Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
- Thread starter
- #61
Una mengi ya kijifunza ndugu.. inawezekana huelewi background ya vitu nikivyovieleza.Kwanza inabidi ukajifunze "elementary" economics;
Ukitaka ku-import hizo pesa utatoa wapi? Ongelea wewe mwenyewe ukitaka kununua vitu lazima uwe na pesa na wewe kuwa na hiyo pesa lazima ukafanye kazi. Nchi ndiyo hivyo hivyo, lazima watu wafanye kazi nchi ipate pesa. Au watu hao wauze mazao nje ili mpate fedha ya kigeni muagize hayo mafuta. Kama pesa hakuna hapo nchini au mfukoni mwako lazima ukakope. Kwa Tanzania kwa sasa lazima ijikite kwenye export oriented economy na infrastructure investment. Hata kama unakopa na una invest kwenye infrastructure italipa, Tanzania bado inatakiwa ikue. Usikope kulipa mishahara.
Sasa jiulize mwenyewe hizo sectors ambazo Tanzania inaweza kujiimarisha iwe na export oriented economy ni zipi? Pamba isiuzwe, nguo zishonwe ziuzwe ulaya au Marekani, Food processing, fruits etc etc
Hizo data ulizotoa namba zake ndogo sana, huwezi kujenga uchumi kwa namba kama hizo. Unajua Tanzania biashara yake kidunia ni "negligible" ukilinganisha na nchi zingine? Yaani mapato ya Coca Cola cmpany kwa mwaka huwezi kulinganisha na Tanzania. Magufuli anachofanya yupo kwenye right track. Ila utekelezaji wake uwe flexible. Requires agility; yupo too "rigid".
Usianze kumwosha yule mwizi wenu JK kwa propaganda za "ukilaza"; Magufuli is by far the right man, ajirekebishe tu kwa hayo anayokosea, hasa dictatorship.
Miradi ya magufuli ikiisha italipa.
Naona urudi shule kwanza ndo uje tubishane kwa hoja