MAMBO 10 YA KIPEKEE USIYOYAJUA KUHUSU BERNARD KAMILIUS MEMBE.
Tunaendelea tulipoishia..
Hii ni "episode" ya tano katika mwendelezo wa "series" yetu juu ya historia na wasifu wa mwanasiasa na mwanadiplomasia wa muda mrefu Bernard Kamilius Membe.
Kama nilivyoeleza katika "episode" iliyopita.Leo kwa kifupi sana nitajikita katika kuzungumzia mambo 10 ya kipekee usiyoyajua kuhusu Bernard Kamilius Membe.
Ungana nami kama ifuatavyo:
1.Bernard Kamilius Membe ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa baba na mama yake.Kabla ya mdogo wake ambaye ndiye anajulikana kumfuatia kuzaliwa aitwaye Ester(marehemu)kulikuwa na wadogo zake watano waliomfuatia kuzaliwa lakini kwa bahati mbaya wote walifariki kabla ya kuzaliwa.Kwahiyo kama wadogo zake hawa wangeishi leo hii familia yao ingekuwa na watoto 12 na sio 7 idadi ambayo nayo imepungua na kubaki watoto 5 kwasababu tayari kaka yake Simon na mdogo wake Ester wameshatangulia mbele za haki.
2.Bernard Kamilius Membe alipofikisha miaka mitano alipelekwa na wazazi wake wilaya Ruangwa kwa ajili ya kumsalimia babu yake upande wa baba yao.Alipofika kule wakati katoka nje kucheza na watoto wenzake mmoja wa mashuhuda(mtoto waliyekuwa wanacheza naye)alimwona bibi mmoja kutoka katika moja ya nyumba za jirani akimwita Bernard Kamilius Membe na kumpatia mhindi ili aule.Baada ya kuula ule mhindi alianza kulalamika kuumwa tumbo na hakuchukua muda alizimia.Baada ya kuzimia familia yake ilimpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu ikagundulika ule mhindi ulikuwa na viashiria vya sumu.Alipatiwa matibabu lakini hakuamka kwa zaidi ya siku 5.
3.Bibi mzaa baba wa Bernard Kamilius Membe alifariki kwa kuuawa kisha kuliwa na simba.Tukio hili lilimkuta akiwa shambani analima tena akiwa na wanaye ambapo baba yake Bernard Kamilius Membe alikuwa na miaka mitatu wakati kaka yake yaani baba yake mkubwa Bernard Kamilius Membe alikuwa na miaka saba.Kaka mtu alipoona mama yao kavamiwa na simba alimbeba mdogo wake na kukimbia kijijini kuwajulisha wanakijiji kuwa mama yao kavamiwa na simba.
4.Baada ya kumaliza kidato cha nne katika shule ya seminari Namupa iliyopo mkoani Lindi Bernard Kamilius Membe pamoja na mwenzake Paul Maokola ambaye ndiye alikuwa msimamizi wa miradi ya maendeleo jimbo la Mtama wakati wa ubunge wake kwa vipindi viwili(2005-2010 na 2010-2015)walichaguliwa kwenda kusomea upadri kwenye seminari ya Peramiho wakati wakisubiri majibu yao.
5.Baba yake Bernard Kamilius Membe alifariki kwa ajali ya bunduki wakati anawinda.Alijikwaa kwenye kichuguu na kutereza wakati ameikoki bunduki yake nayo ikamfyatukia.Alivuja damu kwa zaidi ya masaa matatu na hospitali ilikuwa mbali sana na kijiji chao.Alipofikishwa hospitali hakukaa sana alifariki.
6.Bernard Kamilius Membe alikuwa na ndoto za kufanya kazi benki.Na hii ilimfanya achague masomo ya uchumi yaani HGE kidato cha tano na sita.Kumbe Mungu alimpangia kazi tofauti na aliyoitegemea.Yeye akaenda kuwa mtumishi wa "ofisi nyeti" alafu rafiko yake wa karibu(Paul Maokola)tangu wanasoma O Level pale Namupa Seminari ndio akaajiriwa benki hadi alipostaafu na kisha Bernard Kamilius Membe akamwajiri tena kama msimamizi wa miradi ya maendeleo jimbo la Mtama.
7.Bernard Kamilius Membe ni "classmate" wa Dk.Bernard Achiula(Mkurugenzi wa chuo cha diplomasia-Kurasini).Walisoma wote Namupa Seminari.Ni Bernard Kamilius Membe ndiye aliyemfuata nchini Ujerumani na kumwomba aje kushiriki ujenzi wa taifa lake katika masuala ya diplomasia.Dk.Bernard Achiula ni miongoni mwa wabobezi wa masuala ya diplomasia.
8.Bernard Kamilius Membe amewahi kufundisha kwa muda mfupi shule ya sekondari Lindi baada ya kumaliza kidato cha sita.Alikuwa ni mwalimu wa kujitolea.
9.Bernard Kamilius Membe ni mwanasiasa wa kwanza mwenye asili ya kabila la Wamwera kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama kuwa mbunge.
10.Akiwa kwenye kozi ya "masuala nyeti" nchini Uingereza katika chuo cha Scotland Yard alikutana na rais wa sasa wa Zimbabwe Komredi Emmerson Dambudzo Mnangagwa(The Crocodile).Wote walichaguliwa kusoma kozi moja.Na huu ndio ukawa mwanzo wa ukaribu wao ambao umedumu kwa miongo kadhaa sasa.Kwa wachache wasiofahamu ni kwamba Komredi Emmerson Dambudzo Mnangagwa(The Crocodile)amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa "ofisi nyeti" ya Zimbabwe.
Je unajua Jen.Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe walielekezwa na Mwl.Julius Kambarage Nyerere kumwajiri Jack Steven Gotham kwenye "ofisi nyeti"?.
Tujumuike tena pamoja kesho kwenye muda kama huu.......