Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Mkuu Lunyungu,

Sikujua kama muda wa mtu kuwepo hapa forums unamfanya huyo mtu kuwa na ujuzi zaidi wa mambo! Mimi sina ugomvi wowote na Zitto. Soma posts zangu zote hapa jf na utagundua kuwa leo ni mara ya kwanza kwangu kuwa na debate na Zitto.

Sidhani kama nimekuzuia kujadili mambo ya maana kwenye hii thread. Yaani watu mnaanza wenyewe kumuingiza Zitto kwenye mjadala (huku Zitto naye akiwaunga mkono kwa kujikwoti hapa), watu wengine nao wanaingia kutaka kujua upana na uhusika wa Zitto na kisha hilo linakuwa tatizo?


Mimi nimesha kueleza bwana drop that please.Una matusi la wazi wazi eti kwamba Zitto anatushikia akili tuna ingia mkumbo .This is not acceptable at all . Hata wewe ukifanya kitu tukaona we will always agreed and support you .Sasa tafadhaliu jua kwamba hakuna wa kufuata mkumbo . Zitto huwa anapingwa hapa openly pale hawawezin kukubaliana naye na hilo halina shida hapa ni JF . Maswali unayo uliza sasa muulize JK na kundi lake , mtu kuji kwoti is never a sin ila anaonyesha msisito wa kile alicho kisema wakatu watu kama nyie mnapo anza kuupika ukweli kuufanye uongo .

Muhimu ni kwamba JK awe faster learner na si kila kitu lazima awazie CCM . Watanzania over 30mn wana CCM ni less than 5mn sasa iweje kila mara CCM iwe ya kwanza Taifa langu liwe na mwisho na atake uongozi kwa jina la Nchi yangu Tanzania lakini akishapata madaraka anaimba CCM kwanza ?
 
ushauri wa zitto ilijulikana wataufuata ...sema walikuwa wanaogopa kuonekana wamefuata ushauri wa mpinzani[inside]......ndio maana wanasingizia shinikizo la wafanyabiashara....ukweli ni kuwa hata ushauri wa kuimiliki dowans au kuomba watanzania wenye uwezo wauwashe na kuwauzia tanesco umeme ...utafanyiwa kazi karibuni....ila serikali hii ...inashangaza rais hana balls za kuamua anaogopa ogopa...hadi ashikiwe ...kitu mkononi...
 
Mimi sasa naamini kabisa kuwa nchi hipo kwenye autopilot, maana mpaka matatizo yawe makubwa ndio uHAMUZI UTOLEWE TENA BAADA YA KUPATA IDEAkutoka kwa watu walioko nje ya serikali.

tatizo ni kuwa wanafikiria bkuficha ufisadi wakati wote kwahiyo hawawezi kufikiri kutatua matatizo yaliyopo wakati ufisadi unawaandama
 
Inasikitisha sana kuwa watu wansifia uamuzi huo.

Ilitakiwa watu zamani sana kuwa wameandamana kupinga MGAO.

Na mwakani muwachague hao hao wanaosubiri hadi dakika ya mwisho, utafikiri POLISI kwenye film za Marekani ambao huwa wanakuja wakati kazi imeisha...........

Kila siku Tanzania itaishi kwa umeme wa Dharura. Maji yakijaa na umeme kuwa mwingi watu tunalala tena. Unaweza kupata mwanga kuwa tumerogwa......
 
JK mkuu, cha kufanya ni kuwaita Wartsila, Ericsson na GE hapo TZ very soon, kuwe na kikao na uwaambie TZ tunahitaji gas powered generators za 300MW kwenye fast track modality, watoe quotes na since hayo makampuni yote ni among the world best, mwenye quote ya bei ya chini ndie apewe hiyo tender ili say in 12 months, tuwe tumemaliza hii issue once and for all.

Mkiwasha IPTL week ijayo ukitokea uharibifu mwingine kwa juhudi za kina Rostam tutakuwa tumerudi palepale.

Hapa tunaweka plaster kwenye tatizo, KATA MZIZI WA FITINA JK watu tumove on na uwekezaji sio tunaact kama huu ni mwaka 1947.
Mkuu Moelex23,

Well said. Natamani mkuu wa kaya asome vema mistari hii!
 
Haya ni maswali mazito sana Kaizer. Labda swali la kuongezea tu - kama wanaweza kuamuru (au kushauri kama Zitto alivyofanya) leo kuwa IPTL iwashwe? nini kitawazuia kesho wasiamuru (na kushauri) kuwa izimwe?


