Kikwete abariki kura ya wazi

Kikwete abariki kura ya wazi

Nasikitika kwa Rais Mzima kubariki upuuzi huu kama ni hivyo hakika hakuna tena Katiba.
 
Kura ya wazi ndio itaonyesha dhamira ya mjumbe kama yupo upande wa Watanzania ama ana yake binafsi kwenye bunge maalumu.

Wale wote wenye kutaka kura ya siri ni dhahiri tayari wameonyesha kuwa wana ajenda zao zenye maslahi kwao tu. Watanzania kwenye hili hatuwezi kukubali.

Dhamira ya kila mjumbe ni lazima ijulikane. Katiba hii ni ya kila raia, sasa kwanini ninyimwe haki yangu kushuhudia kura gani imepigwa kwenye kila kifungu!?

mbona wandishi habari wanazuiwa kukuhabarisha yanayojiri kwenye kamati? na je, kwanini nchi inapoteza pesa kibao kununua masanduku na makaratasi ya kura? kwanini watu wasipange mistari nyuma ya wagombea wanaowataka? magamba acheni unafiki wenu.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwenyekiti wa ccm taifa amewataka wajumbe wote wa bunge maalumu la katiba wanaotoka chama cha mapimduzi wasipige kura ya siri na yoyete atakaye unga mkono kura ya wazi atakuwa ameenda kinyume na matakwa ya chama

Mnduku sana huyu jamaa
 
Hapa kuna hatari ya kupata katiba ya ccm wala si ya watanzania. Ushauri wangu wabunge 201 na wale wa upinzani wasusie wabaki wabunge wa ccm kuonyesha msimamo wao
 
Ni kweli kabisa!!! Maana imeonekana jitihada za Pinda zimegonga mwamba....Mimi nasema unafiki na udhaifu wa mkuu wa kaya ndiyo unaipeleka nchi pabaya...

Kama alikuwa hataki Katiba mpya kwanini aliruhusu mchakato wa Katiba? Tume ya Warioba imetumia billions of shillings kukusanya maoni, leo CCM wanataka kuturudisha nyuma..

CCM na ilaniwe...

Mnyika alisema "tumefika hapa sababu ya raisi dhaifu" wakamuona ----- haya
 
Hili bunge livunjwe tu,mara msimamo wa ccm,mara ukawa,mi sioni maana yoyote ile,kama ccm hawakuwa tayari na mchakato wa katiba mpya si wangeacha tu kuliko kuisababishia nchi hasara kwani tumeona hakuna cha maana kinachojadiliwa na tunakaribia kumaliza mwezi sasa.
Kuna mambo yanafanyika katika nchi hii ambayo hayawezi au hayajawahi kufanyika mahali popote pale ulimwenguni.
 
Tunataka kura ya Siri tu hii ya wazi
Wakapigiane kwenye vikao vyao vya kiccm
Wasituvurugie nchi hapa tunataka katiba
Ya wananchi sio ya chama.
 
Na shauri Kama ccm watalazimisha
Kura ya wazi makundi yote ikiwemo
Vyama vya upinzani waondoke Dodoma
Waiache ccm .alafu sisi wananchi tuanze kuisaka
Tanganyika kwanguvu tuone Kama wataweza
Shindana na wananchi .maana hawa Maccm
Hawaitakii mema nchi hii Kama Noma iwe Noma
 
mimi naumia sana hivi kweli ccm wanafanya mambo haya, hawana huruma na wananchi wajue watu waliofika kuanzia kidato cha nne tunawashangaaaaaa ipo siku
 
Kura ya Bunge la Katiba si haki ya Mjumbe mwenyewe ni haki ya Kundi au Genge unalowakilisha. Kama wewe ni Mwakilishi wa NGO lazima NGO husika ijiridhishe kama umetekeleza ulichotumwa na Taasisi yako? Mwakilishi wa Walemavu yuko pale kuwakilisha mawazo ya walemavu sio yake binafsi, walemavu wanahaki ya kujua aina ya kura aliyopiga mwakilishi wao kuepuka kununuliwa au kuuzwa kura yao. Kura ya Siri ina harufu ya wizi au vishiria vya Rushwa.

Kwa akili yako uliyochukua lumumba nani mwinge zaidi ya ccm anaweza kutoa rushwa kununua kura hapo bungeni?
 
hatutaki mambo ya siri sir hapa,tunataka uwazi,anaye taka kufanya siri akafanye chumbani na mkeo

na kura za uchaguzi ziwe zinapigwa wazi au unaonaje? hakuna haja ya kuingia gharama kununua masanduku na karatasi za kura. sawa?
 
Silly country! Badala raisi ahimize umoja yeye anahimiza mpasuko!!! Basi tu tumechelewa ila ilifaa itungwe sheria ya kuzuia mikutano/vikao vya vyama toka bunge maalumu linaanza hadi linaisha!

unamshangaa? huyu huyu cheap president ndiye aliyewataka wanaCCM kuacha unyonge na kuwashauri waanze kuwashambulia wanaCHADEMA. The weakest president TZ has ever had!!!
 
Hayo sio majibu wewe,muda mwngne utumie akili na sio kua -------- wa kuburuzwa tu na hisia za watu,unajua kwa nin waliweka kura za siri hata katika uteuzi wa rais,wabunge na diwani?usiweke akili matakon na kuja kuongea ili mradi uonekane,tunaiharibu nchi kwa upumbavu mdogo tu ambao na wewe unachangia

swadakta. nadhani huyo gamba amekuelewa sasa maana hawa magamba wakati mwingine ni wagumu sana wa kusikia. nadhani magamba yamefunika hadi machoni na masikioni...hawaoni na wala hawasikii.
 
Mbn kura za urais ubunge mpaka Diwani mnapiga za siri na hamjawah kusema ziwe za wazi?

Hilo ni jambo tofauti. Hakuna maamuzi ya kikao yanayopigiwa kura ya siri. Na hakuna maamuzi ya Bunge lolote Ulimwenguni linalofanya maamuzi kwa kura ya siri. Tofautisha na kumpigia mgombea kura au kura ya maoni, hivyo ni vya siri
 
na kura za uchaguzi ziwe zinapigwa wazi au unaonaje? hakuna haja ya kuingia gharama kununua masanduku na karatasi za kura. sawa?

Unazungumzia mambo mawili tofauti, kumpigia mtu kura na kupiga kura ya maamuzi katika kikao
 
Kura ya siri mbona ndiyo ustaarabu jameni, Tuelimike, tutekeleze.

Aina zote mbili za kura ni za kistaarabu, lakini zina kazi tofauti. Hakujawahi kuwa na kura ya siri katika maamuzi ya kikao au ya Bunge popote. Katika kumchagua mtu ni lazima kura iwe ya siri
 
Nasikitika kwa Rais Mzima kubariki upuuzi huu kama ni hivyo hakika hakuna tena Katiba.

Si upuuzi. Ni vizuri kujielimisha. Kura ya maamuzi ya Bunge huwa ni ya wazi popote pale. Ni kura ya kumchagua mtu tu ndiyo huwa ya siri
 
Hapa kuna hatari ya kupata katiba ya ccm wala si ya watanzania. Ushauri wangu wabunge 201 na wale wa upinzani wasusie wabaki wabunge wa ccm kuonyesha msimamo wao

Haiwezi kuwa ya Watanzania kwa kuwa itapitishwa na wengi, ambao ni CCM? Ipitishwe na wachache ili iwe ya Watanzania? Hebu fafanua.
 
Back
Top Bottom