Kikwete abariki kura ya wazi

Unazungumzia mambo mawili tofauti, kumpigia mtu kura na kupiga kura ya maamuzi katika kikao

kwani kura ya uchaguzi sio kura ya MAAMUZI ni ya nini kumbe? ikiwa CCM wanataka ipigwe kura ya siri ili wawajue watu wanaopiga kura hiyo kuna haja gani sasa ya kupoteza fedha kununua masanduku ya kura? basi, watu wawe wanapiga mistari nyuma ya wagombea na kuhesabiwa badala ya kubebeshana mizigo ya gharama za kununua masanduku ya kura na makaratasi ya kupigia kura. tangu zamani tumekuwa tukipiga kura za siri na kamati ya kumshauri mwenyekiti kificho imesema kwamba upigaji kura wa aina yoyote(siri au wazi) una nguvu sawa. sasa kwanini tusiegemee kwenye kura ya siri (kama ilivyo kawaida ya upigaji kura tangu enzi za mababu) badala ya kupoteza muda wa watanzania? au kwa kuwa wanaodai kura za wazi ni CCM ndio maana mwenyeketi kificho (mwanaCCM) naye anafuata matakwa ya CCM. ikiwa kura za wazi zina nguvu sawa na zile za siri kwanini basi CCM wang'ang'anie kura za wazi? si wakubali kura za wazi ili mjadala uendelee badala ya kupoteza muda na kuzidi kutafuna pesa za umma? unasemaje kuhusu hili?
 
Hilo ni jambo tofauti. Hakuna maamuzi ya kikao yanayopigiwa kura ya siri. Na hakuna maamuzi ya Bunge lolote Ulimwenguni linalofanya maamuzi kwa kura ya siri. Tofautisha na kumpigia mgombea kura au kura ya maoni, hivyo ni vya siri

ikiwa kamati ya kumshauri kificho inakubali kwamba kura zote (siri au wazi)zina nguvu sawa, ni kwanini CCM bado wanazidi kung'ang'ania kura za wazi kwa maslahi ya chama badala ya maslahi ya wananchi? acheni ugamba wenu, tutengeneze katiba ya nchi. sisi tusiokuwa na vyama tunaumia sana tunapoona serikali ya CCM ikitaka kuchakachua katiba ya wananchi. kama vipi wapinzania na wajumbe 201 wataondoka dodoma na kuwaacha CCM watengeneze katiba yao ya CCM. katiba ya wananchi itatengenezwea mwaka 2016 baada ya CCM kuondoka madarakani. wanaudhi sana hawa magamba bhana!!!!!!!
 
Si upuuzi. Ni vizuri kujielimisha. Kura ya maamuzi ya Bunge huwa ni ya wazi popote pale. Ni kura ya kumchagua mtu tu ndiyo huwa ya siri
popote pale wapi? Jieleimishe kwa kuangalia nchi nyingine zilitengenezaje Katiba na wao kataiba haikutengenezwa kwaniaaba ya Chama kilichopo Madarakani bali ilikuwa kwa malengo ya kupata katiba ya kuweza kuwajenga wao na kuwa wamoja si hii inayofanyika leo baadhi ya wanachama wa CCM mfano ataunga mkono swala la kura ya siri basi atafukuzwa uanachama je Democracy ya mtu ipo wapi hapo? Sasa na wewe ni kuite Mpuuzi kwa kutoelemika na kufuata mkumbo
 
2015 si mbali amalize kwani sijaona mpaka sasa kama anafanya lolote kwa maaslahi ya taifa zaidi ya ccm, na ubinafsi
 
Yaah.. nafikiri mpango wa kuwa na sirikali tatu kaburi lake limewadia. Hongera CC kwa maamuzi magumu..!
 

Hivi na yeye alichaguliwa kwa kura ya wazi siyo? Na huko CC na Halmashauri kuu ya Chama na hata mkutano mkuu hufanya mambo kwa kura ya wazi siyo? Kama hawafanyi hivyo basi wanahujumu watanzania. Kama wanafanya hivyo basi ni utamaduni wao nawapongeza.
 
Si upuuzi. Ni vizuri kujielimisha. Kura ya maamuzi ya Bunge huwa ni ya wazi popote pale. Ni kura ya kumchagua mtu tu ndiyo huwa ya siri

Tahmini naomba uweke CV yako hapa kwa kuwa unashindwa kujua tofauti ya vikao na mambo yanayobishaniwa huwamuliwa kwa namna gani. Kama CV yako imekaa vizuri utajua kuwa linapotokea jambo linalobishaniwa na zaidi sana jambo linalogusa nafsi ya mtu na mfumo jambo hilo huamuliwa kwa kura ya Siri. Kwa kuwa mambo mengi ya katiba yamekasimiwa yaamuliwa na nafsi za watu waliotumwa bila kushinikizwa na mifumo iliyowatuma huko basi kura ya siri ndiyo haki ya mtu huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…