Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

amesema wale walio husika kwa namna moja ama nyingine ( iwe kampuni,mtu binafsi,katibu au mkurugenzi wa wizara) kuvurunda kwa waziri lazima na wao wawajibishwe kwa kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi/kufutiwa kibali/leseni kwa wageni.... Je yeye kama mteuzi wa mawaziri hawajibiki kwa uteuzi mbovu.???
 
Ni janga mkuu mfano Agrey mwanri alipaswa kuwa waziri wa TAMISEMI unapomuweka na huyu mama mwenye kiburi! Sijui tusubiri tuone!
 
Mkitaka kujua kuwa JK ni mzee wa visasi angalia alivyomchinjia mbali Mama Malecela. Juzi tu kamtosa mwanae William Wakati ule alimpiga zengwe mzee Malecela ili asikae magogoni. William badala ya kulalamika na CHADEMA, fanya mpango urudi NY, siasa za JK zitakutia umaskini tu. Mpaka Mbatia kakupiga bao la kete???
 
Baada ya muda hatimaye baraza limetangazwa,nakupa pole Kigwangala kwa sababu umezoea huruma mfano jinsi ulivyopata ubunge,pia siku za hivi karibuni umekua mnafiki kwa kutosaini karatasi za Zitto ukitegemea huruma ya kuwekwa baraza la mawaziri...pole sana ila acha unafiki
 

Mkuu, japo mimi sio mwanasheria, lakini maelezo yako yana-make a lot of sense! Yani kuna logic ndani yake. Ila kwa wale ambao wanaidai Tanganyika yao, hili la Dk.Mwinyi linawapandisha hasira zaidi!
 
pole ya nini sasa wkt nafasi zenyewe hutumi hata barua za maombi au alitoa tamko gan ulilosikia.
 
Kigwagallah alikuwa ana matumain makubwa sana ya kuikamata wizara ya afya kwi! Kwi! Kwi! Kwi!
 
Namshauri Zito asiendele kujishikamanisha na hawa wanafiki akina Kigwangala na Makamba watu walimwambia aache kukaribiana nao yeye akadai hao ni wapiganaji walioweka maslahi ya vijana na taifa mbele lakini ndiyo wa kwanza kuisariti na pia kuipinga hoja yake ambayo ingeleta ukombozi halisi
 
sijiu imekuwaje kuna mtu wa ndani kabisa aliniambia kimwagala alikuwa amepewa uwasiziri pamoja na makamba, masele na Tzeba..Mod wakaichia baharini lakini leo nao yametokea...
 
Nionavyo mimi,baraza jipya la mawaziri lililotangazwa leo limepatikana kwa mtindo wa changanya kete
Ni kama majina yaliandikwa na kuwekwa kwenye kapu,yakavugugwa na yakaanza kutolewa kulingana na Orodha ya wizara.
Mifano michache hii inaweza kuthibitisha hili

Dr Hussein Mwinyi Mbunge toka Zanzibar anapewa wizara ya Afya ambayo si ya Muungano!
Selina Kombani-Tamisemi!
Hawa Ghasia
Mbunge aliyeteuliwa mchana
Mkuchika
Nyarandu
Malima

Ongezea..
Kama kungekuwa na upangaji wa makini tusingeona watu wenye tuhuma kurudi,watu dhaifu kupewa wizara nyeti nk
Wadau mtachangia zaidi
Nawasilisha
 
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

KIVIPI HAPA WAKUU?

Tatizo la wanaJF ni ushabiki na sio reality. Kwanza lazima tutambue kuwa Rais ana haki Kikatiba (ambayo tumeiunda sisi wenyewe) kumteua yeyote kuwa waziri. Vilevile Rais ni binadamu kama binadamu mwingine na si malaika. Hata angemteua mjomba wako bado ungesema yule ambaye si mjomba ni mbaya.

Mimi binafsi nampongeza Mhe. RAIS kwa kutuondolea kero ya mawaziri waliochafuliwa na ripoti ya CAG. Pia kwa kuunda Baraza jipya ambalo binafsi najua litafanya kazi ya Watz.


Waziri asiyekuwa na Wizara maalum.
Kwanza, Hii wizara ilikuwepo siku nyingi
Pili, Prof. Mwandosya ni kichwa kila mtu anajua. Ni watu wachache sana ambao katika mfumo wa elimu hawajasoma (Masters) wakaruhusiwa kusomea (Phd), hivyo serikali inataka kumtumia kwa kazi maalum pale Ikulu kwa maendeleo ya Taifa, wala sio kiraka kama wengi mnavyodhani.

Waziri wa Fedha nimeona CV yake anafaa, Manaibu wake wote wazuri mfano huyu mama Janet anafaa sana tuache umimi na majungu

Waziri wa Ujenzi wote tunamjua

Waziri wa Uchukuzi (Dr. Mwakyembe) wote tunamjua

Waziri wa Africa Masharika wote tunamfahamu

Waziri wa Mambo ya Nje wote tunamfahamu

Waziri wa Makazi wote tunamfahamu


Kwa mtazamo wangu asilimia 80% ya mawaziri ni wazuri tuwaache wafanye kazi tusiwakatishe tamaa na kuwatisha kabla ya kazi.
 
Jamaa alikuwa anaharisha bila sababu pole ndo shukrani ya unafiki
 

Ni mfumo ndio unadetermine ufanisi na sio watu, watanzania ni lini mtakuja kuelewa?
 
pamoja na yote......... wanafiki wana kazi kubwa kuingia cabinet, hawaaminiki
 
jk alitumia nguvu nyingi kumpa ubunge wa nzega,kumbe alijua atamtumia kwenye ufisadi wa stimulus package,msk ilipokea mabilioni yale na hk ni mwanahisa kivuli kwa niaba ya baba mwanaasha!hk ni fisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…