Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Huu ni muendelezo wa nyuzi zangu za kiuchumi ambazo ni matokeo ya kutafiti taarifa mbalimbali za serikali kwenye masuala ya fedha na uchumi.
Msukumo wa kuamua kufanya hizi tafiti, unatokana haswa na kuchukizwa na yale majigambo ya wanasiasa na watu wasioelewa mambo, ya eti uchumi kwenye awamu hii ya Magufuli uchumi unakua sana, ilihali namba hazisemi hivyo na zinanuka.
Unaweza kupitia huu uzi hapa ambao, nilijaribu kuweka baadhi ya viashiria vya mdororo mkubwa wa kiuchumi katika kipindi hiki ambacho wasioelewa wamejiingiza kwenye mtego wa kuamini uchumi wetu upo vizuri.
‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?
Lakini, katika kipindi chote hichi cha watu kusifia utendaji kazi wa serikali ya Magufuli na mpaka wengine kufikia hatua ya kutaka Magufuli awe Raisi wa maisha, nimegundua wengi hoja zao zimelenga eneo moja, ambalo kwalo ndio haswa wameweka fikra kwamba hiyo ndo tafsiri halisi ya maendeleo ya kiuchumi.
Mambo kama ujenzi wa mabarabara, flyovers, SGR, Mradi wa umeme, kununua ndege, upanuzi wa bandari, miradi ya maji n.k (uwekezaji kwenye maendeleo ya vitu)
Wengi wa wanaodhani serikali inapiga kazi, wamekuwa haswa wakibabaishwa na maendeleo ya vitu ambayo kwa kiasi fulani serikali ya Magufuli imeyakumbatia sana na nikiri tu kwamba Magufuli na serikali yake wameonesha kuvitilia kipaumbele.
Hizi takwimu hapo juu ni thamani halisi ya ‘non-current assets’ zote zinazomlikiwa na serikali kuanzia mwaka wa fedha 2016 mpaka 2019. Na humo ndani ndo kuna hayo maendeleo ya vitu tunayoyasema ambayo nikiri serikali ya Magufuli wamefanikiwa.
Ndani ya miaka minne iliyopita serikali ya Magufuli imewekeza karibu Trillioni 30 kwenye maendeleo ya vitu ambayo nimejaribu kuyaorodhesha hapo juu.
Ukiangalia kwa makini, maendeleo haya ya vitu ndio haswa imekuwa ni wimbo wa watu wote wanaosifia utendeji kazi wa serikali ya Magufuli, pasi na kuelewa ya kwamba uwekezaji wa serikali kwenye maendeleo ya vitu (miundombinu) ni sehemu moja tu ya mfumo mzima wa uchumi katika nchi yoyote.
Economy = Private Sector Consumption + Investment + Government spending + Trade (Hizi ndizo sehemu kuu za mfumo wa uchumi wowote duniani)
Kwa mtizamo huo wa mfumo wa uchumi, serikali ya Magufuli imeweza tu kufanikiwa kwenye eneo moja la Government Spending kwenye kuboresha maendeleo ya miundo mbinu, lakini kwa wakati huo huo imeshindwa kuchochea ukuaji wa uchumi kwenye sekta binafsi kwenye upande wa private sector economy, Investment and Trade (Import and Export)
Mfano wa kwanza wa kiashiria cha mdororo (importation of intermediate goods)
(Intermediate goods - Transport equipment, Building and construction, Machinery)
Hii chart inaonesha trend ya importation ya intermediate goods kuanzia mwaka 2000 mpaka 2019.
Ki nadharia ya kiuchumi, importation ya intermediate goods inavokuwa kubwa, maana yake ni kwamba uchumi upo vibrant na unakuwa kwa kasi sana. Mfano kama wewe unafanya biashara ya kusaga nafaka, halafu biashara ikiwa inakuendea vizuri, ni lazima utataka uendelee kutengeneza faida kwa kuongeza machine ingine ya kusaga, so hapo ndo mana tunasema ukiona importation ya intermediate goods ipo kubwa ni kwamba uchumi upo vizuri sana.
