Kikwete alikuwa genius wa uchumi, Magufuli itabidi akajifunze kwake kama kweli ana nia ya kurudisha uchumi wa Tanzania kwenye reli

Labda hupo nje ya nchi kwa muda mrefu.
Reli ya Dar Moshi hadi Arusha ilikufa,ni miaka zaidi ya 20 imefufuliwa na Mjomba Magufuli.
Reli ya kati ilikuwa mfu anaetembea,leo inafanya kazi imefufuliwa.
Dar tuna train za Makyembe inatusaidia sana.
GSR itakuwa ndio mpango wenyewe wa kukimbiza maendeleo.

Reli ya TAZARA vipi mkuu?? Nayo imekufa au vipi?? Na ile njia ndo inayobeba mizigo zaid ya 40% kutoka bandari ya Dar ila hawatumii reli sie wenye malori ndo tunapata dili za Congo,Zambia,Zimbabwe achilia za Botswana na Malawi kutokea Dar

Kwanini wateja hawapitishi kwenye reli halafu safari ianzie Mbeya~Malawi kwa truck au Songwe(Tunduma)??
 
[emoji853]Uuuwiii
Magufuli angekuwa ana akili watu kama wewe ndyo wakuwapa nafasi katika serikali yake. Tatizo anaweka wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Na nawahakikishieni hao hao ndyo watakaombeza na kumkejeli atakapoondoka huku wakimfaagilia atakayemfata.
 
Reli ya TAZARA vipi mkuu?? Nayo imekufa au vipi?? Na ile njia ndo inayobeba mizigo zaid ya 40% kutoka bandari ya Dar ila hawatumii reli sie wenye malori ndo tunapata dili za Congo,Zambia,Zimbabwe achilia za Botswana na Malawi kutokea Dar

Kwanini wateja hawapitishi kwenye reli halafu safari ianzie Mbeya~Malawi kwa truck au Songwe(Tunduma)??
Mizigo ingesogezwa hadi Mbeya kwa reli,japo sijui vizuri hii reli ya ubia
 
Huu ni muendelezo wa nyuzi zangu za kiuchumi ambazo ni matokeo ya kutafiti taarifa mbalimbali za serikali kwenye masuala ya fedha na uchumi.

Msukumo wa kuamua kufanya hizi tafiti, unatokana haswa na kuchukizwa na yale majigambo ya wanasiasa na watu wasioelewa mambo, ya eti uchumi kwenye awamu hii ya Magufuli uchumi unakua sana, ilihali namba hazisemi hivyo na zinanuka.

Unaweza kupitia huu uzi hapa ambao, nilijaribu kuweka baadhi ya viashiria vya mdororo mkubwa wa kiuchumi katika kipindi hiki ambacho wasioelewa wamejiingiza kwenye mtego wa kuamini uchumi wetu upo vizuri.

‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

Lakini, katika kipindi chote hichi cha watu kusifia utendaji kazi wa serikali ya Magufuli na mpaka wengine kufikia hatua ya kutaka Magufuli awe Raisi wa maisha, nimegundua wengi hoja zao zimelenga eneo moja, ambalo kwalo ndio haswa wameweka fikra kwamba hiyo ndo tafsiri halisi ya maendeleo ya kiuchumi.

Mambo kama ujenzi wa mabarabara, flyovers, SGR, Mradi wa umeme, kununua ndege, upanuzi wa bandari, miradi ya maji n.k (uwekezaji kwenye maendeleo ya vitu)

Wengi wa wanaodhani serikali inapiga kazi, wamekuwa haswa wakibabaishwa na maendeleo ya vitu ambayo kwa kiasi fulani serikali ya Magufuli imeyakumbatia sana na nikiri tu kwamba Magufuli na serikali yake wameonesha kuvitilia kipaumbele.

View attachment 1504944

Hizi takwimu hapo juu ni thamani halisi ya ‘non-current assets’ zote zinazomlikiwa na serikali kuanzia mwaka wa fedha 2016 mpaka 2019. Na humo ndani ndo kuna hayo maendeleo ya vitu tunayoyasema ambayo nikiri serikali ya Magufuli wamefanikiwa.

Ndani ya miaka minne iliyopita serikali ya Magufuli imewekeza karibu Trillioni 30 kwenye maendeleo ya vitu ambayo nimejaribu kuyaorodhesha hapo juu.

