Kikosi cha Brazil kitakachoelekea Urusi 2018 Kombe la Dunia

Kikosi cha Brazil kitakachoelekea Urusi 2018 Kombe la Dunia

!
!
Zamani Kikosi Kilikuwa Kinajaa Watu Wa Luigi Yao. Naona Siku Hizi Wamejaa Wachezaji Wa Ulaya Tu, Wa Ligi Ya Kwao Mmoja Tu.
Mwaka 2010 miezi kama hii wakati Brazil wanajiandaa kwenda kushiriki WC kule bondeni kwa madiba aliyekuwa striker wao tegemezi wa wakati huo Luis Fabiano aliliongelea kuhusu hili.

Aliulizwa na mwandishi wa habari ni kwanini kikosi cha Brazil siku hizi kinajaa sana wachezaji wanaocheza ligi za ulaya tofauti na miaka nyuma!?

Alichokisema ni kwamba, baada ya Brazil kuchukua ubingwa 1970 walikaa miaka 24 ndio wakaja kuchukua tena ubingwa ambapo ilikuwa ni 1994. Na katika muda wote huo wa miaka 24 walikuwa wanapeleka wachezaji wengi wanaocheza ligi ya ndani(Brazilian football league) na walikuwa wanapiga kandanda safi haswa, yaani walikuwa wanapiga lile samba lenyewe lenye ufundi mwingi hata barcelona wanasubiri.

Lakini cha ajabu pamoja na kucheza mpira mzuri uliowavutia wapenzi wengi wa mpira, walikuwa hawafiki mbali kwenye michuano, walikuwa wananyanyaswa sana na timu za ulaya. Na hii ni baada ya wao kutesa sana miaka 1970 huko ndio timu za ulaya zikaja na mbinu ya kuwadhibiti.

Baada ya wao kuteswa sana na timu za ulaya ndio mmoja wa magwiji wao anayeitwa Mario Zagalo akatoa wazo la kubadirisha mfumo mzima wa uchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, hatua moja wapo ilikuwa ni kuchagua wachezaji wengi watakao copy na soka la ulaya. Na kweli walivyofanya hivyo kwa mara ya kwanza walifika fainali mara tatu mfululizo 1994,1998 na 2002 kwa vikosi vilivyokuwa vinasheeni wachezaji wanaotoka ulaya.

Wabrazil hawakupenda kabisa timu yao ilivyokuwa inacheza lakini walikuwa wananyamazishwa na ubingwa.

Brazili ya miaka ya nyuma ilikuwa inapiga kandanda safi lakini ilikuwa haina tofauti na Arsenal mpira mwingi alafu magoli hakuna ndio maana wakabadilika now days wanaocheza kiulaya ulaya tu.
 
Back
Top Bottom