Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

Ha ha ha! Naona Anne Kilango hana lake pamoja nakuwageuka watanzania. Mwenzie Sophia Simba anakula vya mwisho mwisho kabla ya viti maalum kufikia ukingoni.

Anne Kilango ni aina ya wanafiki wa kutupwa tulio nao.
 
Hii inayoenesha jinsi muungano ulivyo geresha na pia katiba yatu iliyotanda ukungu. Naomba kama kuna mtu mwenye kumbukumbu atujulishe kama ilishawahi tokea kwa mbunge wa Zanzibar kuongoza wizara ya Tanzania bara peke yake.

Relevant question ni: je sheria ya nchi inamruhusu rais kuteua mwakilishi kuongoza wizara ya Tanzania bara?
 
si alisema akimwagwa moshi vijijini itaenda chadema?. Kama ndivyo basi Utabili wake umetimia.
 
MMM na Wengineo;
NI IMANI YANGU UKO SALAMA NA NITAKUWA SIJATENDA KOSA LA JINAI KUTAJA JINA LAKO MMM HAPO, KWANI NIMEFANYA HIVYO KWA NIA NZURI TU NA HASA UKIZINGATIA UELEWA WAKO KWENYE HAYA MAMBO. MMM NA WENGIO NINA MASWALI YAFUATAYO AMBAYO KWA HAKIKA NAHITAJI UFAFANUZI HASA WA KATIBA YETU.

1. Je inawezekana mtu akateuliwa kuwa waziri wakati hajaapishwa kama mbunge? hapa nimelenga kwa Prof. Muhongo, Ms. Mkuya na Ms. Mbene ambao jana na leo ndiyo walipata uteuzi wa Rais na leo wako kwenye Baraza la Mawaziri kabla hawajaapishwa.

2. Je ni halali kwa mbunge wa Zanzibar Dr. Mwinyi kuongoza wizara Bara ambayo siyo ya Muungano? kwani sasa amekuwa Waziri wa Afya.

3. Je nini maoni yako/yenu kuhusu Waziri Mwandosya kutokuwa na Wizara maalumu hasa katika uchumi wetu ambapo gharama za uendeshaji wa Serikali ni kubwa sana.

NB: Haimaanishi wengine wasichangie hii mada. Nyote wenye concern wanakaribishwa pia kuchangia, kwani nchi ni yetu sote.
 
Kwa hii CV mbona sioni DR imetokea wapi?
 
Kutakuwa na Tija gani?au ndiyo kuendeleza Bifu!let him rest in peace!
 
Kawa sekretari wa ikulu sio waziri mkuu
 
Jaman mie nalia na Nagu na malima..safari ya fikra za ukombozi ktk fahamu zetu bado sana

Huwezi jua labda alisomeshwa na marehemu waziri Malima snr.
Mwacheni atoe takrima, after all andiyo sera ya CCM
 

Mkuu haikusaidii chochote wewe kama mwislamu kuwa na waziri mwislamu mwenzako mbambaishaji na asiyeweza kazi. Ndo maana unaona ameamua kumrudisha Kigoda na kuwaacha ndani Shukuru Kawambwa na Malima kupunguza pengo upande huo hauna watu. Tukitoka kwenye dini tutahamia kwenye ukabila. Mimi wasukuma wenzangu wawili wamepigwa chini nami nianze kulalamika? Hapana! Walikuwa wezi na wa mali za umma kwahiyo let them go. Tunataka maendeleo kwa waTZ wote.
 
Hivi Makamba ndiye alikuwa M/kiti aliyesanua noma ya Ngeleja?
Agombee akutane na kichaa cha makamanda
 
Nasubiria bajeti ya wizara isiyokuwa wizara ya waziri asiyekuwa na wizara.
 
Hii inayoenesha jinsi muungano ulivyo geresha na pia katiba yatu iliyotanda ukungu. Naomba kama kuna mtu mwenye kumbukumbu atujulishe kama ilishawahi tokea kwa mbunge wa Zanzibar kuongoza wizara ya Tanzania bara peke yake.

FJM,

..imewahi kutokea.

..Zakhia Meghji ni m-znz na aliongoza wizara ya afya.

..yupo Juma Hamad Omar aliongoza wizara ya utalii enzi za utawala wa mzee rukhsa na akahusika na uharibifu wa mazingira ktk mbuga za wanyama za Tanganyika.

NB:

..hata Mzee Ruksa nadhani aliwahi kuwa waziri wa afya. wenye kumbukumbu naomba msaada wenu.
 
Reactions: FJM
Kawambwa ni dhaifu mno mno. Hana uthubutu hata chembe. Mambo ndani ya wizara yake yanaenda kombo lkn hachukui hatua. Hata anashindwa kuwawajibisha wakuu wa primary wabadhirifu. Udhaifu huu ni wa kiwango cha juu.
Kwa waziri anayeendesha wizara nyeti kama ya elimu, haifai kuwa dhaifu kiwango hiki.
Kawambwa hafai, nasikitika kasalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…