Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Si=ubiri uone hata kama hiyo hoja itapata nafasi kuwasilishwa. Hizo nyumba zimeshakwenda, tusahau
 
Kwa kifupi tukizungumzia kurudisha nyumba za Serikali walizizouziana kwa bei ya kutupa maana yake halisi ni kuin'yang'anya CCM serikali na kuingiza wapinzani ndipo tutaongelea na kurudisha nyumba za serikali tulizoporwa, Leo hii wale wale waliopitisha Bungeni mswaada wa kuuziana Nyumba zetu yaani CCM wanajaribu kutuaminisha kuwa yale makosa yalitendwa kwa bahati mbaya tu na hakukuwa na malengo fulani

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Sendeka: Nyumba za serikali zirejeshwe [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Saturday, 11 February 2012 09:49 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Midraji Ibrahim, Dodoma
MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), amesema kati ya uamuzi wa makosa uliowahi kuchukuliwa na Serikali ya chama chake cha CCM, ni kuuza nyumba za umma hivyo akataka zirejeshwe Serikalini mara moja vinginevyo atawasilisha hoja binafsi Bungeni.

Hii sio mara ya kwanza kwa wabunge kuhoji kuuzwa kwa nyumba za serikali wakitishia kutoa hoja binafsi bungeni kutaka mchakato huo ukome.

Aprili 5 mwaka 2008 aliyekuwa mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alitishia kutoa hoja binafsi bungeni kutaka watu ambao si wafanyakazi wa serikali ambao wameuziwa nyumba za serikali wanyang'anywe nyumba hizo.

“Nataraji kuja na hoja ya kulitaka Bunge liamuru nyumba hizo zirudishwe… napingana na Waziri (John) Magufuli aliposema waliovunja mkataba wamenyang’anywa nyumba, siyo kweli,” alisema Sendeka na kuongeza:

“Nina ushahidi hata wale waliopata kwa sababu ya undugu wa waliokuwa na madaraka bado hawajarejesha.”





Historia ya nyumba za serikali

Nyumba za watumishi wa serikali zilianza kujengwa na watawala wa Kijerumani na Waingereza. nyumba hizo ambazo sasa idadi yake inakadiriwa kufikia 10,000 ziko za daraja la tatu, pili na kwanza kulingana na nyadhifa za watumishi wa serikali.............



Sababu za kuuza nyumba hizo hazikuwekwa bayana. Wakati maelezo mengine yanasema kuwa hatua hiyo imefikiwa kuwasaidia watumishi wa serikali kuwa na nyumba, mengine yanasema nyumba hizo ziliuzwa kwa kuwa ni mzigo kwa serikali. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]


2006 Tulidanganywa hivihivi na naamini 2015 CCM watakuja na uongo..eti watarudisha nyumba za Serikali wakati wameishia ahadi na sasa tunaona Madaktari wanavyovutana na Serikali ili wapatiwe nyumba


[TABLE="class: Panel	ViewArticlePanel"]
[TR]
[TD="class: Heading, colspan: 2"]Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwa[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Details"]By Habari Tanzania | Published 10/3/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
​


na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali yake imefikia uamuzi wa kuzirejesha baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wa umma baada ya kubaini kwamba zilijengwa katika mazingira nyeti.

Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao chini ya kivuli cha utaratibu aliojipangia wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi.

“Hatukusudii kuzichukua nyumba zote…kwa mfano kuna OCD kauziwa nyumba ya OCD iliyo katika eneo la polisi, na yule OCD aliyeuziwa kahamishwa kutoka Mtwara kwenda Mafia…au kastaafu na nyumba kapangisha…Kwa kweli kuna maeneo ambayo lazima tufanye marekebisho,” alisema Kikwete.

Ingawa hakufafanua iwapo uhakiki wa nyumba zitakazorejeshwa umeshafanyika au la, na wakati hasa utakapoanza utekelezwaji wa kazi hiyo, kauli yake hiyo imehitimisha minong’ono na malumbano ambayo yamekuwapo kwa muda sasa, kuhusu suala hilo.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, John Kijazi, alikaririwa na vyombo kadhaa vya habari (si Tanzania Daima) akikanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la kila Jumapili siku kadhaa zilizopita kuhusu kuwapo kwa mpango wa serikali wa kuzirejesha nyumba hizo ambazo uuzwaji wake uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu ulizusha manung’uniko makubwa.....................