Ukiangalia kwa makini, maendeleo haya ya vitu ndio haswa imekuwa ni wimbo wa watu wote wanaosifia utendeji kazi wa serikali ya Magufuli, pasi na kuelewa ya kwamba uwekezaji wa serikali kwenye maendeleo ya vitu (miundombinu) ni sehemu moja tu ya mfumo mzima wa uchumi katika nchi yoyote.

Economy = Private Sector Consumption + Investment + Government spending + Trade (Hizi ndizo sehemu kuu za mfumo wa uchumi wowote duniani)

Kwa mtizamo huo wa mfumo wa uchumi, serikali ya Magufuli imeweza tu kufanikiwa kwenye eneo moja la Government Spending kwenye kuboresha maendeleo ya miundo mbinu, lakini kwa wakati huo huo imeshindwa kuchochea ukuaji wa uchumi kwenye sekta binafsi kwenye upande wa private sector economy, Investment and Trade (Import and Export)

Mfano wa kwanza wa kiashiria cha mdororo (importation of intermediate goods)
View attachment 1504947

(Intermediate goods - Transport equipment, Building and construction, Machinery)

Hii chart inaonesha trend ya importation ya intermediate goods kuanzia mwaka 2000 mpaka 2019.

Ki nadharia ya kiuchumi, importation ya intermediate goods inavokuwa kubwa, maana yake ni kwamba uchumi upo vibrant na unakuwa kwa kasi sana. Mfano kama wewe unafanya biashara ya kusaga nafaka, halafu biashara ikiwa inakuendea vizuri, ni lazima utataka uendelee kutengeneza faida kwa kuongeza machine ingine ya kusaga, so hapo ndo mana tunasema ukiona importation ya intermediate goods ipo kubwa ni kwamba uchumi upo vizuri sana.

Ndo mana unaona kwenye utawala wa kikwete 2005-2015 trend ya importation ya intermediate goods ilikuwa inakuwa mwaka hadi mwaka.

Ona uchawi sasa, kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19 trend ya importation ya intermediate goods imekuwa ikienda chini maradufu (kutoka Trillioni 8 mwaka 2014 mpaka sasa Trillioni 6 mwaka 2018/19), na hii inakupa tafsiri ya moja kwa moja kwamba uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ambao umaefanywa na serikali ya Magufuli bado haujazaa matunda ambayo yangetazamiwa. Ikiwa na maana, miundombinu ipo lakini bado haijatoa chachu ya kuongezeka kwa level ya shughuli za kiuchumi kama tulizoshuhudia kwenye utawala wa Rais Kikwete.

Mfano wa pili wa kiashiria cha mdororo (oil imports)

View attachment 1504951

Oil use – Transportation (sea, air, land), industries, construction sectors

Hichi pia ni kiashiria kizito ambacho binafsi kimenishtua sana, haswa ukizingatia kwamba mafuta (oil) ni mali ghafi moja muhimu sana kwenye maendeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote.

Ki nadharia, nchi kama Tanzania inapokuwa inaagiza sana mafuta nje ya nchi ina maana, mahitaji ya mafuta yanakuwa yanaongezeka ambapo kuongezeka huko ni dalili ya kwamba kuna msukumo mkubwa wa kukua kwa uchumi ndani ya nchi. Iki maanisha, kuna ukuaji mkubwa wa sekta ya usafirishaji na viwanda, ambayo ni moja ya sekta chachu kwenye uchumi wa nchi yoyote ile duniani.

Unaweza kushangazwa kwamba, oil imports iliyopo kwenye utawala wa Magufuli ni nusu ya Oil imports ya mwaka 2013/14 ambao naweza kusema ndo ulikuwa mwaka bora wa kiuchumi katika historia ya nchi yetu.

Mwaka 2013/14 pekee Tanzania iliagiza karibu mafuta yenye thamani ya Tzs Trillioni 4.2 wakati mwaka 2018/19 nchi iliagiza mafuta yenye thamani ya Tzs Trillioni 1.8. Hii inakupa haswa taswira ya anguko la kiuchumi lililotokea kwenye nchi yetu kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19.

