Kikosi cha Simba SC kimeondoka kwenda Afrika Kusini kujiandaa na Msimu Mpya 2019/2020

Kikosi cha Simba SC kimeondoka kwenda Afrika Kusini kujiandaa na Msimu Mpya 2019/2020

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Naam...Baada kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya Tanzania TPL, 20 18/2019 na klabu ya Simba SC kutawazwa kuwa Mabingwa wa Tanzania kwa mara ya pili mfululizo, hatimaye ile safari ya kwenda Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya kwa ajili ya mashindano ligi kuu na michuano ya Kimataifa sasa ipo tayari.

Kikosi cha Klabu ya Simba SC, Mnyama Unyamani, leo Julai 15, 2019 kimeondoka kwa safari ya kwenda Afrika Kusini ambapo kitakuwepo huko kufanya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Pre-Season.

Nyota wote wa Simba SC Ijumaa walikusanyika kwenye kambi ya timu hiyo Hotel ya Sea Scape iliyopo kando ya bahari ya Hindi jijini Dar es salaam na kupewa semina maalum Jumapili kabla ya leo Jumatatu kukwea MWEWE kwenda Afrika Kusini.

Simba SC, wakiwa nchini Afrika Kusini wanatarajia kucheza michezo ya kirafiki na baada hapo kikosi hicho kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 5, 2019 ikiwa siku tatu kabla ya maadhimisho ya Simba Day Agosti 8.

FB_IMG_1563172146710.jpeg
FB_IMG_1563176606167.jpeg
FB_IMG_1563176660466.jpeg
 
Ligi ianze tu, tuone udambwi wa Chama Shiboub na Kahata, ukiachilia mbali Mr Assist Ajibu na huku Grason Fraga akiruka vichwa kama vyooote

Safari hii watatafutana mno watani zetu aisee..!

ThisIsSimba
 
Na hiyo safari ya ndege wameiunga atcl au nao sehemu ya kuhujumu shirika.
 
Mnaenda jiandaa kupigwa 5 mèchi za kimataifa
Tunajiandaa kucheza nusu fainali au fainali CCL, ligi ya TPL hatuhangaiki nayo kwa vile hatuna mpinzani..We endelea kulima shamba huko Moro [emoji23]
 
Tunajiandaa kucheza nusu fainali au fainali CCL, ligi ya TPL hatuhangaiki nayo kwa vile hatuna mpinzani..We endelea kulima shamba huko Moro [emoji23]
Nusu faiʼnali kwa wačhezaji gani au wale wauza matikitì mliowaokota brazil n india?
 
Back
Top Bottom