Najaribu kufikiri je Maneno matupu huvunja mfupa?




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]




 
Nyumba zile za serikali maintenance costs zilikuwa kubwa sana ndiyo maana zikauzwa. Utakuwa maintenance cost ya nyumba hasa hizo za waheshimiwa bei zake zilikuwa inflated mpaka balaa halafu vitu vinavyowekwa ni vya lowest quality.

Hata ingekuwa nini siyo sote ambao tungeweza kupata hizo nyumba. Zingeuzwa kwa tenda wangenunua wahindi basi - akina Manji, Dewji na wengine ambao wana haki ya kuishi mjini.

Nyumba nyengine zilikuwa hoi waliouziwa hayo magofu wamevunja na kujenga nyumba nyengine za maana sasa utairudisha vipi?
 
Vyovyote iwavyo, mi naona Sendeka anapoteza muda kwa sababu maazimio ya bunge hudharauliwa na serikali
 
makosa yalishafanyika,ni wakati wa kumwadabisha magufuli,sasa hivi kaja na staili ya kuchafua mabango ya watu na wino mwekundu,kwani yanapunguza nini,huyu ni mgonjwa wa akili na tunamwendekeza,mtakuja kushtukia anatangaza kubomoa ikulu iko karibu na bahari,he is mad
 
Si=ubiri uone hata kama hiyo hoja itapata nafasi kuwasilishwa. Hizo nyumba zimeshakwenda, tusahau
When the political capital is right, nyumba hizo zitarudi tu, tupende tusipende.
Watu mna memory ndogo sana mnasahau kuwa mtaji wa karibu nyumba zote za Msajili wa Majumba(sasa NHC) ZILTAIFISHWA na serikali ta Tanzania.
Wenyewe wapo bado wanaishi.
Waliouziwa nyumba za serikali waziendeleze tu ili baadaye ziwe mali ya umma tena.
 

..vipi ....stail yako inaonekana imekutashi ..aidha una nyumba ..,oysterbay au una kampuni ya ubongo...
 
Tatizo nyumba ziliuzwa kama nyumba wakasahau value za kiwanja, pia hakuangalia location zilizokuwapo. Haiwezekani utoe sababu ya gharama za matengenezo kubwa eti uuze nyumba, zikowapi walizojenga? Lazima zirudi walijenga mpya watakula hasara.
 
  1. Maintenance cost haikuwa kubwa ila wizi mkubwa ulikuwa unafanywa na watumishi wa serikali na wakandarasi.
  2. Viongozi waliokuwepo hawakuwa na uhakika wa kurejea madarakani hivyo wakatumia nafasi zao kujimilikisha maeneo nyeti ya umma.
  3. Serikali ilipaswa kutengeneza mkakati maalum wa kutengeneza nyumba hizo au kujenga mpya kama vile ilivyoanzisha bima ya afya ili kugharimia matibabu ya watumishi wake.
 
Huwezi kulinganisha gharama za maintenance ya nyumba katika tropical area na gharama za kuwaweka mawaziri hotelini miezi nenda miezi rudi kwa ukosefu wa nyumba. Nyumba za kitropic ukishapiga rangi tu na kubadilisha madirisha inadumu kwa zaidi ya miaka 10 bila kuhitaji another maintenance. Njoo na kisingizio kingine. Hata kama nyumba zilikuwa hoi serikali ingeweza kujenga nyumba mpya katika kiwanja hicho hicho. Mbona serikali hiyo hiyo ilitangaza kuwa inajenga nyumba mpya za wafanyikazi wake? H izo hela ilizitoa wapi. Kajipange upya Bibi kijakazi.
 
Tatizo nyumba ziliuzwa kama nyumba wakasahau value za kiwanja, pia hakuangalia location zilizokuwapo. Haiwezekani utoe sababu ya gharama za matengenezo kubwa eti uuze nyumba, zikowapi walizojenga? Lazima zirudi walijenga mpya watakula hasara.