Ndo mana unaona kwenye utawala wa kikwete 2005-2015 trend ya importation ya intermediate goods ilikuwa inakuwa mwaka hadi mwaka.
Ona uchawi sasa, kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19 trend ya importation ya intermediate goods imekuwa ikienda chini maradufu (kutoka Trillioni 8 mwaka 2014 mpaka sasa Trillioni 6 mwaka 2018/19), na hii inakupa tafsiri ya moja kwa moja kwamba uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ambao umaefanywa na serikali ya Magufuli bado haujazaa matunda ambayo yangetazamiwa. Ikiwa na maana, miundombinu ipo lakini bado haijatoa chachu ya kuongezeka kwa level ya shughuli za kiuchumi kama tulizoshuhudia kwenye utawala wa Rais Kikwete.
Mfano wa pili wa kiashiria cha mdororo (oil imports)
Oil use – Transportation (sea, air, land), industries, construction sectors
Hichi pia ni kiashiria kizito ambacho binafsi kimenishtua sana, haswa ukizingatia kwamba mafuta (oil) ni mali ghafi moja muhimu sana kwenye maendeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote.
Ki nadharia, nchi kama Tanzania inapokuwa inaagiza sana mafuta nje ya nchi ina maana, mahitaji ya mafuta yanakuwa yanaongezeka ambapo kuongezeka huko ni dalili ya kwamba kuna msukumo mkubwa wa kukua kwa uchumi ndani ya nchi. Iki maanisha, kuna ukuaji mkubwa wa sekta ya usafirishaji na viwanda, ambayo ni moja ya sekta chachu kwenye uchumi wa nchi yoyote ile duniani.
Unaweza kushangazwa kwamba, oil imports iliyopo kwenye utawala wa Magufuli ni nusu ya Oil imports ya mwaka 2013/14 ambao naweza kusema ndo ulikuwa mwaka bora wa kiuchumi katika historia ya nchi yetu.
Mwaka 2013/14 pekee Tanzania iliagiza karibu mafuta yenye thamani ya Tzs Trillioni 4.2 wakati mwaka 2018/19 nchi iliagiza mafuta yenye thamani ya Tzs Trillioni 1.8. Hii inakupa haswa taswira ya anguko la kiuchumi lililotokea kwenye nchi yetu kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19.
Ona uchawi sasa - Ni wakati huu huu wa kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19 serikali imetumia Trillioni Zaidi ya 30 kuwekeza kwenye vitu. Kiuchumi baada ya serikali ya Magufuli kuwekeza Zaidi ya Trillioni 30 ndani ya miaka 4, tungetegemea tuone importation ya mafuta ikikua maradufu hata ya kuzidi ile ya mwaka 2013/14.
Lakini kitendo cha importation ya mafuta kudondoka kinakuambia kwamba, bado hakuna output kwenye uwekezaji huu wa trilioni zaidi ya 30 ambao umefanywa kwenye utawala huu wa awamu ya tano.
No offense, kama kuna kitu Magufuli anahitaji kukifanya kunusuru huu uchumi wa hii nchi, ni yeye akutane tu na Kikwete ampatie mbinu za kiuchumi kwa sababu mpaka sasa, hizi mbinu zake za kiuchumi za kuwekeza kwenye Capex wakati sekta binafsi inakufa, haziwezi kuzaa matunda yoyote.
Wasifiaji watasifia sana kwa sababu ya tafsiri fupi ya uchumi ni kitu gani, ila tukiingia kwenye viashiria haswa vya uchumi, uchumi wa kipindi hichi upo hoi bin taabani.
Tubishane kwa hoja, hoja ndizo zinazojenga taifa na sio mikono wala ngumi
N.Mushi