Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl. Nyerere, Sehemu ya tatu (3)

Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl. Nyerere, Sehemu ya tatu (3)

Kuweka record sawa.
Urambo iligawanywa mwaka 1995 na kuwa majimbo mawili ya urambo mashariki na urambo Magharibi.
Mwaka 1995 urambo Mashariki ilichukuliwa na NCCR MAGEUZI mbunge akiwa Abraham Msina huku Kapuya akishinda Urambo Magharibi.

Mwaka 2000 Urambo Mashariki ilirudi tena CCM baada ya ALI AMANI KARAVINA kushinda kwenye uchaguzi mkuu kutokana na mvutano wa CUF na NCCR MAGEUZI.

Kinachonitatiza mpaka nikauliza swali langu ni kwamba record hazionyeshi kama Mzee Sitta aliwahi kushiriki katika chaguzi hizo mbili za 1995 na 2000.
Mzee Sitta alikuwa mbunge wa Urambo toka 1975 mpaka 1995.
1995 aliangushwa kwenye kinyang'anyiro na Prof. Juma Athumani Kapuya. Rais Mkapa akamteua kuwa boss wa TIC
Then 2005 Urambo iligawanywa kuwa majimbo mawili. Urambo mashariki (ambapo Sitta akarejea tena Bungeni) na urambo magharibi (ambalo kwa sasa ni jimbo la kaliuwa ambalo lilishikiliwa na Prof. Kapuya kabla hajapigwa chini na Magdalena Sakaya)

Huenda mtoa mada akaja na clarifications kutetea hoja yake. Maana kwa sasa tubaki kwenye hoja ya JK na BKM kama anavyokuja na epsiode ya 4 leo
.
 
Sioni busara kuleta masuala ya kidini kwenye Utanzania. Maana dini kubwa mbili zilikuja na Waarabu walioleta utumwa na Wazungu walioleta ukoloni.

Tanzania huenda isingekuwa na hizi dini kama sio Waarabu na Wazungu.

Tukibaki kwenye hoja ya CV. Kuna wakati CV inatizamwa kwa jicho la Elimu. Na kuna wakati inatizamwa kwa jicho la uzoefu na muda wa kuwa katika siasa au kazi.
Tukichukua la pili kama kigezo cha CV, bila shaka John Malecele (Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais 1990-94) alikuwa na sifa kubwa kuliko JK. Bila shaka alipungukiwa na uadilifu ndiyo maana alipoteza Uwaziri Mkuu ana alikatwa 1995 & 2005.
Pia kama ni uzoefu, Joseph Sinde Warioba (Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Raus 1985-90; Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa muda mrefu kabisa kama sikosei 1972-1985)

Wote hao wawili bila shaka walikuwa na sifa in term of CV kuliko Mkapa au JK; ila 5 bora hawakuvuka. Hakuna aliezua agenda ya udini
Mtu ambaye alikuwa overqualified alikuwa S.A.S.
 
Safi sana, haya mambo ndo tunayoyataka hapa JF

Kwa kuongezea tu, Baada ya JK na watu wake kwenda msasani kwa mwalimu, walimkuta mwalimu na watu pale anaongea nao, baada ya kusikiliza nia yao na kuwabariki wakagombee.

Hata hivyo mwalimu alikuwa na wazo tofauti kichwani, akakata shauri la kwenda Dodoma kuthibiti nguvu yao maana aligundua kuwa bila kuwadhibiti wangechukua nchi!

Hata kwenye kupiga kura ndani ya CCM kati ya BWM na JK, Mwalimu alifanya kampeni ya kuandika vimemo kwa mkono wake akiwaomba wajumbe wa Zanzibar wamuunge mkono BWM.

Lakini ukiacha hilo, baada ya JK kumgalagaza Msuya na BWM kwenye round ya hao watatu, Mwalimu alivunja kanuni za CCM kwa kulazimisha kura zipigwe kati ya BWM na JK wakati kitu hicho hakikuwemo ktk kanuni, Yaani ilipaswa JK atangazwe tu kuwa mgombea maana yeye ndo aliibuka kidedea dhidi ya wote kwenye mkutano mkuu
Duh!.
 
Kingine ambacho nimesahau kuweka record sawa.
Mtoa mada pia anafanya upotoshaji wa kujua wa bila kujua.

Mwaka 1995 kati ya wagombea watatu wa mwisho waliopigiwa kura na mkutano mkuu CCM walikuwa ni
Lt. Col. Jakaya Mrisho Kikwete (Waziri wa Fedha wakati huo)
Mhe. Benjamin W. Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia)
Mhe. Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais)

Kama nilivyopangilia; JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na Mkapa then Msuya akawa wa 3.

Kwa kuwa katiba ya CCM iko wazi, mjumbe anaepata zaidi ya asilimia 51 ya wajumbe anapita moja kwa moja. Ndiyo maana JK alipopata wingi wa kura zaidi ya 51% mwaka 2005, akasema "safari hii kura zimetosha"

Hakuna aliemfanyia mizengwe JK 1995; unless kama kuna jambo ambalo mtoa mada analo alete ushahidi. Ila katiba na taratibu za CCM zinafahamika. Na kwa wale tuliokuwepo tukifuatilia, tunasikitika kuona mtu ana hadaa mchana peupe.

Muandishi, nakushauri ufanye homework. Ili hata kama unadanganya basi uongo wako usiwe too obvious.

JF ni great thinkers forum. It is very shameful to write white lies
Pia Mwalimu alikuwa haandiki vikaratasi ukumbini Chimwaga. Kama humfahanu Mwalimu kaa kimyaa. Kampeni ilifanyika wakati wa chakula cha mchana maana kura ya mwisho ilifanyika baada ya mapumziko wakati wa chakula cha mchana. Kama unajua basi simulia nani walifanya hilo vurugu la mchana!
 
Kumbe sarakasi zilianza zamani Sana!!
 
Kwanini huu uzi umefufuliwa tena!?kuna nini kinaendelea!?

Au jasusi mbobezi ANATAKA kunuka Baada ya kushindwa kunuka kipindi cha simba wa yuda!!?
 
Pia Mwalimu alikuwa haandiki vikaratasi ukumbini Chimwaga. Kama humfahanu Mwalimu kaa kimyaa. Kampeni ilifanyika wakati wa chakula cha mchana maana kura ya mwisho ilifanyika baada ya mapumziko wakati wa chakula cha mchana. Kama unajua basi simulia nani walifanya hilo vurugu la mchana!
Jakaya alitumika kumdhibiti malima,hapakua na mpango wa yeye kuwa rais, nyerere alifanya vikao na mkapa na ndiye aliyekua mlengwa,jakaya alishtuka baadae,Bara na visiwani hutoa wajumbe idadi sawa, visiwani wote waislam ukijumlisha na WA bars,kwa vuguvugu la dini lilikuwepo wakati huo 'deep state's ikaona imtumie jakaya
 
Sijui kama unaelewa unachoandika. JK alikuwa mgombea urais. Asubuhi aliongoza kura, alasiri aliangushwa na Mkapa.
 
Kwa hiyo Nyerere baada ya yeye kutawala miaka 23, akatuchagulia Mwinyi na Mkapa wa kututawala miaka 20 mingine. Kweli yule mzee alitupatia.
 
Kwa hiyo Nyerere baada ya yeye kutawala miaka 23, akatuchagulia Mwinyi na Mkapa wa kututawala miaka 20 mingine. Kweli yule mzee alitupatia.
Mwinyi halikua chaguo lake,akipigwa dafrao na Kambi ya jumbe wakilipiza alichowafanyia kule nyuma
 
Back
Top Bottom