Kikwete abariki kura ya wazi

Kikwete abariki kura ya wazi

ccm janga la kitaifa, wanataka kura ya wazi ili kila mwananchi ashuhudie, lakini hawataki waandishi wa habari waingie kwenye kamati ili mwananchi aelewe jinsi majadiliano yanavyoendelea. Hapa hakuna jipya wachosaka ni kushughulikiana.
 
Kura ya wazi ndio itaonyesha dhamira ya mjumbe kama yupo upande wa Watanzania ama ana yake binafsi kwenye bunge maalumu.

Wale wote wenye kutaka kura ya siri ni dhahiri tayari wameonyesha kuwa wana ajenda zao zenye maslahi kwao tu. Watanzania kwenye hili hatuwezi kukubali.

Dhamira ya kila mjumbe ni lazima ijulikane. Katiba hii ni ya kila raia, sasa kwanini ninyimwe haki yangu kushuhudia kura gani imepigwa kwenye kila kifungu!?
 
Kura ya wazi ndio itaonyesha dhamira ya mjumbe kama yupo upande wa Watanzania ama ana yake binafsi kwenye bunge maalumu.

Wale wote wenye kutaka kura ya siri ni dhahiri tayari wameonyesha kuwa wana ajenda zao zenye maslahi kwao tu. Watanzania kwenye hili hatuwezi kukubali.

Dhamira ya kila mjumbe ni lazima ijulikane. Katiba hii ni ya kila raia, sasa kwanini ninyimwe haki yangu kushuhudia kura gani imepigwa kwenye kila kifungu!?

Kwani kuna mjumbe wa bunge la katiba ambaye umemchagua mpaka ujue dhamira yake?

Kosa kubwa lililofanywa ni kuwachagua wanasiasa kuwa wajumbe wa bunge la katiba.Tangu lini muajiriwa akamtungia sheria muajiri?Wananchi ni waajiri wa wanasiasa kwa hiyo obviously wao ndo walipaswa kwenda kuwatengenezea wanasiasa sheria wanasiasa jinsi ya kutawala!

KUSHIRIKI KWA WANASIASA TU KWENYE BUNGE HILO,KUNAIFANYA KATIBA ISIWE YA WANANCHI!

TUNATAKA KIONGOZI ATAKAYELETA KATIBA MPYA YA WANANCHI 2015!
 
Ndiyo maana tunataka maamuzi ya upatikanaji wa KATIBA MPYA uandaliwe na hili BUNGE maalumu la katiba, na siyo kundi lolote. Hivyo ni vema vyama ama makundi yoyote yasishinikize misimamo yao, ni vizuri wakubaliane kwa hoja za msingi katika mambo yote.

What You are saying Is Just a MYTH, kila kundi linashinikiza kile wanachotaka kwa maslahi Yao na si kwa maslahi ya watanzania. Huo ndo ukweli!
 
Anguko la ccm limetimia, mfa maji haachi kutapa, ndicho kinachowakumba ccm, wanajua tumekwisha, ila ndio hivyo wanajaribu kujinasua kama mf maji, msiogope watanzania, tunao wakombozi kule bungeni, ni wachache ila ni matajiri wa hoja za kumkomboa mtanzania, tuombe Mungu awalinde na njama mbovu dhidi ya ccm, kwa ajili ya kutupigania wanyonge.
 
Kwa watanzania waliodhani tutapata katiba mpya poleni, katiba inayoandaliwa ni ya ccm na sio watanzania, poleni sana watanganyika, katiba mpya chini ya ccm ni ndoto!
 