Kwani value ya viwanja vya serikali inakuwa ni bei gani? Mbona watu wa ardhi wanajichukulia vingi vingi halafu wanaviuza kwa bei kubwa kabisa? Mfano Mbezi beach, Kigamboni mpya na kadhalika.

Kwenye system yo yote ile kuna wanaofaidika na wale wanaokula hasara hiyo haipukiki.
 
Warudishe, ila pia tuwalipe fidia wale walizikarabati vizuri. Kasheshe ni wale waliojenga nyumba mbili au tatu kwenye kitalu kimoja baada ya kuuziwa
 
Tunahitaji rais ambaye anaweza kuwa na uthubutu wa kutimiza hilo jukumu la kurudisha nyumba za walala hoi nafikiri katika wagombea wetu wa 2015 lazima tuwaandalie DO LIST na hilo jukumu liwemo hatuhitaji tena SERA kwani nimegundua ni sanaa tupu.
 

Binti, hiyo red ina muda wake na huwa ina eksipaya. Marafiki wa Hitler walisha fulia. Marafiki wa Idd Amini wako wapi? aliyefaidi kwa hili mwisho wake unakuja.

Nyumba hizi zilidhalilishwa. Hivi karibuni nimesikia kwamba hata waliompa PhD magufuli pale UD waligawiwa nyumba za serikali.

Thamani ya ardhi hutegemea eneo. Ktk miji mikubwa mfano ile ya uropu, ardhi huwa na thamani kuliko hata hilo jumba lenyewe kwa maana kwamba huwezi uka devalue ardhi kama jengo.

Hizo nyumba wafurahie tu kwa sasa kwa kuwa CCM bado wako madarakani lakini ni bahati mbaya kwao maana tunaelekea kuwapoteza CCM. Hapo hawatakwepa kuzirudisha maana ktk nchi hii hakuna sheria inayoruhusu ardhi kwa matumizi ya umma iwe ya mtu binafsi. Hata siku moja!
 
..wangeuza chache kwa wawekezaji kama NSSF,NHC, etc, na kuvunja na kujenga nyingine ktk maeneo husika.

..kama serikali ilikuwa inataka kuwasaidia watumishi wake kumiliki nyumba basi ingewapatia mikopo nafuu ya ujenzi wa nyumba.

..halafu kuna wengine walikuwa hawastahili kabisa kupewa nyumba hizo. fikiria mtu kama Raisi Mkapa amepewa nyumba halafu serikali imemjengea nyumba nyingine kama haki yake ya mafao.

NB:

..kwenye nchi za wenzetu ukipewa nyumba ya msaada na serikali basi inakuwa na masharti kibao ikiwemo kutoruhusiwa kuiuza kwa faida kubwa, kuipangisha etc etc. wanafanya hivyo ili mhusika asi-abuse system na kutumia ujanja kuikosesha serikali mapato.

..sote tunaona kwamba hao "watumishi masikini" wamevunja nyumba walizopewa na kupandisha sky scrappers. kwa msingi huo serikali ilipowauzia ilijikosesha mapato kwani ingeweza kujenga hizo sky scrappers na kuzipangisha yenyewe.
 

Watu kama nyinyi ndio tunawatafuta na mawe huko barabarani........................... Yaani unatetea upumbavu gani wewe. fikiria kwanza kabla ya kuitetea hiyo serikali yako ya kipumbavu.

Kimtazamo kama serikali ilikuwa inawapenda watumishi wake ndio ingetumia haya maeneo kujenga maplot ambayo yangesaidia watumishi wengi zaidi. Hatakama wangejenga kwa mikopo watumishi wangelipa kodi na deni lingelipwa. Hivi viwanja vingekuwa ni dhahabu kwa watumishi na serikali kama vingesimamiwa vizuri bila ubaguzi. Haya maplot yangewasidia sana sana watumishi wanaoanza kazi wanaohamishwa na wananchi pia wanapopata matatizo kama mafuriko, nyumba kuungua na wanapoingia mahali ambapo sio wenyeji kwa mkataba maalumu, kwa ajili ya kujiandaa kuingia huko uraiani. Iwe amejenga iwe amepangisha mkataba ukiisha bye bye.
 

si bure wewe ni kati ya waliofaidi nyumba za serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…