BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 397
- 445
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Mwenge wa Uhuru ni moja ya Tunu kubwa iliyopo kwenye Taifa kwani umekua kichocheo kikubwa cha maendeleo kwenye Taifa ikiwemo kuchochea mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini kila mahali unakopita nchi nzima.
"Ni wazi kuwa Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa kichocheo kikubwa katika mapambano dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Aidha Mbio za Mwenge wa Uhuru umekua kichocheo kikubwa cha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwani kupitia Mbio hizi za Mwenge wananchi wanahamasika kubuni, kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo yenye manufaa kwa jamii na uchumi wa maeneo yao."
"Kupitia jumbe mbalimbali za Mwenge wa Uhuru wananchi wamekua wakielimishwa namna bora ya kupambana na adui maradhi, ujinga na umaskini sambamba na kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya dhulma, rushwa, ubadhirifu wa rasilimali."
Kikwete amesema Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii ya Watanzania kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora, kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa ambao ni adui mkubwa wa haki, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI pamoja na madawa ya kulevya.
Kikwete amesema hayo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 zilizofanyika katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha, Mkoani Pwani Jana Jumatano tarehe 2 Aprili, 2025 Mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Philip Mpango.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 zitakimbizwa kwenye mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Visiwani na kufanya shughuli mbalimbali za kuchochea maendeleo na kutoa jumbe mbalimbali za kuhimiza maendeleo na ustawi wa jamii chini ya kauli mbiu ya "JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU."