchi na mkolon mwingereza mwaka 1961 ,nchi ikiwa ya 1 kwa uzalishaj na uzaji wa katan dunian.pia nchi maarufu kwa uzalishaji na uzaji wa kahawa,korosho na raslimal nying sana .Lakini mwaka 1985 kaacha nchi hohehahe,miongon mwa nchi maskin zaid dunian,pia nchi inayotegemea misaada kuliko nchi nyingine,huduma za kijamii zikiwa duni sana.

Mkuu
Ulichoandika hapa ni tofauti na kichwa cha habari.

Labda tukuulize unafahamu sifa za kiongozi wa taifa kuitwa baba wa taifa?

a) Kama jibu ni ndiyo zitaje, kisha fafanua kwanini?

b) kama jibu ni hapana, kwanini umeiweka hii hoja hapa na hujui unachokiwakilisha.
 
maswali mazuri haya tunasubiri majibu!
 
Back
Top Bottom