Niko hapa Dodoma na weekend hii nilikuwa mitaa mbalimbali ikiwemo CHAKO NI CHAKO ambako wakubwa wanaenda kuteketeza kuku. Ili nipate habari za CCM nilitinga kama wenyewe. Katika mazungumzo ya wengi wa wabunge wameapa kutetea Tanganyika iwepo kwa namna yoyote kama wenzao wa Zanzibar walivyobadilisha katiba yao na kujipa karibu madaraka kamili.
Mmoja wao alisema " niko tayari kufukuzwa CCM mbona vyama viko kibaao na pia tutapitisha mgombea binafsi shida iko wapi?. Licha ya mgombea binafsi sisi watu 90 tumeshajipanga kuhamia CHADEMA . Kwa hiyo kama ni kadi yao wachukue tu lakini hatuwezi kuwatelekeza wananchi watatuona kama hatuna akili timamu, wananchi wamesema wanataka Tanganyika yao na sababu za msingi zipo tele halafu kikundi kidogo cha watu kituburuze !!! hakika watakula wa chuya siku ya kuipigia kura Tanganyika hakika CCM hawataamini macho yao. tutasimama wote kuiunga mkono iwe kura ya wazi au ya siri" mwisho wa kunukuu na ninawasirisha. Je hapa nani ataibuka mbabe CCM au wabunge wa wananchi.
 
Mpaka dakika hii dalili zinaonyesha Tanzania itaongozwa na katiba itakayotungwa na kuridhiwa na CCM. Hii ni hatari kubwa sana kwani tulihitaji katiba ya wananchi. Kura ya wazi inayopigiwa debe na ccm ina ajenda ya siri na iko kimkakati zaidi. Hivyo rai yangu kwa wajumbe walio makini ni kuondoka mapema huko bungeni na kuwa acha hao ccm wafanye watakalo kwani wingi wa wa wajumbe watautumia vibaya kura ya wazi ikipita. Najua posho ya 300000 kwa siku zitawauma lakini Mungu awape nguvu muokoe taifa.
 
kama ni kweli tusubirie tuone hiyo siku

ni kweli mkuu na pia Wazanzibar wameapa kuwa hawako tayari kwa hoja yoyote ya kuipunguzia Zanzibar madaraka au kuifanya mkoa. Sasa hapo unategemea nini.
 
Kama kuna haja ya kura ya wazi basi wala haina haja ya kupiga kura,tuashumu tu kwamba watu wote wana maamuzi sawa kwasababu wenye maamuzi sawa hawana haja ya kupiga kura vinginevyo ni upotevu wa rasirimali,ila tumeweka kura kwasababu tunaelewa kwa kila jambo kuna mitizamo tofauti na siyo kweli kwamba kila anayekuwa na hoja tofauti ni mbaya ama adui kama inavyotaka kuoneshwa na CCM kwa wenye mitizamo tofauti ..mbona jambo la heri,kitaifa na amani kuhusu Zanzibar mwaka juzi watu walipiga kura za siri?
 
wajumbe wasikubali kura ya wazi, kukubali kura ya wazi ni sawa na usaliti kwa wananchi, ccm tumekwisha wafahamu.
 
Alafu hii nchi tokea imekuwepo watu tumeshiriki katika shughuri zote za kidemokrasia kwa kuamua mustakabali wa Taifa letu kwa kupiga kura,kura ya siri.Sasa inavyotokea leo mnawaambia wananchi tunaanza kura za wazi kwanza ni kuwachanganya wananchi lakni pia CCM wajue haitaishia hapo,itabidi sasa masuala yote ya kuamua masuala ya kitaifa kama kumchagua Mbunge na Rais pia mtuandalie utaratibu huu mpya ili mambo muhimu yote ya nchi hii yawe wazi na si siri tena,na kwa kuanza pia tunataka wanahabari waruhusiwe
 
Safi sana mheshimiwa rais lazima wanafiki wajulikane na wanasiasa muflis wafyekwelewe mbali sioni mantiki ya kura ya siri kwenye maslahi ya kitaifa hapo ndo pa kuwasaga saga wenye ndimi mbili

Katiba ya ccm au ya nchi?
 
hatutaki mambo ya siri sir hapa,tunataka uwazi,anaye taka kufanya siri akafanye chumbani na mkeo

Mbn kura za urais ubunge mpaka Diwani mnapiga za siri na hamjawah kusema ziwe za wazi?
 
Mungu inusuru nchi yetu.tumeaminishwa kuwa kila mtu anaweza kuwa Rais wa Nchi hii.bahati mbaya hata wenye uelewa kama nazi Koroma sasa wanatuongoza.Huyu hana tofauti na Mangungu!

Utadhani hana ubongo aisee
 
Back
Top Bottom