Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Ninajiquote nilichosema tarehe 15/10/2009

Ninapendekeza;

  • Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
  • Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhuInaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.
  • Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.
Mnisamehe kwa kujiquote!

Ikulu inasema wafanyabiashara ndio wamemwomba Rais. Ni sawa tu........

Tenda Wema wenda zako ndugu yangu...lakini kwenye ukweli siku zote uwongo hujitenga. Tunaofuatilia mambo ya Tanzania kila kukicha tunajua wewe ndiye uliyekuwa wa kwanza kutoa kauli hiyo. Bravo Zitto!
 
Umejikwoti hapo juu ukieleza kuwa ulishauri kuhusu IPTL.

Je ulipendekeza IPTL na Dowans baada ya kuulizwa au ni uamuzi binafsi?

Mkuu pse,
Do your homework very well before you come here.
 
Kwani Zitto ni waziri wa Umeme Tanzania?..
nilimaanisha kikwete, kwamba , kwanini sasa , na kwanini tumefika hapa, maana uamuzi wa leo umetoka kwa kikwete au hapa tunamjadili zito? thread ya pendekezo la zito si ipo?
 
Zitto ameanza kujikwoti hapo juu kuwa yeye ndiye alitoa hili wazo la IPTL. Je alilitoa kama nani? umejiuliza hilo swali?

Kama Mtanzania ambaye alifahamu tatizo la mgao lilikuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi.
 
Jifariji tu na nafsi yako. My record is clear

That's correct.

Your record is clear that; almost a year ago, you went on record urging the Govt to buy Dowans power generation machines (whatever the name). For you, it was an emergence then (at is still an emergence now).

A whole year of emergence in making.
 
Rais? rais gani? Hii autopilot ndiyo mnaiita rais?
 
Zitto ameanza kujikwoti hapo juu kuwa yeye ndiye alitoa hili wazo la IPTL. Je alilitoa kama nani? umejiuliza hilo swali?

Na wewe unamuuliza swali hili kama nani, umejiuliza swali hili....na unachangia mjadala wa maswala ya mgao wa umeme tanzania kama nani?..Ngeleja?.?
 
Namba nne na namba tano zote zinakaribiana ila kwanza Kevo anabishana kuhusu namba moja au mbili. Bado namsubiria afanye chaguo lake.

Mkuu,

Siko hapa kufanya league na wala hilo haliko kwenye list yangu!
 
Sasa kuna maana gani ya kuwa na wasaidizi, basi tufute baraza la mawaziri, au unasemaje mkuu?.

Badala ya kujibu swali wewe nawe unauliza swali.

Jibu swali kwanza ili uwe kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuuliza swali pia. Narudia swali langu.

-- kama kazi zote za utendaji wa serikali zinafanya (au zinatakiwa kufanywa) na wasaidizi wa raisi, kazi ya raisi ni ipi?
 
naona topic imegeuka imekuwa Zitto..mmesahau mna matatizo ya umeme tayari naona,nasikia mbaya lakini mkome maana wenyewe ndio mnawachagua wale talebani AKA CCM wanaowaletea shida zote hizi!
 
Mitambo ya IPTL ikiwashwa je, mgao wa umeme utakuwa haupo tena?
Kama sikosei taarifa zinasema kuna upungufu wa Megawati 150. IPTL wakizalisha hizo 100MW halafu Songas wakiwasha huo mtambo unaofanyiwa matengenezo wa 20MW zitakuwa zimebaki MEGAWATI 30.

Vipi kuhusu hizi 30MW itakuwaje? Je, watazifidia vipi ili mgao usiwepo kabisa?
 
Back
Top Bottom