Ona uchawi sasa - Ni wakati huu huu wa kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19 serikali imetumia Trillioni Zaidi ya 30 kuwekeza kwenye vitu. Kiuchumi baada ya serikali ya Magufuli kuwekeza Zaidi ya Trillioni 30 ndani ya miaka 4, tungetegemea tuone importation ya mafuta ikikua maradufu hata ya kuzidi ile ya mwaka 2013/14.

Lakini kitendo cha importation ya mafuta kudondoka kinakuambia kwamba, bado hakuna output kwenye uwekezaji huu wa trilioni zaidi ya 30 ambao umefanywa kwenye utawala huu wa awamu ya tano.

No offense, kama kuna kitu Magufuli anahitaji kukifanya kunusuru huu uchumi wa hii nchi, ni yeye akutane tu na Kikwete ampatie mbinu za kiuchumi kwa sababu mpaka sasa, hizi mbinu zake za kiuchumi za kuwekeza kwenye Capex wakati sekta binafsi inakufa, haziwezi kuzaa matunda yoyote.

Wasifiaji watasifia sana kwa sababu ya tafsiri fupi ya uchumi ni kitu gani, ila tukiingia kwenye viashiria haswa vya uchumi, uchumi wa kipindi hichi upo hoi bin taabani.

Tubishane kwa hoja, hoja ndizo zinazojenga taifa na sio mikono wala ngumi

N.Mushi
JK ni level nyingine ndiyo maana hasifii hata haya maigizo yenu
 
Nje ya mada..!

Mleta hoja unaweza ukawa una point za maana sana ila jina lako linatia ukakasi kiasi kwamba linatatiza umakini wa kufiria ulichoandika.
Huenda likawa na maana nzuri huko kwenu, ila kwenye kadamnasi ya waTz jina linakushushia heshima yako.

Yako majina mengi, badili hiyo ID...ni ushauri tu.
Nimekuskia mkuu, ntalifanyia kazi
 
Wewe ni mjinga hujui unachoongea. Kikwete angeongezewa mwaka mmoja tungekuwa uchumi wa kati.angeongezewa mingine 5 tungekuwa tumewapiku wakenya mapema sana.
Upo on point sana, achana na huyo hana hoja ya msingi, kwa ile speed ya uchumi wa kikwete mwaka 2017 tungeshaifikia level ya uchumi wa kati na kuipita.

Trajectory ya uchumi tayari ilikuwa kwenye reli, ilikuwa ndo stage ya take off.
 
Huu ni muendelezo wa nyuzi zangu za kiuchumi ambazo ni matokeo ya kutafiti taarifa mbalimbali za serikali kwenye masuala ya fedha na uchumi.

Msukumo wa kuamua kufanya hizi tafiti, unatokana haswa na kuchukizwa na yale majigambo ya wanasiasa na watu wasioelewa mambo, ya eti uchumi kwenye awamu hii ya Magufuli uchumi unakua sana, ilihali namba hazisemi hivyo na zinanuka.

Unaweza kupitia huu uzi hapa ambao, nilijaribu kuweka baadhi ya viashiria vya mdororo mkubwa wa kiuchumi katika kipindi hiki ambacho wasioelewa wamejiingiza kwenye mtego wa kuamini uchumi wetu upo vizuri.

‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

Lakini, katika kipindi chote hichi cha watu kusifia utendaji kazi wa serikali ya Magufuli na mpaka wengine kufikia hatua ya kutaka Magufuli awe Raisi wa maisha, nimegundua wengi hoja zao zimelenga eneo moja, ambalo kwalo ndio haswa wameweka fikra kwamba hiyo ndo tafsiri halisi ya maendeleo ya kiuchumi.

Mambo kama ujenzi wa mabarabara, flyovers, SGR, Mradi wa umeme, kununua ndege, upanuzi wa bandari, miradi ya maji n.k (uwekezaji kwenye maendeleo ya vitu)

Wengi wa wanaodhani serikali inapiga kazi, wamekuwa haswa wakibabaishwa na maendeleo ya vitu ambayo kwa kiasi fulani serikali ya Magufuli imeyakumbatia sana na nikiri tu kwamba Magufuli na serikali yake wameonesha kuvitilia kipaumbele.

View attachment 1504944

Hizi takwimu hapo juu ni thamani halisi ya ‘non-current assets’ zote zinazomlikiwa na serikali kuanzia mwaka wa fedha 2016 mpaka 2019. Na humo ndani ndo kuna hayo maendeleo ya vitu tunayoyasema ambayo nikiri serikali ya Magufuli wamefanikiwa.

