Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Naam...Baada kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya Tanzania TPL, 20 18/2019 na klabu ya Simba SC kutawazwa kuwa Mabingwa wa Tanzania kwa mara ya pili mfululizo, hatimaye ile safari ya kwenda Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya kwa ajili ya mashindano ligi kuu na michuano ya Kimataifa sasa ipo tayari.
Kikosi cha Klabu ya Simba SC, Mnyama Unyamani, leo Julai 15, 2019 kimeondoka kwa safari ya kwenda Afrika Kusini ambapo kitakuwepo huko kufanya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Pre-Season.
Nyota wote wa Simba SC Ijumaa walikusanyika kwenye kambi ya timu hiyo Hotel ya Sea Scape iliyopo kando ya bahari ya Hindi jijini Dar es salaam na kupewa semina maalum Jumapili kabla ya leo Jumatatu kukwea MWEWE kwenda Afrika Kusini.
Simba SC, wakiwa nchini Afrika Kusini wanatarajia kucheza michezo ya kirafiki na baada hapo kikosi hicho kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 5, 2019 ikiwa siku tatu kabla ya maadhimisho ya Simba Day Agosti 8.