Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania amewafuta kazi
mawaziri waandamizi katika
baraza lake la mawaziri. Katika
mabadiliko hayo, waziri wa
fedha Mustapha Mkullo ni
miongoni mwa waliowekwa
kando.
Mawaziri wapya waliochukua
nafasi mpya kuwapisha
walioachwa ni kama ifuatavyo
(walioachwa majina kwenye
mabano), Waziri wa Nishati na
Madini - Profesa Sospeter
Muhongo (William Ngeleja),
Waziri wa Fedha - Dr William
Mgimwa ( Mustapha Mkullo),
Waziri wa Uchukuzi - Dr
Harrison Mwakyembe (Omar
Nundu), Waziri wa Maliasili na
Utalii - Khamis Kagasheki
(Ezekiel Maige), Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii - Dr
Hussein Mwinyi (Dr Haji
Mponda) na Waziri wa
Viwanda na Biashara - Dr
Abdallah Kigoda (Dr Cyril
Chami).
Ubadhirifu
Kabla ya kusoma orodha hiyo
mpya, Rais Kikwete alisema
majadiliano ya kina
yamefanyika na wenzake kabla
ya kuikamilisha, "Tumeona
wawili kati ya wale tunaweza
kuwahamishia katika wizara
nyingine, lakini tukitazama
baraza zima kwa ujumla wake,
tumewapanga hapa na pale
kuwabadilisha baadhi ya wizara
ili kuimarisha utendaji.
Hatujabadili idadi ya wizara,
tulikuwa na mjadala mkali
kidogo na wa kina kidogo - ipo
rai kuwa wizara hiyo imekuwa
kubwa mno".
Hatua hiyo ni sehemu ya
utekelezaji wa mapendekezo
yaliyotolewa na mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali ambaye alibainisha
hitilafu kadhaa za ubadhirifu
wa fedha za umma kwenye
wizara hizo.
Fedha za umma
Sura nyingi mpya zipo katika
nafasi za manaibu waziri.
Miongoni mwao ni January
Makamba anayechukua unaibu
waziri kwenye Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia,
akina mama wawili Saada
Mkuya Salum akiwa naibu
waziri wa fedha kutokea
Zanzibar bega kwa bega na
mwenzake mpya Janet Mbene
anayesimamia wadhifa huo huo
kwa upande wa Tanzania bara.
Vile vile Rais Kikwete kwa
mara ya kwanza amewateua
manaibu waziri wawili
kusaidiana majukumu kwenye
Wizara ya Nishati na Madini.
Mabadiliko hayo yamekuwa
yakisubiriwa kwa muda tangu
mjadala mkali ulipozuka
bungeni kuwahusu mawaziri
ambao wizara zao zilituhumiwa
kuhusika na ubadhirifu wa kiasi
kikubwa cha fedha za umma.
Hata hivyo Rais Kikwete
amewaeleza watanzania kuwa
kuanzia sasa, uwajibika wa aina
hiyo utawahusu maaafisa
waandamizi wote katika
wizara husika.
ORODHA YA MAWAZIRI NA
NAIBU MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu)Ndugu
Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
(Utawala Bora)Ndugu George
Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(UTUMISHI)Ndugu Celina
Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA
RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais
(MUUNGANO)Ndugu Samia H.
Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais
(MAZINGIRA)Dr. Terezya P.L.
Huvisa, Mb.,
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji na
Uwezeshaji)Ndugu Mary M.
Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (TAMISEMI)Ndugu
Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Ndugu
Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Ndugu Shamsi
Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa UjenziDr. John P.
Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi,
Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Dr. Shukuru J.
Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu
Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa
Kimataifa Ndugu Bernard K.
Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na
Sheria Ndugu Mathias M.
Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Ndugu Emmanuel
Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi Dr. David M.
David, Mb.,
Waziri wa Kazi na
Ajira Ndugu Gaudentia M.
Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof.
Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Prof.
Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa MajiProf. Jumanne
Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara
Maalum Prof. Mark
Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika Eng. Christopher
Chiza, Mb.,
Waziri wa UchukuziDr.
Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dr.
Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na
Utalii Ndugu Khamis
Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na
Biashara Dr. Abdallah O.
Kigoda, Mb.,
Waziri wa FedhaDr. William
Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter
Muhongo, Mb.,
5. NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA
RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu
wa RaisNdugu Charles
Kitwanga, Mb.,
7. OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa,
Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na
AjiraDr. Makongoro M.
Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo,
Chakula na UshirikaNdugu
Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya NchiNdugu Pereira A.
Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na
BiasharaNdugu Gregory G.
Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na UvuviNdugu
Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa
KimataifaNdugu Mahadhi J.
Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,Ndugu Goodluck J.
Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na WatotoNdugu
Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya UfundiNdugu
Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika MasharikiDr. Abdulla
Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na
UtaliiNdugu Lazaro Nyalandu,
Mb.,
Naibu Waziri wa UjenziNdugu
Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii,Dr. Seif
Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na
MadiniNdugu George
Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na TeknolojiaNdugu
January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa UchukuziDr.
Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na
MichezoNdugu Amos Makala,
Mb.,
Naibu Waziri wa MajiEng. Dr.
Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na
MadiniNdugu Stephen Maselle,
Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na
SheriaNdugu Angela Jasmine
Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa FedhaNdugu
Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa FedhaNdugu
Saada Mkuya Salum, Mb.,
Wataapishwa Jumatatu tarehe
8 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi
katika viwanja vya Ikulu