Ndani ya miaka minne iliyopita serikali ya Magufuli imewekeza karibu Trillioni 30 kwenye maendeleo ya vitu ambayo nimejaribu kuyaorodhesha hapo juu.

Ukiangalia kwa makini, maendeleo haya ya vitu ndio haswa imekuwa ni wimbo wa watu wote wanaosifia utendeji kazi wa serikali ya Magufuli, pasi na kuelewa ya kwamba uwekezaji wa serikali kwenye maendeleo ya vitu (miundombinu) ni sehemu moja tu ya mfumo mzima wa uchumi katika nchi yoyote.

Economy = Private Sector Consumption + Investment + Government spending + Trade (Hizi ndizo sehemu kuu za mfumo wa uchumi wowote duniani)

Kwa mtizamo huo wa mfumo wa uchumi, serikali ya Magufuli imeweza tu kufanikiwa kwenye eneo moja la Government Spending kwenye kuboresha maendeleo ya miundo mbinu, lakini kwa wakati huo huo imeshindwa kuchochea ukuaji wa uchumi kwenye sekta binafsi kwenye upande wa private sector economy, Investment and Trade (Import and Export)

Mfano wa kwanza wa kiashiria cha mdororo (importation of intermediate goods)
View attachment 1504947

(Intermediate goods - Transport equipment, Building and construction, Machinery)

Hii chart inaonesha trend ya importation ya intermediate goods kuanzia mwaka 2000 mpaka 2019.

Ki nadharia ya kiuchumi, importation ya intermediate goods inavokuwa kubwa, maana yake ni kwamba uchumi upo vibrant na unakuwa kwa kasi sana. Mfano kama wewe unafanya biashara ya kusaga nafaka, halafu biashara ikiwa inakuendea vizuri, ni lazima utataka uendelee kutengeneza faida kwa kuongeza machine ingine ya kusaga, so hapo ndo mana tunasema ukiona importation ya intermediate goods ipo kubwa ni kwamba uchumi upo vizuri sana.

Ndo mana unaona kwenye utawala wa kikwete 2005-2015 trend ya importation ya intermediate goods ilikuwa inakuwa mwaka hadi mwaka.

Ona uchawi sasa, kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19 trend ya importation ya intermediate goods imekuwa ikienda chini maradufu (kutoka Trillioni 8 mwaka 2014 mpaka sasa Trillioni 6 mwaka 2018/19), na hii inakupa tafsiri ya moja kwa moja kwamba uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ambao umaefanywa na serikali ya Magufuli bado haujazaa matunda ambayo yangetazamiwa. Ikiwa na maana, miundombinu ipo lakini bado haijatoa chachu ya kuongezeka kwa level ya shughuli za kiuchumi kama tulizoshuhudia kwenye utawala wa Rais Kikwete.

Mfano wa pili wa kiashiria cha mdororo (oil imports)

View attachment 1504951

Oil use – Transportation (sea, air, land), industries, construction sectors

Hichi pia ni kiashiria kizito ambacho binafsi kimenishtua sana, haswa ukizingatia kwamba mafuta (oil) ni mali ghafi moja muhimu sana kwenye maendeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote.

Ki nadharia, nchi kama Tanzania inapokuwa inaagiza sana mafuta nje ya nchi ina maana, mahitaji ya mafuta yanakuwa yanaongezeka ambapo kuongezeka huko ni dalili ya kwamba kuna msukumo mkubwa wa kukua kwa uchumi ndani ya nchi. Iki maanisha, kuna ukuaji mkubwa wa sekta ya usafirishaji na viwanda, ambayo ni moja ya sekta chachu kwenye uchumi wa nchi yoyote ile duniani.

Unaweza kushangazwa kwamba, oil imports iliyopo kwenye utawala wa Magufuli ni nusu ya Oil imports ya mwaka 2013/14 ambao naweza kusema ndo ulikuwa mwaka bora wa kiuchumi katika historia ya nchi yetu.

Mwaka 2013/14 pekee Tanzania iliagiza karibu mafuta yenye thamani ya Tzs Trillioni 4.2 wakati mwaka 2018/19 nchi iliagiza mafuta yenye thamani ya Tzs Trillioni 1.8. Hii inakupa haswa taswira ya anguko la kiuchumi lililotokea kwenye nchi yetu kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19.

