Kikatiba, Waziri Mkuu ndiye Msimamizi wa Mawaziri wote. Sasa Lukuvi na Kabudi watasimamia Mawaziri vipi?

Yawezekana Lukuvi akaja kuwa Waziri Mkuu. Nawaza tu kwa sauti
 
Lukuvi atakuwa kama Mshauri Mkuu wa Mh. Rais kuhusu mambo yote ya uongozi kwa ujumla navyoona mimi, kitu ambacho ni kizuri sana sanaaa..
...Vipi kuhusu ubunge wake?...baraza la mawaziri halitoshi kumshauri?....hivyo vyeo havipo kikatiba, Sasa wakistaafu na hivyo vyeo vipya watapewa pension?
 
Tanzania mzima inajua kuwa mama amebugi kuwaondoa akina lukuvi, ushauri WA wazee ndiyo umefanya warudishwe
 
Hawana potential wowote. Ile statement ya "hagombei uspika"ni alarm tosha kuwa ni kifungo cha kisiasa flani hivi. Jiulize, je Rais kaambiwa na Lukuvi kuwa hagombei?
 
Tanzania mzima inajua kuwa mama amebugi kuwaondoa akina lukuvi, ushauri WA wazee ndiyo umefanya warudishwe
Hakuna mtu muhimu mbele ya anayechezea taasisi ya Urais. Ataondolewa tu. Alichofanya bi Tozo ni kuwapiga pini. Anawatoa kwenye siasa anawaingiza kwenye utaalam huku wakiwa washazeeka
 
... hatoki kirahisi Mkuu! Ni process fulani ndefu tofauti na mawaziri wa kawaida ambao taarifa za kuondolewa kwao wanaweza kuzipatia bar. Pengine ndio maana mama hakutaka maprocess marefu kaamua atumie shortcut fulani hivi.
Hivi kazi ya wabunge ni nini?!?

Kabudi na lukuvi wanaenda ikulu kumshauri mini tens rais..
Ssh kachemka. Na lugha rahisi ni kuwa ikulu kuna marais watatu kwass.
 
Hoja yangu imejikita kwenye kile ambacho Rais Samia amekisema kuwa, hao kina Kabudi na Lukuvi atawapa jukumu la kumsaidia kuwasimama (akasema kuwachapa viboko!) mawaziri wake. Kwa lugha ya malkia hao jamaa wanakwenda kuwa overseers wa baraza lake la mawaziri.

Rais hajasema anawateua kuwa washauri wake bali anawateua kuwa wasimamizi na watendaji rasmi wa kiserikali nje ya katiba!
 
Zanzibar-ASP mtuambie nyie wazenji labda mnamuelewa mzenji mwenzenu.
Hata sisi wazenji bado hatumuelewi huyu mama, kwa kuwa hata yeye hajielewi.

Juzi alisema anafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ili kuwaondoa wote wataka urais wa 2025 ili wakapiganie vyema huo urais huko nje ya serikali yake na kumuacha yeye akifanya kazi za kiserikali, leo anasema wale wataka urais aliowafukuza anawaleta ikulu ili kumsaidia kuendesha serikali yake!

Nani anaweza kukuelewa?
 
Mimi siwez kujadili kwanini wamepewa kazi maalum,
mpaka nijue kwanini alitamka atawatoa waliokuwa kwenye
kinyang'anyoro cha 2025 wakajipange vizuri.
Danganya toto.
 

Changamoto.
 
Haswaa, wewe ndio umeelewa mada hapa. Na ndio msingi wa hii hoja.
 
Rais anawapeleka wabunge kuwafungia Ikulu inaruhusiwa?

Anasema atawapa kazi huko za kusaidia saidia kusimamia mawaziri wakati hawa ni wabunge wanaotakiwa wakawatetee wananchi wao majimboni.

Hapa mimi sijaelewa mama ana mpango gani na maamuzi hayo.

Wakikubali wataenda kuwa waosha vyombo ikulu.

Wakatae ulaghai huu haraka kulinda heshima zao.

Wakawatetee wananchi waliowachagua. Waachane na hizi laghai za wajanja wa mjini wanaomshauri mama mambo ya janja janja.
 

Atakuaje mshauri wakati yeye Lukuvi na Kabudi ndio aliwataja kuwa threat wake 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…