tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Unazungumzia mambo mawili tofauti, kumpigia mtu kura na kupiga kura ya maamuzi katika kikao
kwani kura ya uchaguzi sio kura ya MAAMUZI ni ya nini kumbe? ikiwa CCM wanataka ipigwe kura ya siri ili wawajue watu wanaopiga kura hiyo kuna haja gani sasa ya kupoteza fedha kununua masanduku ya kura? basi, watu wawe wanapiga mistari nyuma ya wagombea na kuhesabiwa badala ya kubebeshana mizigo ya gharama za kununua masanduku ya kura na makaratasi ya kupigia kura. tangu zamani tumekuwa tukipiga kura za siri na kamati ya kumshauri mwenyekiti kificho imesema kwamba upigaji kura wa aina yoyote(siri au wazi) una nguvu sawa. sasa kwanini tusiegemee kwenye kura ya siri (kama ilivyo kawaida ya upigaji kura tangu enzi za mababu) badala ya kupoteza muda wa watanzania? au kwa kuwa wanaodai kura za wazi ni CCM ndio maana mwenyeketi kificho (mwanaCCM) naye anafuata matakwa ya CCM. ikiwa kura za wazi zina nguvu sawa na zile za siri kwanini basi CCM wang'ang'anie kura za wazi? si wakubali kura za wazi ili mjadala uendelee badala ya kupoteza muda na kuzidi kutafuna pesa za umma? unasemaje kuhusu hili?