Ona uchawi sasa - Ni wakati huu huu wa kuanzia mwaka 2015/16 mpaka 2018/19 serikali imetumia Trillioni Zaidi ya 30 kuwekeza kwenye vitu. Kiuchumi baada ya serikali ya Magufuli kuwekeza Zaidi ya Trillioni 30 ndani ya miaka 4, tungetegemea tuone importation ya mafuta ikikua maradufu hata ya kuzidi ile ya mwaka 2013/14.

Lakini kitendo cha importation ya mafuta kudondoka kinakuambia kwamba, bado hakuna output kwenye uwekezaji huu wa trilioni zaidi ya 30 ambao umefanywa kwenye utawala huu wa awamu ya tano.

No offense, kama kuna kitu Magufuli anahitaji kukifanya kunusuru huu uchumi wa hii nchi, ni yeye akutane tu na Kikwete ampatie mbinu za kiuchumi kwa sababu mpaka sasa, hizi mbinu zake za kiuchumi za kuwekeza kwenye Capex wakati sekta binafsi inakufa, haziwezi kuzaa matunda yoyote.

Wasifiaji watasifia sana kwa sababu ya tafsiri fupi ya uchumi ni kitu gani, ila tukiingia kwenye viashiria haswa vya uchumi, uchumi wa kipindi hichi upo hoi bin taabani.

Tubishane kwa hoja, hoja ndizo zinazojenga taifa na sio mikono wala ngumi

N.Mushi
Lo. Umepotosha sana, yaani theory zako za uchumi ni tofauti na ulivyosema. Haiwezekaniki. Na vilaza wenzio wengi wamekuunga mkno.
Yaani nchin kuwa na importation kubwa uchumi ndiyo unakua? Kuwa na deficit uchumi unakua au kuwa na surplus?

Magufuli yupo right:
Infrastructure investment - SGR kama watu watapanda wengi na kutumia train basi italipa - uchumi unakua, utasaidia people and goods movements ie logistics etc.
Ndege watu wengi wasafiri, more money italipa
Stieglers gorge - 2000 MW, matumizi ya umeme yatakua, viwanda, extraction of metals etc
Roads - Yes easier and convenient movement of goods
Madini - he has done wonders

Problem ya Magufuli ni
1. Construction industry inabidi aiweke mikoni mwa watu wake wazawa na private sector. All investments must be translated to the CSR model
2. Freedom of creativity and innovation,
3. Uhuru wa habari na democracy.

Comment zako zimeungwa mkono na wengi mno, na hii inaonyesha jinsi gani nchi yetu vilaza ni wengi!!!!
 
Baada ya mapitio ya siku 12 na kupata ushauri kutoka kwa wababe wa siasa uchumi, kilicho onekana ni kuwa bado tuna tatizo la kuweza kuendesha uchumi wa kibepari and the following is what was observed:

Capitalism is widely blamed for a range of social and economic woes. Both socialists and capitalists blame each other for the rise of crony capitalism. Socialists believe that crony capitalism is the inevitable result of pure capitalism. On the other hand, capitalists believe that crony capitalism arises from the need of socialist governments to control the economy.

In practice, this is the dominant form of capitalism worldwide due to the powerful incentives both faced by governments to extract resources by taxing, regulating, and fostering rent-seeking activity, and those faced by capitalist businesses to increase profits by obtaining subsidies, limiting competition, and erecting barriers to entry. In effect, these forces represent a kind of supply and demand for government intervention in the economy, which arises from the economic system itself.

I have apackage of the serious discussion which made our country to follow current discourse.
Pigilia msumari kwenye paragraph yako namba moja.

Umetoa point moja kali sana ya tafakuri, na hii naomba tukipata siku tuifanyie tathmini ya kina

"bado tuna tatizo la kuweza kuendesha uchumi wa kibepari"

Hoja ni: Policy makers wa Tanzania wafanye nini ili waweze kuendesha uchumi wa kibepari??
 
