SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Nimewahi kusema hata wachezaji tunaowaleta kucheza ligi yetu, tukitambua wale wazuri sana halafu hawana rekodi za kuchezea timu za taifa huko watokako, tuwape uraia chap kwa haraka.Sio una wasiwasi bali ni kweli hao wanaocheza ligi za nje ya Africa ukimuacha Samatta na Dismas wana uraia wa nchi nyingine lakini wana uwezo wa kuchezea timu ya taifa bila shida maana inaruhusiwa kwenye mpira...
Mimi sina shida na kuwapa uraia wachezaji wenye asili ya Tanzania walioko huko nje, swali langu la msingi, wamekana uraia wao wa huko nje kama matakwa ya sheria zetu za uhamiaji zinavyotaka?
Kama tumeamua kufumba macho, kwa nini sasa tusibadili sheria za uhamiaji kama tumeona suala la uraia pacha lina faida. TFF hawana mamlaka ya kuvunja sheria za nchi.