Kimsingi hakuna, kisha nimefikiria hivi bado si tunafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, msingi wake ukiwa kwenye azimio la arusha, ambapo utaifishwaji wa mali kwa maslahi ya taifa ulikuwa justified.

Mi nadhani JK ainvoke tu kale kajitabu ka mwalimu ka azimio, hakuna natakayemuuliza !
 
JK amesambaza taarifa hii kwenye vyombo vya habari bila kumjulisha Ngeleja, Jamaa mpaka sasa anaongea pumba tuu.

sasa yeye ndo pumba zaidi atapelekaje taarifa kwenye vyombo vya habari kwani ndo vinavyotekeleza maagizo yake au?kuongozi nchi si lele mama
 
Ningelikuwa Millionea basi ningelifanya tangazo kwenye CNN, BBC, Fox, Al-Jaazir, nk kuwa msije kuwekeza Taanzania hadi ile nchi iwe na umeme wa uhakika na maji ya uhakika. Na ningelisubiri mtu anitukane na kuniandama kama yule jamaa wa film za Mapanki na hapo ningelimpa habari /maneno yake.

KATUNI(48).jpg
 
Ningelikuwa Millionea basi ningelifanya tangazo kwenye CNN, BBC, Fox, Al-Jaazir, nk kuwa msije kuwekeza Taanzania hadi ile nchi iwe na umeme wa uhakika na maji ya uhakika. Na ningelisubiri mtu anitukane na kuniandama kama yule jamaa wa film za Mapanki na hapo ningelimpa habari /maneno yake.
Sikonge,hii ya mapanki imenikumbusha mbali sana! Huwezi amini wale watu waliokwenda kuandamana karibu nusu yao mlo wao wa mchana siku hiyo kitoweo kilikuwa mapanki,halafu wakaenda kuandamana kulaani ile filamu na kusema wao hawali Mapanki!
 
Sikonge,hii ya mapanki imenikumbusha mbali sana! Huwezi amini wale watu waliokwenda kuandamana karibu nusu yao mlo wao wa mchana siku hiyo kitoweo kilikuwa mapanki,halafu wakaenda kuandamana kulaani ile filamu na kusema wao hawali Mapanki!

Duu,
Yaani waliandamana kupinga kuwa hawajala wakati ndiyo kwanza wametoka kula? Nilicheka kumsikia mama yule aliyekuwa akiongea kazini na akawa akisema "Nalidukwa..." yaani natukanwa hahaaaaa...... Halafu huyohuyo si ajabu na yeye alipewa visenti akaenda kuandamana kuwa wao HAWALI.

Ila wale PANK wengine walikuwa na sura hao!!! Macho makubwa kama ng'ombe..... Na yule Dogo aliyetengeneza gari lake kwa viwaya na akalichukua pank moja na kulipakia....... Mhhhh, eti roli la mapanki linauzwa laki moja?? Hapo unaona kuwa CCM is here to stay.
 
Kama mambo yenyewe ni haya,bora TIC waweke wazi kipengele cha upatikanaji wa umeme kwa Investors "Invest at your own risk" kuliko fedheha hii tunayoipata sasa.
 
Kama mambo yenyewe ni haya,bora TIC waweke wazi kipengele cha upatikanaji wa umeme kwa Investors "Invest at your own risk" kuliko fedheha hii tunayoipata sasa.

Hahahaha:lol: hapo nadhani ndio tutaambiwa tuna vigezo bora vya uwekezaji maana tutakuwa tumeamua kuwa wa-wazi!
 
Rais ni reactive. Anatakiwa awe proactive.

Kikwete hana huo ujasiri. Hana uti wa mgongo wa kufanya maamuzi magumu. Anapendelea kutafuta njia rahisi ya kutokea. Mpaka abanwe kwenye kona ndipo angalau ataongea la maana. Mifano ipo mingi tu. Bogus kweli huyu jamaa!
 
Sasa naanza kuelewa ni kwa nini nchi nyingine Africa zinakuwa na mapinduzi ya kijeshi. Tuna raisi kihiyo wa uongozi na mawazo na anataka aendelee kuiingiza nchi jangani. Wenye uwezo wa kusema basi kazi imekushinda ndio akina Msekwa wanaozidi kumpigia debe kuwa hakuna mwingine zaidi yake.

