Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012


hapo kwenye blue sijakuelewa kabisa!!
 
hata ushushwe malaika awe mbunge kama ccm ipo madarakani hukuna tumaini lolote linaloweza kupatiana
 
Hawa wawili January Makamba na Simbachawene...........Zile kelele zao Bungeni Zimezaa matunda ila wataishia kama kina Ngeleja na Maige coz nao walikuwa hivyo hivyo
 
Sasa huku kwetu nani ni waziri au mbunge ndani ya Zanzibar???? Huu upuuzi
 
Ushauri wa bure kwa CCM, wasihainge hata kwa nusu saa kusimamisha mgombea Moshi Vijijini 2015. CCM ni bye bye. Umeonaeee jimbo linakwenda kule kusikokua na mizengwe chama makini (CHADEMA)
 
Reactions: FJM

Jamani nawaombeni msaada! hivi usalama wa taifa si uko chini ya utawala bora? kama ni kweli mkuchika anapeleka domo kaya lake usalama wa taifa hivi kweli hiyo ni sawa?
 
Bado ana usanii uleule, na bado anaendelea kuwatetea mawaziri wanaokula rushwa.
 
..Hussein Mwinyi ni mbunge wa Kwahani, Zanzibar.

..hata mimi nimeshangaa kuteuliwa wizara isiyo ya muungano kuiongoza.

..nawaomba Mashekhe wa UAMSHO waje kutuondolea huyu toka ktk wizara yetu wa-Tanganyika.

NB:

..labda kuna mpango wa kuongeza suala la afya ktk mkataba wa muungano.
 
Nimegundua wachangiaji wengi wana udhaifu wa aina fulani, kama mtoto wa kambo hata umfanyie nini anaona anaonewa. Huu ni ushabiki,na tabia ya shabiki hawezi kuisifu timu pinzani. Haya hebu nikiwaambia pangeni nyie hilo baraza kwa wabunge wenu wa CDM itakuwa *&^%$%^& mtupu. Nilidhani mna busara kumbe hamna kitu siku zinavyokwenda mbele ndio mnazidi kuchanganyikiwa. Subirini muone utendaji wao, mnahukumu hata kabla hawajaanza kazi. Kwendeni zenu huko...!!
 
namshukuru rais wangu mh jk kuonesha kuwa katiba si lolote,kwa kumteua uwaziri mtu ambaye hajaapishwa kuwa mbunge ni kinyume na katiba ya sasa ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayodai rais atateua waziri au naibu kutokana na wabunge walio bungeni...sasa Hawa ambao hawajaapa kiapo cha ubunge si kuinajisi katiba??!
 
Ni waziri wa AOB
Sipati picha plate namba ya gari yake sijui wataandikaje
 
Mimi nimeshachoka na huju Kikwete, hana jipya zaidi ya kuiharibu Tanganyika yetu
 
ni Pension Na kusoma magazeti. Unajua hata ubunge wengine kwao ni sehemu ya kupatia pesion sio kuwajibika.
 
JK amenifurahisha kuwapiga chini akina Alhaj na Hijjat na kuwaingiza watu wanaomwabudu Mungu aliye hai eg Mkullo out, Mgimwa ndani.

Tafadhali, usifanye utani na imani za watu. Hii comment yako haifurahishi hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…