Mimi naamini kwenye long term investments zitakuwa zimefanyiwa input/output na cost/ benefit analysis kwenye feasibility study. Miradi km SGR ni muhimu kama tunataka uchumi wa kisasa na unaohimili ushindani kikandana dunia na wenye kuvutia wawekezaji lazima uwekeze kwenye vichocheo vya uchumi. Uchumi huishi katika mnyororo na mduara hutegemeana. Lets be patient for the benefits
Nijibu kwanza haya maswali

1. Unaweza kukaa bila kula chochote kwa siku saba?

2. Je unaweza kujua ni kitu kitatokea baada ya mwaka mmoja unaokuja?

Mantiki ya kukuuliza hivo ni kwamba, usiwe mtumwa wa kudhani kwamba hivo unavoviita long term basi vitakuwa na manufaa kwenye long term. Uncertainties zipo nyingi sana kwenye mambo ya kiuchumi, na mambo hubadilika.

Ndo mana kwenye uchumi wowote lazima kuwe na balance ya kuhakikisha wakati nchi ina pursue long term investments kama za miundombinu mikubwa, isiwe ndo kikwazo cha kudumaza uchumi wa sasa.
 
Lo. Umepotosha sana, yaani theory zako za uchumi ni tofauti na ulivyosema. Haiwezekaniki. Na vilaza wenzio wengi wamekuunga mkno.
Yaani nchin kuwa na importation kubwa uchumi ndiyo unakua? Kuwa na deficit uchumi unakua au kuwa na surplus?

Magufuli yupo right:
Infrastructure investment - SGR kama watu watapanda wengi na kutumia train basi italipa - uchumi unakua, utasaidia people and goods movements ie logistics etc.
Ndege watu wengi wasafiri, more money italipa
Stieglers gorge - 2000 MW, matumizi ya umeme yatakua, viwanda, extraction of metals etc
Roads - Yes easier and convenient movement of goods
Madini - he has done wonders

Problem ya Magufuli ni
1. Construction industry inabidi aiweke mikoni mwa watu wake wazawa na private sector. All investments must be translated to the CSR model
2. Freedom of creativity and innovation,
3. Uhuru wa habari na democracy.

Comment zako zimeungwa mkono na wengi mno, na hii inaonyesha jinsi gani nchi yetu vilaza ni wengi!!!!
Namba hazidanganyi, weka stats za namba kama alivyoweka mwenzako kuonesha kwamba hivyo ndivyo au laah we ndiye kilaza zaidi.
 
1. Lo. Umepotosha sana, yaani theory zako za uchumi ni tofauti na ulivyosema.

2. Yaani nchin kuwa na importation kubwa uchumi ndiyo unakua? Kuwa na deficit uchumi unakua au kuwa na surplus?

Umeandika bla bla nyingi sana, naomba uwe mtulivu nikujibu hizi point mbili ambazo naona kabisa zinakufanya unazidi kutopea kwenye dimbwi la ujinga.

Kwanza, mimi similiki theory za kiuchumi, kwa hiyo sio sahihi kusema "theory zako" kama ulivyoanza hapo mwanzo.

Kingine, nataka nikuelimishe ni vipi importation kwenye bidhaa za intermediate goods na oil ni kiashiria kikubwa sana cha uchumi.

Kuwa makini, sijasema importation ya kama jumuishi ya bidhaa zote zinazoingia nchini, nime specify "intermediate goods" na "oil" nadhani hapa ndo ntakuwa nimekuacha bila bila.

Ki uhalisia kabisa, hakuna nchi inaweza ku operate uchumi wake bila kuwa na intermediate goods na oil. Hizi ni drivers za uchumi wa nchi yoyote ile, hususani nchi kama Tanzania ambayo haipo self sufficient kwenye hizo bidhaa.

Hivyo basi inakuwa ni rahisi kupima performance ya uchumi kwa ku track level ya importation ya hizi bidhaa.

Nadhani nimetumia lugha rahisi sana kukuelewesha, siku ingine usiwe mtu wa kupinga pinga tu, kuwa mtulivu upate maarifa.
 
Magufuli amejenga miundombinu ambayo ikikamilika ndo tutaweza kumtathimini ila sasa imetosha!! mamilioni ya watu walikuwa matajiri wakati wa Kikwete ila sasa ni maskini wa kutupwa familia nyingi zinalala njaa, sasa miaka yake mitano ijayo namshauri ahamasishe ukuaji wa sekta binafsi kupitia punguzo la kodi na kuruhusu NGO zikue maana sasa zimebanwa na zinauwawa na serikali , kampuni binafsi zinakufa kwa kasi sheria lukuki na kodi ya kufuru, akiweka sera za kuamsha sekta binafsi ndo hapo kila mtu atamsifia kwa nyimbo na mapambio! kawaida ya wabongo ni kukusifia ukiwa madarakani ukitoka wanakuponda!!
 