Wako wapi wenye busara ndani ya CCM ili wamueleze JK kuwa hawezi kazi (yuko uchi)? CHADEMA huu unatakiwa uwe ndio wimbo mpya, sema wazi kuwa JK kazi haiwezi.
 
Mitambo ya IPTL ikiwashwa je, mgao wa umeme utakuwa haupo tena?
Kama sikosei taarifa zinasema kuna upungufu wa Megawati 150. IPTL wakizalisha hizo 100MW halafu Songas wakiwasha huo mtambo unaofanyiwa matengenezo wa 20MW zitakuwa zimebaki MEGAWATI 30.

Vipi kuhusu hizi 30MW itakuwaje? Je, watazifidia vipi ili mgao usiwepo kabisa?

Suluhisho la haraka na litalokuwa na immediate impact ni JK kutoa amri kuwa mitambo ya Downas iwashwe mara moja na mambo ya kutaifisha, kuinunua au kuikodisha yafuate baadaye. Akifanya hivyo leo leo hakuna mtu atakaye lalamika kwani wapinzani wa kubwa wa hili wamekwisha onja joto ya jiwe.

By the way, Jamani, Dk. Mwakyembe yuko wapi? Mbona kaingia mitini hivyo? Hata kujitokeza kutufariji wenzake tuanoumia kutokana na maamuzi yake?
 
Hahahaha:lol: hapo nadhani ndio tutaambiwa tuna vigezo bora vya uwekezaji maana tutakuwa tumeamua kuwa wa-wazi!

Ni bora tuwe wa-wazi kuliko usanii huu tunaoufanya,aidea ya Sikonge ya kutumia CNN,BBC na Aljazeera,ni muafaka kabisa.Hivi unaweza amini TANESCO wako confortable kila siku kutoa matangazo ya ratiba ya Mgao wa umeme magazetini ,utadhani ni sifa badala ya kutafuta njia za kutatua tatizo lenyewe.
 
Bottomline is not about who said what first and who suggested what at what time, what is important is whether this situation could have been prevent and thus save billions of shillings 3 weeks ago, and the answer is yes this situation was preventable... what has changed regards to the iptl saga between then and now, nuthin..., yaani point ngogo ndogo kama hizi JK anatakiwa azichangamkie chap chap maanake they are no brainers and they are quick wins!!!!! 2010 jamani......
 
KULA BREAK:

Jamaa akiendesha BMW mpyaa kwenye highway na ghafla akapitwa na kigari kimechokachoka cha Hyundai. Kwenda mbele jamaa wa BMW akakuta ile Hyundai imesimama na jamaa anajaza maji sehemu ya injini. Jamaa kaenda ghafla akaina tena Hyundai inakuja wanguwangu na ikampita vuuuuuhhh. Jamaa kwenda mbele akakuta mchezo ni uleule, gari linajaza maji. Jamaa wa BMW kaongeza mwendo na kwa mara ya tatu akapitwa tena vuuuuu. Kwenda mbele akakuta gari imesimama na maji yanaongezwa. Jamaa wa BMW akasimama na kwenda kuangalia hilo injini linalokunywa maji namna hiyo.
Kufika pale akaangalia kwenye injini na kukuta Minigeria mitano. Yote imejaza msuli ile mbaya ila minne imechoka ile mbaya na mmoja anachekelea si kawaida. Jamaa akamuuliza yule mwenye kuchekelea "sasa wewe unacheka nini?" Jamaa akamjibu " Mimi leo niko kwenye gia ya kurudi nyuma (riverse)".

Itabidi nitafute Mi-9geria kadhaa iwe inaendesha mitambo ya kuzalisha umeme....
Turudi kwenye umeme....
 
The real menace of our Republic is this invisible government which like a giant octopus sprawls its slimy length the nation. Like the octopus of real life, it operates under cover of a self created screen....At the head of this octopus are Dowans,Kagoda and the likes interests and a another group of powerfully investors and business personell. The coterie of powerful inestors and business personell virtually run the Tanzanian government for their own selfish purposes. They practically control the political party in power.

Our government has forgotten its role to their people and the Tanzanian people are simply forgetting their role to their own government!

Ohoo! Unaturudisha kulekule kulikosababisha mpaka tuwe gizani hivi sasa. "Mitambo ya IPTL na Dowans haina dhambi yeyote. Wenye dhambi ni wale walioruhusu nchi kuingia katika mikataba mibovu" Quote from Elvis Musiba yesterday.
 
Back
Top Bottom