Nenda kwenye swali moja kwa moja mkuu sote tunajua bepari ni nani.
Any Government is a capitalist number one. They hold capital larger than many citizens in the country. So the prudent economic decision of investing in high output projects can determine the proper growth of the economy. Informed from the same, when talking of investment you should know that the government must be on the Stirling wheel to remove all economic distortions
 
Pigilia msumari kwenye paragraph yako namba moja.

Umetoa point moja kali sana ya tafakuri, na hii naomba tukipata siku tuifanyie tathmini ya kina

"bado tuna tatizo la kuweza kuendesha uchumi wa kibepari"

Hoja ni: Policy makers wa Tanzania wafanye nini ili waweze kuendesha uchumi wa kibepari??
Naantombe Mushi, asante sana lakini nakimbia kijijini Kirongwe, Mwanga, Kilimanjaro. Tutachangia siku nyingine.
 
Umeandika bla bla nyingi sana, naomba uwe mtulivu nikujibu hizi point mbili ambazo naona kabisa zinakufanya unazidi kutopea kwenye dimbwi la ujinga.

Kwanza, mimi similiki theory za kiuchumi, kwa hiyo sio sahihi kusema "theory zako" kama ulivyoanza hapo mwanzo.

Kingine, nataka nikuelimishe ni vipi importation kwenye bidhaa za intermediate goods na oil ni kiashiria kikubwa sana cha uchumi.

Kuwa makini, sijasema importation ya kama jumuishi ya bidhaa zote zinazoingia nchini, nime specify "intermediate goods" na "oil" nadhani hapa ndo ntakuwa nimekuacha bila bila.

Ki uhalisia kabisa, hakuna nchi inaweza ku operate uchumi wake bila kuwa na intermediate goods na oil. Hizi ni drivers za uchumi wa nchi yoyote ile, hususani nchi kama Tanzania ambayo haipo self sufficient kwenye hizo bidhaa.

Hivyo basi inakuwa ni rahisi kupima performance ya uchumi kwa ku track level ya importation ya hizi bidhaa.

Nadhani nimetumia lugha rahisi sana kukuelewesha, siku ingine usiwe mtu wa kupinga pinga tu, kuwa mtulivu upate maarifa.
Kwanza inabidi ukajifunze "elementary" economics;
Ukitaka ku-import hizo pesa utatoa wapi? Ongelea wewe mwenyewe ukitaka kununua vitu lazima uwe na pesa na wewe kuwa na hiyo pesa lazima ukafanye kazi. Nchi ndiyo hivyo hivyo, lazima watu wafanye kazi nchi ipate pesa. Au watu hao wauze mazao nje ili mpate fedha ya kigeni muagize hayo mafuta. Kama pesa hakuna hapo nchini au mfukoni mwako lazima ukakope. Kwa Tanzania kwa sasa lazima ijikite kwenye export oriented economy na infrastructure investment. Hata kama unakopa na una invest kwenye infrastructure italipa, Tanzania bado inatakiwa ikue. Usikope kulipa mishahara.
Sasa jiulize mwenyewe hizo sectors ambazo Tanzania inaweza kujiimarisha iwe na export oriented economy ni zipi? Pamba isiuzwe, nguo zishonwe ziuzwe ulaya au Marekani, Food processing, fruits etc etc

Hizo data ulizotoa namba zake ndogo sana, huwezi kujenga uchumi kwa namba kama hizo. Unajua Tanzania biashara yake kidunia ni "negligible" ukilinganisha na nchi zingine? Yaani mapato ya Coca Cola cmpany kwa mwaka huwezi kulinganisha na Tanzania. Magufuli anachofanya yupo kwenye right track. Ila utekelezaji wake uwe flexible. Requires agility; yupo too "rigid".

Usianze kumwosha yule mwizi wenu JK kwa propaganda za "ukilaza"; Magufuli is by far the right man, ajirekebishe tu kwa hayo anayokosea, hasa dictatorship.
Miradi ya magufuli ikiisha italipa.
 
Back
Top Bottom